Kikwete amejitahidi kiasi kuepukana na mawaziri ambao wana tuhuma/kashfa za ufisadi kwenye cabinet yake mpya. Lakini nimegundua kuwa wanasiasa vilaza wenye uwezo mdogo wa akili, ubunifu na kuchapa kazi ndiyo wamepewa kuongoza wizara nyeti.
Kwa maoni yangu, kwa kutumia mawaziri walewale wa Cabinet, Kikwete angekuwa na baraza la mawaziri lenye ufanisi mkubwa kama angefanya uteuzi huu:
1. Waziri wa Fedha, Prof. Anna Tibaijuka
Huyu ana uzoefu wa UN, UNCTAD, ana PhD ya agro-economics na alikuwa economics professor UDSM. Anakubalika sana kimataifa. Donors hawana imani na uwezo wa Mustafa Mkulo. Angesaidia kurudisha imani ya donors kwa Tanzania ambao walipunguza misaada kwenye bajeti iliyopita kwa kama $250m.
2. Waziri wa Maliasili na Utalii, John Magufuli
Utalii inaongoza kwa kuingiza pato serikalini lakini bado Tanzania imelala sana. Afrika Kusini inapata watalii milioni 8 kwa mwaka sisi bado hata hatujafikisha 1 million. Pia angekomesha biashara haramu ya vitalu, magogo na meno ya tembo.
3. Waziri wa Nishati na Madini, Harisson Mwakyembe
Huyu ni mchapa kazi mahiri. Anaijua sheria vizuri na angesimamia mikataba mibovu ya madini ibadilishwe. Makampuni makubwa ya madini yanamdharau waziri wa sasa William Ngeleja kuwa hajui kinacho endelea. Ngeleja aliwahi kupongeza De Beers kuuza mgodi wa Mwadui Williamson diamonds kwa Petra kimakosa badala ya kuuza hisa hizo kwa serikali ya Tanzania.
4. Waziri wa Kilimo, Samuel Sitta
Angesaidia kuleta msukumo mpya kwenye sekta ya kilimo ambayo bado inalegalega sana. Angeboresha kilimo kwa standards and speed. Kilimo cha kisasa kingefana. Tanzania ingekuwa nchi ya milk and honey.
5. Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Prof. Mark Mwandosya
Ni mfuatiliaji mzuri. Angesaidia kuboresha utendaji kazi wa halmashauri zote nchini. George Mkuchika, ambaye ni swahiba mkubwa wa Kikwete alishindwa kuongoza wizara ndogo kama ya habari. Kumpa Mkuchika wizara hii nyeti ni jambo la ajabu sana na la kutotegemewa.