CAF wametumia vigezo gani kupata timu katika mashindano ya Africa Football league (AFL)

Yaani at least kwa miaka ya hivi karibuni Wangesema Rivers kidogo ingeingia akilini.
Haya mashindano ni bonanza
Hebu tuwalinganishe Rivers na Enyimba kwa hii miaka mitano kwenye mashindano ya CAF, Rivers kaizidi nini ENYIMBA..?

1 Idadi ya mashabiki (maana AFL inatafuta makusanyo ya fedha pia).

2. Ushiriki na hatua walizofika kwenye mashindano ya CAF vilabu katika miaka hii mitano.

3.HISTORIA, LEGACY pamoja na BRAND.

Haya wewe unaejua sana, tueleze Rivers kamzidi nini Enyimba hapo ndani ya hii miaka mitano.
 
Hoja yako ni ipi? Ulitamani wewe Kwa mawazo yako, ziingie timu zipi kwenye haya mashindano?
Nimeona mmebishana kuhusu Enyimba na moja ya hoja yako ni kwamba umesema Enyimba amefanya vizuri katika mashindano ya CAF. Swali langu kwako ni je Enyimba ana point ngapi katika ranking ya CAF?

Najaribu kuuweka mjadala katika upana wake
 
Ngoja nikupe vigezo

1: timu iwe inavaa jezi nyekundu simba ☝🏽 Na al ahly wanaingia hapa

2 : timu imiliki uwanja wake wa mazoezi ☝🏽 Timu zote zinaingia hapa

3: timu iwe (atlist) nimeamua kutumia na ka language uelewe ndani ya miaka 25 iliyopita imeingia makundi caf champions league👍🏽 Hapa wote tuna hicho kigezo

4: timu isiwe na mchanganyiko wa rangi za kijani na njano kwenye jezi zao 👍🏽 Hapa wote tumepita hadi mamelodi skuhz anavaa njano na buluu☝🏽

5: timu mashabiki wake wawe hawajawahi kuitwa nyani na kocha 👍🏽Hapa napo naona wote tumefuzu tunaocheza

6: timu iwe haijawahi fungwa mara mbili mfululizo na ihefu fc 👍🏽 Hii nayo naona wote tupo sawa

7: timu iwe ina msemaji mmoja anaeeleweka kama msemaji 👍🏽hapa napo naona wote tumefuzu
Sasa ndugu wewe unayesema vigezo huelewi ni vipi nimejitahidi kukuelewesha kwa hivi vichache ambavo naona vitaeleweka
Lakini kabla sijaenda naomba nimalizie cha mwisho
Timu na washirika wake wawe hawajawahi piga msemaji wa timu nyingine 😁👍🏽 Hiki ndo kigezo muhimu kuliko vyote na ndo wanachokizingatia sana
Ahsante mwenye uzi🤝
 
Back
Top Bottom