Caught on Tape: Mkakati wa Mamluki wafichuliwa!

Status
Not open for further replies.
Date::1/12/2009
Waislam nchini wapinga oparesheni Sangara
Geofrey Nyang'oro na Zaina Malongo
Mwananchi

WAUMINI wa dini ya kiislam wamepinga oparesheni sangara inayoendeshwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa madai kuws chama hicho na operesheni hiyo, haina manufaa kwa uisalam kwa kuwa imejaa ukabila, ubinafisi na udini

Wakizungumza kwa nyakati tofauti kwenye kongamano la kiisilamu, lililofanyika jana jijini Dar es Salaam, walisema oparasheni Sangara imekuwa ikimchafua rais Jakaya Kikwete bila sababu licha ya mambo mengi mazuri, aliyoyafanya kwa taifa.

Shekhe Saidi Mwaipopo aliwataka waisalamu kutambua kuwa chama hicho, hakina msaada wowote wa maendeleo ya uislamu kutokana na chama hicho kujaa ukabila udini na ubinafisi.

"Napenda waislamu muelewe kuwa chama cha Chadema hakina msaada wowote juu ya uislamu na kimekumbatia udini, ukabila na ubinafisi kutokana na sababu hiyo, tutatembea nchi nzima kuwaeleza wanachi ukweli wa jambo hili na kuwataka wasikiunge mkono chama hicho,"alisema Mwaipopo.

Akizungumzia Oparasheni Sangara, alifafanua imekuwa ikichafua rais Kikwete bila ya sababu za msingi kwa kuwa rais huyo tangu ameingia madarakani amesababisha mafisadi kukamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya Sheria.

Pia alisema kipindi hiki cha Rais Kikwete kumekuwa na uhuru mkubwa wa kuabudu kutokana na serikali yake kuruhusu mihadhara ya kidini ambayo, ilikuwa ikizuiliwa na serikali ya awamu ya tatu.

Mwaipopo alisema kama oparesheni Sangara ingekuwa ni ya kweli basi ingekuwa tayari kutaja baadhi ya sifa ambazo Rais Kikwete amekuwa akizifanya badala ya kumchafulia jina lake kila inaopoendesha mikutano yake.

Alisema kutokana na ubinafisi wa chama hicho, kimeshindwa kuviunga mkono vyama vya upinzania vya Chama cha Wananchi (CUF) na Sauti ya Umma (SAU) vinavyoshiriki uchaguzi mdogo wa Jimbo la Mbeya vijijini ambao unaotarajia kufanyika mwezi huu.

Katika hatua nyingine, Mwaipopo aliwataka viongozi wa dini za kiislamu Mashekhe na Maimamu kuingia kwenye siasa kuanzia nafasi za serikali za mitaa hadi ubunge ili kwenda kuwatetea wananchi.

Alisema kama viongozi hao wa dini hawatajitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi mambo yao, mengi yataendelea kukwama kutokana na kukosekana kwa watetezi kwenye vyombo vya maamuzi kama ilivyokuwa kwenye mahakama ya kadhi.

Akisoma tamko la waislamu hao, kuhusu OIC na Mahakama ya Kadhi katibu wa Baraza la habari la Kiislamu Tanzania (Bahakita) Shekhe, Sadick Godigodi alisema wamekubaliana kwa kauli moja kusubiri kauli itakayopotolewa na serikali.

Kutokana na hatua hiyo, waislamu hao wamesimamisha maandamano waliyokuwa wamepanga kufanyika mapema mwezi huu kwa lengo la kuishinikiza serikali kutoa tamko lake kuhusiana na Mahakama ya Kadhi na OIC na walisema kuwa watatoa kauli yao baada ya serikali kutoa tamko.
 
Venance George, Morogoro
BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) limesema kauli iliyotolewa juzi na baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu kupinga oparesheni Sangara inayoendeshwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), si kauli ya waislamu wote.
Akizungumza mjini Morogoro kwa niaba ya Kaimu Mufti wa Tanzania,
Shekhe Suleiman Gorogosi, mratibu wa habari wa Bakwata, ustadhi Issa Mkalinga alisema kauli hiyo ni ya waislamu wachache ambao wamekuwa wakitumiwa na viongozi wa kisiasa kwa manufaa binafsi.
Ustadhi Mkalinga pamoja na Mkurugenzi wa Utawala, ustadhi Karim Mataliwa, aakizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara ya kaimu mufti huyo ya kutembelea mikoani kuhamasisha uhai wa baraza, alisema baraza halitambui kauli hiyo na wala halijihusishi na mambo ya siasa.
"Ujue tunaelekea kwenye uchaguzi mkuu hapo mwakani, hivyo wako baadhi ya wanasiasa wanatumia mwanya wa majukwaa ya dini kupeleka ujumbe wao," alisema.
Akizungumzia ziara ya kaimu mufti mkoani Morogoro, Mkurugenzi wa Utawala alisema kuwa ziara hiyo ni sehemu ya utaratibu aliyojiwekea kaimu mufti ya kutembelea baraza katika mikoa yote Tanzania na kwamba kaimu mufti ametembelea Dodoma na Morogoro na atatembelea mikoa mingine.
Ustadhi Mataliwa alisema lengo la ziara hizo ni kutaka kujua uhai wa baraza na matatizo yanayolikabili baraza katika ngazi hizo ikiwa ni pamoja na kuhimiza kufanya maandalizi ya uchaguzi wa viongozi kuanzia ngazi ya msikiti hadi taifa utakaoanza kufanyika mwezi April mwaka huu.
Wakati huo huo, katika mahojiano na baadhi ya waumini wa dhehebu hilo, mkoani Morogoro wameunga mkono kauli ya Bakwata na kudai kuwa viongozi wa dini ni vema wakafanya shughuli zao za kiroho na kuwaacha wanasiasa kufanya kazi zao za siasa.
Mmoja wa waumini hao, Ismael Rashid, alisema tamko lililotolewa na waislamu katika kongamano la jijini Dar es Salaam la kudai kuwa Chadema haina manufaa na msaada wowote kwa uislamu si maneno ya kiungwaana na si vema kukipakazia chama hicho kwamba ni kikabila na cha kibinafsi.
Rashid ambaye pia ni kiongozi wa chama cha Jahazi asilia mkoani Morogoro alisema hatua iliyochukuliwa na Chadema ya kuacha kuunga mkono vyama vya CUF na Sauti ya Umma (SAU) ilikuwa ni sahihi kwa sababu chadema walisimamisha mgombea ubunge katika jimbo la Mbeya vijijini lakini vyama hivyo vilimwekea pingamizi mgombea huyo na kuenguliwa.
"Pingamizi hilo lilisababisha mgombea ubunge wa Chadema akaenguliwa kugombea
nafasi hiyo, sasa iweje chadema iwaunge mkono?" alihoji Rashid .
Alisema chama cha Chadema hakiungi mkono kampeni za mgombea wa CUF kwa mdai kuwa chama hicho, mwakani inakusudia kusimamisha mgombea wake katika jimbo hilo kwa hiyo kama Chadema ikiunga mkono CUF itashindwa kusimamisha mgombea wake hapo mwakani.



CHANZO:Mwananchi
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom