Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 15,570
- 19,444
mmeshindwa kuweka hivyo vifaa vya kisasa kuokoa maelfu ya binadamu wanakufa kwa ajali....leo hii unasema mtaweka vifaa hivyo kuokoa WANYAMAPORI......
Kutokana na hiyo sensitivity mnayotumia kuzuia ujenzi huo haitakuwa vigumu kuwa na speed detectors cameras katika eneo hilo kwa sababu hata hivyo huwa linalindwa na maafisa wanyama pori. Kwanza kutakuwa na maafisa wanaoukusanya ushuru wa kuingia katika mbuga hizo kwa pande zote mbili za mbuga.
Kutokea kwa ajali sehemu nyinginezo za nchi siyo kielelezo kuwa sehemu hiyo askari wanyama pori watashindwa kulinda madereva wasizidishe speed; vinginveyo unakuwa una-stereotype bila kuwa na sababu ya msingi. Unasahau kuwa sehemu kubwa ya ajali hizo hutokea kwa sababu ya barabara kuwa mbovu.
kuhusu kugonga wanyama, kama umeshawahi kupita barabara ya Mwanza-Bunda saa za jioni utakutana na makundi makubwa sana ya wanyama wanaotoka au kwenda kunywa maji ziwani lakini hawajawahi kugongwa au kuzuiwa wasiendelee kunywa maji.
Petitioners wote niliowaona ambao wamekuwa recruited na na wakenya ni watu walioko nje ya nchi (Marekani na Ulaya) wengine wakiwa hawajahai hata kufika tanzania. Wanachukulia kuwa highway hiyo itakuwa inachukua magari mengi kama yalivyo huko kwao, jambo ambalo siyo sahihi.