OLS
JF-Expert Member
- Oct 12, 2019
- 419
- 670
Agosti 23, 2022 tunatarajia kuwa na zoezi la sensa ya watu na makazi. Zoezi muhimu katika mipango ya sera na maendeleo ya Taifa.
Hata hivyo mwaka huu tumeona matangazo yamekuwa mengi sana hadi inaleta maswali kama fedha za umma zimetukima ipasavyo. Uhamasishaji umekuwa mkubwa kama kuna mgomo ulitangazwa, tofauti na mwaka 2012.
Mbali na nguvu kubwa ya matangazo bado pia kumekuwa na Tamasha la Sensabika ambalo limeanza leo ambapo wasanii na wanamichezo wamejazana leaders club kufanya yao.
Wakati huo tozo zimeongezeka kwa kiasi kikubwa na kumuumiza mwananchi, hali inayonipelekea kutoa wito kwa CAG kutupa ripoti ya bajeti nzima ya sensa ili tuone kama tumezingatia.
Natoa wito kwa wote walioko karibu na CAG kumwambia tafadhali atufanyie hili. Isije ikawa watu wanalambishana asali huku wananchi wakiumia.