OCD wa Mbeya kuburuzwa mahakamani Jumanne wiki ijayo yeye binafsi na sio cheo chake

Mdude_Nyagali

Member
Dec 11, 2022
60
1,237
Kama tulivyowaahidi kwamba tutachukua hatua za haraka za kisheria kwa OCD Mbeya kwa kitendo chake cha kumkamata kinyume na sheria kisha kumpiga na kumchania nguo katibu wa CHADEMA kanda ya Nyasa Ndg. Gwamaka Mbughi . Tayari OCD amepelekewa Demand Notice (Ilani) ya kusudio ya kumshtaki binafsi ifikapo jumanne kama hatakuwa amemlipa Gwamaka milion 100.

Hata hivyo OCD anatakiwa kumuomba radhi Gwamaka kwa siku tatu mfululizo kwa dakika tano kwa kila awamu na mara tatu kwa siku kuanzia tarehe 14 hadi 16 mwezi Novemba 2023 katika chombo cha habari kinachosikika katika Kanda ya Nyasa kwa utaratibu Ufuatao;

Saa Mbili na Nusu Asubuhi
Saa Nane Kamili Mchana
Saa Kumi na Mbili Jioni.

Lakini pia OCD anatakiwa kumuomba radhi Gwamaka kwa siku tatu mfululizo kwa dakika tatu kwa kila awamu na mara tatu kwa siku kuanzia tarehe 14 hadi 16 mwezi Novemba 2023 katika televisheni kati ya Azam TV, ITV Tanzania au STAR TV kabla ya taarifa ya habari ya usiku wa saa mbili.

Kuweka bayana majina Kamili ya watu aliowaweka makusudi mahabusu na waliohusika kumshambulia Gwamaka na kumdhuru pamoja na hatua alizochukua tangu kupokea malalamiko ya Gwamaka.

Wakati OCD akipewa ilani hii bado kesi nyingine iko hatua ya mwisho ambayo ameshtakiwa yeye kwa cheo chake aje aiambie mahakama ni kwanini alizuia maandamano ya amani bila kuweka sababu za masingi?

Wacha watumie nguvu sisi tutatumia akili.

Mdude Nyagali 7 x 70 Sumu ya Nyigu.View attachment OCD Mbeya.pdfView attachment OCD.pdf
 
Attachments

  • Mwabukusi Signed.pdf
    236 KB · Views: 5
Siku zote busara na hekima ndio taa katika uongozi. Ila kwa Mdude aisee wewe ni kichaa Yarabii na hata hujajitambuaa . Hivi hujifunzi kwa kina G Malisa, Yericko, James Mbowe etc..?
Ungefafanua...

Ajifunze nini toka kwa hao uliowataja?

Huyu ni Mdude_Nyagali na hao ni wao. They are quite irrelevant...

By the way, mnataka wafanye nini zaidi ya hiki wanachokifanya? Wanavunja sheria yeyote kwenda mahakamani kupeleka grievances zao dhidi ya OCD Mbeya?

Why are you so surprised??

Hebu soma vijineno vya hawa 👇👇👇watu. I am not sure if they're in their right senses at all...!
Huna akili
Kichaa, mental case hii
Wee jamaa sio mzima
Hahahah Mdude wahi mirembe.
Mental case
Kwa hizi mahakama za CCM usitegeme chochote mkuu

Ndugu Bejamini Netanyahu, si kwamba kina Mdude_Nyagali na wenzake hawajui status ya mahakama zetu. Wanajua fika..

Lakini ni lazima wafanye hivyo kuweka precedence kwa vizazi vijavyo kurejelea no matter watashinda kesi au la..

Kwangu mimi, huo ni uamuzi sahihi na utazidi kuwaweka pabaya wahusika kuliko mtu anavyoweza kudhani...!
 
Hivi kwanini mnamdhihaki na kumwambia awahi mirembe huyu Mdude? Aisee msikariri maisha, pamoja na ubabe wa kiajabu ajabu wanaofanya hawa maafande ipo siku mtu atashinda kesi ya hivi, niaminini nawaambia
Nimewaambia watu hawa...

Liko wazi mno hili kuwa, angekuwa ni mtu wa kuwa Mirembe, basi polisi na serikali Kwa ujumla Ingem - ignore. Lakini huyuhuyu Mdude_Nyagali anawalaza polisi na watawala bila kuvua viatu..!

Go Mdude_Nyagali gooooooooooo. Mimi binafsi nakuunga mkono ili mradi huvunji sheria yeyote ya nchi hii..
 
Kama tulivyowaahidi kwamba tutachukua hatua za haraka za kisheria kwa OCD Mbeya kwa kitendo chake cha kumkamata kinyume na sheria kisha kumpiga na kumchania nguo katibu wa CHADEMA kanda ya Nyasa Ndg. Gwamaka Mbughi . Tayari OCD amepelekewa Demand Notice (Ilani) ya kusudio ya kumshtaki binafsi ifikapo jumanne kama hatakuwa amemlipa Gwamaka milion 100.

Hata hivyo OCD anatakiwa kumuomba radhi Gwamaka kwa siku tatu mfululizo kwa dakika tano kwa kila awamu na mara tatu kwa siku kuanzia tarehe 14 hadi 16 mwezi Novemba 2023 katika chombo cha habari kinachosikika katika Kanda ya Nyasa kwa utaratibu Ufuatao;

Saa Mbili na Nusu Asubuhi
Saa Nane Kamili Mchana
Saa Kumi na Mbili Jioni.

Lakini pia OCD anatakiwa kumuomba radhi Gwamaka kwa siku tatu mfululizo kwa dakika tatu kwa kila awamu na mara tatu kwa siku kuanzia tarehe 14 hadi 16 mwezi Novemba 2023 katika televisheni kati ya Azam TV, ITV Tanzania au STAR TV kabla ya taarifa ya habari ya usiku wa saa mbili.

Kuweka bayana majina Kamili ya watu aliowaweka makusudi mahabusu na waliohusika kumshambulia Gwamaka na kumdhuru pamoja na hatua alizochukua tangu kupokea malalamiko ya Gwamaka.

Wakati OCD akipewa ilani hii bado kesi nyingine iko hatua ya mwisho ambayo ameshtakiwa yeye kwa cheo chake aje aiambie mahakama ni kwanini alizuia maandamano ya amani bila kuweka sababu za masingi?

Wacha watumie nguvu sisi tutatumia akili.

Mdude Nyagali 7 x 70 Sumu ya Nyigu.View attachment 2809702View attachment 2809703
Vipi Jana uliandamana?
 
Back
Top Bottom