CAG: Wastaafu na wenza wao wanaigharimu NHIF Tsh 84.7 billion kila Mwaka Bila Wao kuchangia

CAG Kichere amesema Hasara nyingine wanayoingia NHIF inatokana na Wastaafu na Wenza Wao kufaidika na Fedha za Mfuko huo Bila Wao kuchangia

Kicheere amesema Wastaafu na Wenza Wao wanaugharimu Mfuko wa Bima tsh 84.7 billion kila Mwaka Bila Wao kuchangia.

View attachment 2948111

Mlale Unono
Huyu kichere naona ni chawa tu. Pamoja na wizi mkubwa eti asilimia 99 ya halmashauri zimepata hati safi. Yaani pengine amerejesha kuangalia mpango wa mahesabu tu badala ya kuangalia wizi na rushwa ambao ndio kitu wananchi wanataka kusikia. Halafu analeta ujinga maana ukiwa chawa unakua mjinga. Anajifanya hajui wastaafu wanahudumiwa kutokana na mchango waliyofanya wakiwa kazini. Yote ni kwamba wanafanya pengine hila kutaka kuwadhulumu wastaafu. Tayari mfuko huo wa bima uliyojaa ubadhirifu umesababisha wafaidika kunyimwa matibabu kwa kiwango kinachostahili kwa mfuko kubana fedha za huduma huku ukiwa umewakopesha wafanyakazi wake mabiloni ya michango ya watumishi.
 
Simuonei huruma mstaafu, kwani ndo kasababisha haya wakati akiwa mwajiliwa...hata KICHERE soon panga Hilo Hilo na lawama hizo hizo na kadhia hizo hizo za wastaafu zitampata yeye. Unapokalia kiti kizuri ukajioona Bora kesho atakaa mwingine atakubinya hivyo hivyo... MWISHO wa siku inakuwa MILA YETU kama nchi. Ukimpa mstaafu pesa MWISHO wa siku inarud kwa mzunguko inaongeza uchumi, na ni nadra sana mstaafu kuish miaka 15 bado yuko hai, Kumlisha MTU mzima miaka 10 unaona hasara kama nchi?. Elimu bure kwa watoto, hivyo hivyo na wastaafu wapate bure. NI suala la circle Tu.
IMG-20240327-WA0007.jpg
 
NHIF wasilete majibu mepesi kwa maswali magumu

NHIF wamewekeza wapi fedha za Michango ?

Wameleta fitna bima za watoto zikafutwa

sasa wanaleta fitna Wazee na wastaafu nao waondolewe

wanataka wabaki na Wafanyakazi pekee ambao rate yao ya kuumwa ipo chini sana kukwepa kubeba gharama za matibabu

kama hawawezi kuendesha bima yenye only 8% ya Watanzania wataweza kweli hiyo bima kwa wote ?
Ni kama vile wao hawatastaafu ,NHIF ni bima ya afya watumishi wanachangia Toka mishahara Yao,wako wengi walichangia kwa muda wao wote wa utumishi wao na hawakuwahi kuugua hata siku Moja,Na makubaliano ni kuwa wataendelea kutibiwa kwa muda wa maisha yaliyobaki,eti Leo wanaonekana ndio wanasababisha shirika kupata hasara,haya ni matusi kwa wastaafu.Hivi non profit organization(NHIF)inaweza kupata hasara wakati haifanyi biashara,?, Ni vyema bima hii ikawa chini ya taasisi za akiba za uzeeni(psssf).huku itakuwa idara hivyo gharama za uendeshaji zitakuwa chini,NHIF waache visingizio wasema fedha za wachangiaji ziko wapi !,eti badala ya kuwekeza fedha zetu wanakopeshana na kukopesha.WAMESHINDWA.
 
CAG Kichere amesema Hasara nyingine wanayoingia NHIF inatokana na Wastaafu na Wenza Wao kufaidika na Fedha za Mfuko huo Bila Wao kuchangia

Kicheere amesema Wastaafu na Wenza Wao wanaugharimu Mfuko wa Bima tsh 84.7 billion kila Mwaka Bila Wao kuchangia.

View attachment 2948111

Mlale Unono
Kwani sheria kwa wastaafu kuhusu nhif inasemaje?kwani inatofauti gani na pension?

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
 
Huu upumbavu was Sheria ya 60% ya mafao Kwa wake wa wastaafu ni ya kipuuzi sana!nitaifuta nikiingia!!

Halafu wastaafu hiyo 80% ya Nini kama Bill ya maji umeme na nyumba ya Bure wanazo!!?

Kwanini isiwe 10% ya mshahara was alie madarakani!!?

Ngoja niingie!!

Ujinga umezidi!!
Kwani The system aka DP,wanamaoni gani kuhusu sakata hili ? Au bado wako St Peter wakiendelea kufaidi keki ya taifa bila Kazi.
 
Huyu CAG hapo kwa wastaafu amechemka!!!

Kwenye issue ya wastaafu kutibiwa na NHIF wakati hawachangii chochote. Hapa itabidi wapaache hivyo hivyo.

Kwa mfano mimi binafsi toka tulipoanza kuchangia mfuko mwanzoni mwa miaka ya 2000's sikuwahi kuugua na kutumia kadi ya NHIF.

Kwa nini leo mfuko wa NHIF usinitibu wakati nimestaafu??

Si hivyo tu, hii inaondoa dhana nzima ya Bima ya Afya.
In fact the major concept of Health Insurance Scheme is that "Insurance is a way to manage your financial health risks". That is When you buy insurance, you purchase protection against unexpected health financial losses.

Hii ikiwa na maana ya kwamba, mtu anaweza kushambuliwa na maradhi/ugonjwa wakati wowote, na kuna kipindi mtu anakuwa hana pesa za kumudu gharama za matibabu, sasa hapo Bima ndio inachukuwa nafasi yake.

Funny enough, it was just last week in a TV programme (Kipima joto), kuna kiongozi mmoja wa Chama Cha Wamiliki Hospitali Binafsi (APHFTA) alipokuwa akielezea sababu za NHIF kushindwa kumudu kujiendesha ipasavyo, ni kwamba mfuko unahudumia wagonjwa wengi kuliko wachangiaji wakiwemo wastaafu, amesahau kwamba hawa wastaafu ndio walio wekeza kwenye huo mfuko wa Bima kwa maana ya kuweza kumudu tiba hapo baadae.

Kwa kweli ni kauli yenye kusikitisha na yenye kukatisha tamaa, iliyo tolewa na mtu ambae haelewi dhana nzima ya Bima.

Ni dhahir CAG nae ameshindwa kutafakari vema hapo na kuamua kuiona hiyo kama hoja inayojenga.
Hakika, amenisikitisha sana mtu wa Kariba yake kutokuw na umelewa wa social protection schemes. Sasa alitaka wastaafu watibiwe na nini. Alichokisema ni typically tabia za weusi kula na kuvimbiwa na kusahau kesho IPO. Anyway labda kwakuwa yeye atapata premium service kwa nafasi yake akistaafu..
 
Hivi, kwani wakati wanasema mchangiaji na mwenza wake wataendelea kunufaika na mfuko iwapo mchangiaji atastaafu hawakujua mstaafu hatochangia kwenye mfuko baada ya kustaafu?
 
Huyu CAG hapo kwa wastaafu amechemka!!!

Kwenye issue ya wastaafu kutibiwa na NHIF wakati hawachangii chochote. Hapa itabidi wapaache hivyo hivyo.

Kwa mfano mimi binafsi toka tulipoanza kuchangia mfuko mwanzoni mwa miaka ya 2000's sikuwahi kuugua na kutumia kadi ya NHIF.

Kwa nini leo mfuko wa NHIF usinitibu wakati nimestaafu??

Si hivyo tu, hii inaondoa dhana nzima ya Bima ya Afya.
In fact the major concept of Health Insurance Scheme is that "Insurance is a way to manage your financial health risks". That is When you buy insurance, you purchase protection against unexpected health financial losses.

Hii ikiwa na maana ya kwamba, mtu anaweza kushambuliwa na maradhi/ugonjwa wakati wowote, na kuna kipindi mtu anakuwa hana pesa za kumudu gharama za matibabu, sasa hapo Bima ndio inachukuwa nafasi yake.

Funny enough, it was just last week in a TV programme (Kipima joto), kuna kiongozi mmoja wa Chama Cha Wamiliki Hospitali Binafsi (APHFTA) alipokuwa akielezea sababu za NHIF kushindwa kumudu kujiendesha ipasavyo, ni kwamba mfuko unahudumia wagonjwa wengi kuliko wachangiaji wakiwemo wastaafu, amesahau kwamba hawa wastaafu ndio walio wekeza kwenye huo mfuko wa Bima kwa maana ya kuweza kumudu tiba hapo baadae.

Kwa kweli ni kauli yenye kusikitisha na yenye kukatisha tamaa, iliyo tolewa na mtu ambae haelewi dhana nzima ya Bima.

Ni dhahir CAG nae ameshindwa kutafakari vema hapo na kuamua kuiona hiyo kama hoja inayojenga.
Naona umejikoroga mwenyewe.
Maana ya Bima ni kuweka dhamana ya mali ili kufidiwa ikiwa janga litakukuta, na sio kuwekeza pesa ili uje uzidai ikiwa hukupata janga.

Kwa tafsiri ya BIMA, CAG yuko sahihi kwa 100%. Wastaafu hawachangii chochote kwenye NHIF lakini wanapatiwa huduma kama kawaida. Michango ile ya awali ilikuwa wakati wakiwa kazini, hivyo baada ya kustaafu, hawakatwi chochote na ilipaswa wasipewe huduma yoyote ya Bima. Otherwise, utaratibu uwekwe wa kukatwa pesa kwenye pensheni zao kila mwezi ili wawe na uhalali wa kuendelea kufaidika na huduma za NHIF.
 
Hivi, kwani wakati wanasema mchangiaji na mwenza wake wataendelea kunufaika na mfuko iwapo mchangiaji atastaafu hawakujua mstaafu hatochangia kwenye mfuko baada ya kustaafu?
Ni makosa, tena ni makosa makubwa kwa mtu asiyechangia chochote kwenye mfuko halafu avune huduma za mfuko wa bima ya Afya. Kama wewe sio mchangiaji na ikiwa unavuna huduma maana yake unatumia michango ya wengine.
Lazima mfuko wa NHIF ubakie kwa wachangiaji tu, hizo huruma za kiutu zinapaswa kufidiwa na serikali, ama serikali iwachangie au wastaafu wachangie kupitia pensheni zao otherwise wastaafu wapate huduma nje ya utaratibu wa NHIF ili kulinda uhai wa mfuko
 
Na pale walipokuwa wanatuchukulia fedha zetu (makato) tulipokuwa kazini mbona walinyamaza tu?
Mimi nilikuwa nakatwa karibu 130,000/- kwa mwezi kwa muda wa miaka karibu kumi na tano, sikutumia huduma katika kipindi hicho chote, Mr alikuwa na shughuli zake wala hakujali bima hiyo, na sote tulikuwa wazima wa afya.
Baada ya kustaafu ndiyo shughuli ikaanza, leo sukari kesho pressure, sasa ndiyo tunatumia hiyo bima inakuwaje anatusema tunaigharimu NHIF?. Kama mfuko wameutumia vibaya na kujilipa ovyo ovyo hilo siyo kosa letu.

Huyo Kichere asijione ni mzima kwa sasa lakini ajue naye atafikia huku kwetu wastaafu na hapo ndiyo atakiona cha mtema kuni.
Huyu anajaribu kuficha madudu ya NHIF…hivi amesema kama walijikopesha hela za watumishi?
 
Naona umejikoroga mwenyewe.
Maana ya Bima ni kuweka dhamana ya mali ili kufidiwa ikiwa janga litakukuta, na sio kuwekeza pesa ili uje uzidai ikiwa hukupata janga.

Kwa tafsiri ya BIMA, CAG yuko sahihi kwa 100%. Wastaafu hawachangii chochote kwenye NHIF lakini wanapatiwa huduma kama kawaida. Michango ile ya awali ilikuwa wakati wakiwa kazini, hivyo baada ya kustaafu, hawakatwi chochote na ilipaswa wasipewe huduma yoyote ya Bima. Otherwise, utaratibu uwekwe wa kukatwa pesa kwenye pensheni zao kila mwezi ili wawe na uhalali wa kuendelea kufaidika na huduma za NHIF.
Wewe ni mwehu kabisa kujadili na wewe ni kupoteza muda😂😂😂😂😂
 
Chonde chonde, Wastaafu wasiguswe please. Tusijisahau, hata nyinyi wenye mamlaka mtakua wastaafu siku moja. Wastaafu kuwa na health insurance ni haki yao. Hawa ni wachangiaji wa uhakika wa zamani, ambao walichangia miaka kadhaa pengine bila kuugua. Ni hawa ambao pesa zao zilizoko kwenye mifuko ya jamii, zinatumika kuendeshea nchi.
Sababu ya kutetereka kwa NHIF tatu :
1. Serikali kujikopesha pesa za mfuko bila kurudisha.
2. Wafanyakazi wa NHIF kujikopesha mikopo mikubwa bila riba au riba kidogo na kutokurejesha mikopo hiyo kwa wakati.
3. Bima za vifurushi ambazo wanaokata wengi ni Wagonjwa wenye magonjwa Sugu, hivyo kutaka kupunguza gharama, wagonjwa wanaamua kukata bima. NHIF wawe na utaratibu wa kupima wateja wapya kabla ya kuwapa uanachama wa mfuko. Kwani, bima ikiwa na wanachama wengi wagonjwa, lazima ishindwe kujiendesha. Mfuko unahitaji wachangiaji wengi wasioumwa, ili pesa yao iwahudumie wale wachache wanaoumwa. Bima za vifurushi zimeongeza kundi la wanaoumwa hivyo kufanya idadi ya wanachama wasioumwa kushindwa kufidia wale wanaoumwa.
Asante
Taratibu Kijana! Anamaanisha wale Wastafu untochable
 
Mi nimechangia mpaka nikastaafu, sijawahi kwenda hospitali....Pesa zangu zipo wapi?
 
Ni makosa, tena ni makosa makubwa kwa mtu asiyechangia chochote kwenye mfuko halafu avune huduma za mfuko wa bima ya Afya. Kama wewe sio mchangiaji na ikiwa unavuna huduma maana yake unatumia michango ya wengine.
Lazima mfuko wa NHIF ubakie kwa wachangiaji tu, hizo huruma za kiutu zinapaswa kufidiwa na serikali, ama serikali iwachangie au wastaafu wachangie kupitia pensheni zao otherwise wastaafu wapate huduma nje ya utaratibu wa NHIF ili kulinda uhai wa mfuko
Mfuko unafilisiwa na ukopaji na uwekezaji usio na tija. Du ndio mnataka mje na bima ya afya Kwa wote?
 
Back
Top Bottom