Caught on Tape: Mkakati wa Mamluki wafichuliwa!

Status
Not open for further replies.
Tetesi ni kitu kisicho na ushahidi, kama wanazushiwa waende mahakamani... na huu ni mpango mmoja tu mwingine unahusisha watu wasomi zaidi na very senior na una angle ile ile.. huo utaibuka wiki ijayo Inshallah..

Yalikuwa ni maoni tu, maana wingu linaweza kusafishika na kukawa na tofauti kubwa au ndogo na hayo yaliyojiri. Maana sasa hivi inasemekana kuna juhudi maalum za kuhakikisha suala la EPA linapotea katika kurasa za mbele za magazeti na vipindi vya redio na TV. Juzi tuliona kikao cha CC ambacho mpaka sasa hakijapewa kipaumbele katika habari muhimu nchini kama ilivyotarajiwa.
 
Asante Mwanakijiji K wa taarifa hii amabayo imekuja wakati muhimu sana,

Siku zote nimekuwa nikiwaasa wenzangu waislamu na wakrisito kuwa tusiruhusu umoja wetu na undugu wetu uingiliwe na watu amabao wameshindwa kuongoza nchi. Nyerere angekuwa na mawazo ya udini tusingekuwa hapa tulipo

Kinachoniumiza moyo ni kuwa nakumbuka tukiwa watoto, wazazi wangu wakristo walikuwa hawaruhusu mtu yeyote asiye muislamu kuchinja kuku, tuliamini kuwa waislamu ni ndugu zetu mara watakapobisha hodi watakuja na kula sote-kwani wao hawali kibudu, kwani tuliheshimu na tunaheshimu dini yao

Nakumbuka pia kipindi cha Ramadhani , Idi Maulidi n.k tulijipitisha pitisha kando ya waislamu ili tupate pilau, na tulikaribishwa tukala,

Sijazungumzia kuhusu ndugu na shemeji zangu wengi walio waislamu....marafiki, walimu....wafanya kazi wenzangu

Huwezi kumtofautisha mwislamu na Mkristo Tanzania, hali hii imewashangaza wengi wa nje.Undugu uliojengeka ni mkubwa mno kuliko fedha yeyote tutakayopewa na mtu yeyote ili atugawe, ni afadhali basi tukaishi na umaskini wetu katika upendo huu tulio nao kuliko tukawa matajiri wenye uadui na chuki, by the way misaada kama hiyo tangu tumeanza kupokea haijabadilisha maisha yetu, tumeona wachache wakifaidi. tuna akili, mali, uwezo, umoja, tuna kila sababu ya kuendelea bila kumtegemea mtu yeyote wa adini yeyote kati ya dini zaidi ya 1000 hapa duniani..

Leo anapotokea mtu akaingiza mambo yeyote ya kutugawa ni shetani huyo, hafai huyo, tumpinge huyo....ONA SASA WANAUMBUKA MCHANA KWEUPEEEEEEEE

HAWA NI MAADUNI WA TAIFA ISAMBAZENI TAARIFA HII, HAWA NI WABAYA KULIKO WEZI WA EPA, RICHMOND N.K

MUNGU IBARIKI TANZANIA
waberoya
 
wiki iliyopita nilidokeza kuhusu "mgongano" utakaotokea mwishoni mwa juma. Namalizia kuandika ripoti yangu na nitawawekea hapa muda si mrefu ujao kama "Exclusive News".. majina yatatajwa... stay tuned..

Ti!!! Ti!!!!!! Tittt... hivi sasa ni saa!!!!!!!!!!!!
 
Hii habari kwa kweli inasikitisha sana! Yaani uongozi wetu umetufikisha hapa! Lazima tuikatae hali hii waislam kwa wakristo! Mungu huyu mmoja tunayemuabudu na atuipushe na hili! Viongoziviongozi! Chonde jamani!
 
waislamu na wakristo kataeni kutumiwa..tusifikie mahali ambapo mtu akipewa uongozi akiona uungwaji mkono unashuka na mambo hayaendi ...aanze kusingizia kuwa ..ukweli unapindishwa kwa ajili ya dini au kabila lake..na aanze mfano kwenda kanisani au msikitini kusema ..""aah ndugu zangu mnajuwa mambo ni safi lakini hawa wananichafua kwa sababu tuko wote hapa tunaashiriki.." no...hatujafika huko....

....tukifikia huko hata rais aatashindwa kutawala ....maana hata akimfukuza mtu kazi kwa kula rushwa ie kama lowassa alivyoondolewa...amgeweza kwenda pale azania front ..na kusema...hii richmond ni geresha ...wamenifukuza kwa kuwa nasali hapa.....au mwaka 1995..kikwete angesema ...aah nimeshinda lakini wamekataa kunitangaza kwa sababu ya dini yangu..

no lets work..failure has nothing to do with race,religion,tribe or colour....
 
Huu ndio unafiki wa chama chenu mnachoking'ang'ania, haya na leo nendeni mkajipongeze. Hii tabia ya kuuma na kupuliza itatumaliza watanzania. Haya sasa tuone watakaoruka vihunzi na kukikana chama cha wanafiki. Haijalishi ni mambo ya dini zote kila moja ikitaka kuwaoverule nyingi pamoja na ukabila wa kichinichini, iko siku utalipuka kisawasawa hii nchi isambaratike....the root cause ni hicho chama chenu chenye uchu wa madaraka kilichojaa mafisadi ....mfyuuuuuu.
 
Hii habari imekaa kiuda daku hivi. Waislam wanakaa kumkataa Kiongozi wa kichaga ilhali kuna wachaga waislamu wengi tu this doesnt add up...

Habari ina mkanganyiko na mgoloko mwingi, mara ukabila mara udini muradi kukidhi haja ya kuchochea watanzania. Huu ni mzuka wa OIC na Kadhi utatuletea habari nyingi watu wasipokuwa makini na kummeza nzima nzima kuna hatari mbeleni huko.
 
Swali ambalo nimekaa nikijiuliza bila ya kupata jibu ni je mara baada ya kufanikisha malengo yao hayo, hili suala zima litakuwa limewapa manufaa gani. Hii hali inachangiwa na Utawala wa Sasa, na mwelekeo mzima wa Nchi kutokana na viongozi waliopo.
 
"Waliokuwemo kwenye mkutano huo pia ni pamoja na Albert Marwa (inadaiwa ni mtoto wa kulelewa wa Generali Marwa) pamoja na mtu mmoja aitwaye Mtawa (huyu yasemekana ni mtumishi wa ngazi ya Juu ikulu)."

Ikithibitika hawa wawili walikuwepo kwenye hiyo mikakati, basi hali imefikia pabaya sana. Huyu mmoja "mkwe to be" wa muungwana(kazaa na binti yake yule daktari), huyu mwingine anajulikana ni afisa mwandamizi ikulu.... Wanaingiaje kwenye such scams!....Hii nchi sijui inakwenda wapi?
 
Hii habari imekaa kiuda daku hivi. Waislam wanakaa kumkataa Kiongozi wa kichaga ilhali kuna wachaga waislamu wengi tu this doesnt add up...

Habari ina mkanganyiko na mgoloko mwingi, mara ukabila mara udini muradi kukidhi haja ya kuchochea watanzania. Huu ni mzuka wa OIC na Kadhi utatuletea habari nyingi watu wasipokuwa makini na kummeza nzima nzima kuna hatari mbeleni huko.

udaku ni pale unapofikiri kila kitu ni udaku. Ukiona ni udaku unatakiwa ujimege tu taratibu waachie watu wajadili issue hata kama ni udaku.
 
MkJJ tunashukuru kwa habari,

Inawezekkana huo mpango uliokuwa unapangwa ni tofauti kabisa kwa maana
walikua wanatumia lugha ya kinteligensia so ikawa interpreted hivyo. Kwa haraka haraka
jinsi mpangilio wa vikao vyao ulivyokuwa unaendeshwa ni watu atleast wanao ujuzi walao
mdogo wa kupangilia mambo kukwepa kuwa suspected.

Je sauti zimechunguzwa vya kutosha kujua kweli huo mpango ni kama ulivyo na sio coding ilitumika????

Je hao watu wa Ikulu waliingia kuratibu hiyo kazi ama waliingia kwa nyazifa zao?????? ama kujua kuhusu hiyo njama na kureport???????

Maana aliyerecord sauti lazima ni insider wa hiyo terror group, Je
 
Kama huu ni ukweli basi hali ni mbaya sana. Ama kweli mafisadi hawana soni...Na CCM ni hatari kwa usalama wa taifa letu

Hata hivyo mimi kwa kujua mpango uliopo miongoni mwa MAFISADI walikokuwa wana mtandao wa kumtosa/kumtisha JK kwa sasa nachukuli habari hii kwa machale mno.....

Hao mashehe ubwabwa waliotajwa kuwemo katika kundi hilo naamini inawezekana kabisa kutumika kwa mpango mchafu na wa aibu kama huo. Tukumbuke kuwa wote ni makuwadi maarufu wa MAFISADI.

Siamini kama Mtawa kwa nafasi aliyo nayo anaweza kujihusisha na mpango hovyo kama huo (but in this Post Nyerere Tanzania anything is possible). Kuhusu huyu jambazi Albert Marwa ambaye JK amekataa katakata (kwa ushauri/shinikizo la UWT) kumhalalisha katika familia yake inawezekana kabisa akawemo katika siasa hovyo kama hizo. I believe those who fought fiercily against the idea of him marrying Presidents' daughter will b vendicated.

Kaka HALISI naomba feedback kuhusu hili...



Tanzanianjema
 

kuna mkakati wa kikundi flani cha imani kuwachafua wale wote kwenye jamii yetu wanaopingana nao katika ishu yao ya imani nzito, hapo kwenye luninga ilikuwa inapagwa mkakati ya kutaka kutekeleza azma yao, lakini wakanaswa, anayehusika sana na huu mkakati ni kijana mmoja mdogo sana, anayeitwa Marwa, ambaye alibadili dini siku za nyuma ili kumuoa mtoto wa Mang'enya RIP, aliyewahi kuwa balozi wetu UN, na kiongozi wa zamani wa taifa, ni rafiki wa karibu sana na Kinje, maana na yeye ni mtoto wa Meja General Marwa RIP,


Wakuu Wote; Pongezi sana kwa kuleta Dataz.

Nina mawili matatu ya kuongeza kuhusu wasifu wa kijana Albert Marwa (ingawa sidhani kama bado ni kijana.!!!).

Yeye ni mtoto wa kufikia wa Meja Gen Marwa RIP. Inasemekana Albert ni mzaliwa wa Uganda ambaye aliochukuliwa na Meja Gen wakati wa vita vya kumfukuza Iddi Amin mwaka 1979. Ni kijana mpole anayejificha kiasi kulinganisha na rafiki zake kama kina Kinje. Ni mtu makini sana kwenye mambo yake mengi (ananikumbusha msemo wa "…mwenda pole, ndiye mla nyama").

Nilimfahamu kwa karibu mwanzoni mwa miaka ya 90 akiwa anafanya biashara tofauti tofauti ili mradi anaingiza hela la maana (na hela ya maana aliingiza). Katika mojawapo ya biashara zake aliwahi kuwa na kampuni ya Clearing and Forwarding kipindi kile Serikali ya Mzee Ruksa haikusanyi kodi..!! Katika kipindi hicho aliwahi kuwa mmoja wa wafanyabiashara walioingiza bia za makopo za Heiken Tanzania. Akiwa na kampuni ya Clearing and Forwading alipata hela nyingi kwa kuuza Mafuta/Petrol yaliyoandikishwa kwenda nchi jirani (ambayo hayajalipiwa kodi) nchini Tanzania.

Niseme wazi kuwa pamoja na yote niliyojua kuhusu Albert miaka ya 90 ilikuwa dhahiri kuwa ana biashara "ya pembeni" ambayo inamuingizia hela zaidi ya zile nilizokuwa nazijua. Hili lilidhihirika kati ya mwaka 1997 - 1998 aliponunua nyumba 2 (za serikali) Oysterbay akazifanyia ukarabati mkubwa kabla ya kuzipangisha. Kipindi hicho alikuwa anaishi Upanga opposite na Califonia Dreamer/ Jolies Club.

Mabinti: Albert ni mtu mwenda pole, anajipanga vizuri. Katika moja ya strategy zake naona ana ka-historia ka kujipatia "influence" kupitia mabinti wa vigogo wa serikali. Mwaka 1997 alikuwa anatoka na mtoto wa Zakhia Meghji, Salama. Nikawahi kusikia tetesi kuwa anataka kumuoa ila sijui kama ni mahari ilikataliwa au nini kilichotokea. Wadau hapa wametoa dataz kuwa alibadili dini na kumuoa mtoto wa Balozi wetu UN na siku za karibuni alitaka kumuoa mtoto wa JK...ni dhahiri kuna ka-record fulani hapo.

Tetesi ya biashara zake: Mtakumbuka kuwa miaka ile ya 1990, enzi za Mzee Ruksa Jijini Dsm kulikuwa na mtu aliyefahamika kama Abdul Msomali, walikuwa karibu na Albert. Hii ilileta tetesi kuwa na yeye aliwa ni mtu wa Unga. Pia, miaka ya mwanzoni 2000 nilisikia tetesi tena kuwa ana kundi lake la majambazi au "wazee wa kazi" kama walivyojulikana mitaani. Hili lilitokana na Fact kuwa mdogo wake ambaye ni mtoto wa Meja Gen akiwa na wenzake walikamatwa na bastola wakipanga kufanya uhalifu (sijui kesi iliishia wapi). Tetesi nyingine ni kuwa kutokana Baba yake kuwa Meja Gen alikuwa anafanya biashara ya Silaha kwenye vita vinavyoendelea nchi jirani. Sikuwahi kuhisi wala kuhakikisha lolote kuhusiana na tetesi hizi.

My Take: Ni karibu miaka 20 sasa tangu nilipomfahamu Albert. Ni mtu makini sana, mwenye "connections" zenye nguvu ya ajabu Tanzania (alinunua nyumba za serikali Oysterbay kabla hata ya kifo cha JKN..!!). Ni mtu anayejua kutumia nafasi vizuri, yuko tayari kujipanga hata ikibidi kubadili dini ili mradi mambo yake yanakwenda vizuri. Kwa yeye kujiingiza kwenye masuala ya imani kali, kunamuweka kwenye "spot light" sidhani kama "strategy" hii mpya itampa mafanikio anayoyategemea.

Naomba Kuwasilisha
 
Wakuu mnaweza kufirikia "aloud" na kusema huenda lisemwalo lipo...ukiona kuwa miaka ya 1990 kulikuwa na "tetesi" kuwa Albert alikuwa anafanya biashara ya silaha nchi za jirani na hii taarifa ya leo yenye "uhakika" kuwa kuna mkono wake kwenye mikakati ya kuleta furugu za kidini na kikabila Tanzania. Natumai mmenipata...just trying to think aloud...!!
 
Ant Kikwete au wanamtandao wanaoasi wanaweza sana haya mambo. Haya endeleeni kupinga ufisadi na muwadondoshe mafisadi enyi wanafiki prosisiemu
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom