Buseresere: Mapigano makali yaibuka kati ya waislamu na wakristu!

Status
Not open for further replies.
Kesho utasikia salamu za rambirambi kwenda kwa wahusika! Ndugu yangu kama mabango ya waganga wa kienyeji mjini Dar na mikoani yamengongomelewa kwenye nguzo za umeme na siku za wkend wateja wakuu ni haohao wakubwa usitarajie akili ya kutatua kero za raia. Religion is a fatal bomb.
 
Ina maana hakuna Mama Ntilie kwenye Kitimoto? Kwani nani anachinja Kitimoto? Mbona huko hamji juu?

Huu ni UPUUZI wa Pande zote mbili na Wassira kwa kushindwa ku-solve hili swala, nimemdharau mno na kusema kweli hafai hata kupelekwa Gombe maana hata huko ataharibu. Hili ni swala dogo na linaongeleka sana tu. Hakuna kutumia mabavu na kama kwenye Kitimoto hatulalamikiani kwa nini kwenye nyama tulalamikiane?

Pia inakuwaje kwamba Bucha za Waislaam zilianza kudoda? Si tunaambiwa kuwa nchi hii Waislaam ni wengi?

Narudia tena, WOTE NI WAPUUZI tu na vidini vyenu vya kuletwa na MELI.

nakuhakikishia hakuna mama ntilie anaeuza kitimoto bila kuweka bango.
 
ha ha haa sijui nikwambiaje kwanza nikuulize unajua maana ya islam chunguza kwanza ujue maana yake ndio ulinganishe na huo mwaka ulioandika kwanza Yesu (issa) hakuleta ukristo nitafutie andiko lolote kwenye biblia kwamba yesu ameleta ukristo

maandiko yako mengi lakini hata nikikuwekea hautaamini, utaanza kuleta sababu nyingine nyingi tu. hadi msahafu unautambua ukristo sembuse biblia? si zaidi sasa? jitahidi ufaham maana ya ukristo mkubwa.

kabla hujapewa aya toka kwenye biblia, soma kwanza hii

SURA 2. SURA AL- BAQARA 62. Hakika Walio amini, na Mayahudi na Wakristo, na Wasabai; yeyote atakaye
muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho na akatenda mema basi watapata malipwa
yao kwa Mola wao Mlezi, wala haitakuwa khofu juu yao, wala hawatahuzunika.


 
ha ha haa sijui nikwambiaje kwanza nikuulize unajua maana ya islam chunguza kwanza ujue maana yake ndio ulinganishe na huo mwaka ulioandika kwanza Yesu (issa) hakuleta ukristo nitafutie andiko lolote kwenye biblia kwamba yesu ameleta ukristo

kwa mujibu ya dini yako YESU ni nabii wa 23 na muhammad wa 24, yaani wa mwisho. Je uwislam na ukristo upi ulianza ikiwa YESU alikuja kuukomoboa ulimwengu baada ya anguko la adamu na muhammad kueneza dini yaani kupinga kile alicholeta YESU na manabii waliomtangulia.
 
Hivi tumefikia hatua hii ya kuchinjana sisi kwa sisi badala ya wanyama?.

Binafsi siamini kama hawa ni watanzania,yawezekana ni wavamivi kutika nje waliopitia kwenye ngongo wa dini ili kueneza machafuko.

Ipo haja sasa kwa serikali kupitia mchakato wa vitambulisho vya taifa kuwabaini mara moja wale wote ambao si raia wake na kuwapeleka kunakostahili.

Mbali na hivyo vurugu hizi yawezekana ni muendelezo wa fitina juu ya siasa kupitia dini,hii ni hatari sana ndugu zangu kwa sisi kama watanzania wenye nia njema na mapenzi mema kwa nchi yetu.

Sote ebu tuiombe serikali kukaa pamoja na viongozi wa dini na hatimaye kutoka na mwafaka wa kadhia hii ambao si kwamba inawadhililisha watanzania bali inawadhalilisha viongozi wa dini na serikali.
 
Serikali dhaifu inatupeleka kuzimu sasa.
Sawa sawa mkuu
naona baada ya kukatazwa ng'ombe wameamua kumchinja mchungaji hahaha
waislam bana ndio maana marekani na nchi za magharibi hawataki kusikia
kabisa hii kitu, waislam wa huko ulaya ni majina tuu ila hawana
itikadi.
 
Vile vyobo vya habari vilivyokuja na taarifa kwamba mgogoro wa kidini kanda ya ziwa umeisha baada ya wasira kuteta na viongozi wa dini walitaka kutufurahisha,kutudhalilisha,kujipendekeza(kwa wananchi na viongozi) au udhaifu walionao katika kutuletea habari zilizofanyiwa uchunguzi yakinifu
 
jamani nimesema kati ya walioenda kununua nyama pale wengine wachoma mishikaki na mama ntilie ambao wanahudumia public,sasa hapa wapi huelewi?

Kwani lazima ukale kwa huyo mama ntilie? Embu waislam tuache UJINGA, Kwa hili tunazidi kutia Aibu na tunaendelea kuonekana wa ajabu.
 
kabla ya uchaguz yalisemwa udini wakapinga kwa nguvu zote yametokea na hata watoa matangazo nao wanahucka ila kwa vile wao ni watawala kimya
 
Ni kama ambavyo waislamu wangenunua nyama ya ibada yao wakaenda kuchoma mishikaki na kuuza mahotelini.

kwahiyo leo ndo mmejua mlikua mkila nyama kinyume na mafundisho yenu?.
Anyway,hulazimishwi ila ukitaka kufanya biashara ya nyamafu hakikisha hata kwenye mahoteli inapoenda unaweka tangazo ili wasiokula nyamafu wasije kununua sawa.maana usipofanya hivo na wakagundua umewalisha nyamafu lazima pataleta shida
 
MKUU
aha sasa nimewaza maana hapa wenzetu wanajifanya ushabiki wa imani ambayo ukichunguza sana hupati mantiki.
sasa kama swala ni imani ya kula kilichosaliwa na lazima awe muislamu ndio kachinja je hii ni kwa ng'ombe na mbuzi na kuku na kondoo na kanga tu au kwa kila chenye uhai? maana ndege na senene na pweza ,na samaki wanaovuliwa na wakristo na vinginevyo?
mimi nafikiri wakikaa sana na kujiuliza wanaweza wakabadili mitazamo yao

Halafu kuna hizi nyama za polini kama swala ambazo uwindaji wake ni kwa bunduki, kule kwetu kijijini tunawinda kwa mkuki!
 
Ewe mwenyezmungu tuepushe na vurugu zisizo na ulazima tuketi pamoja tuzungumze yale yote na tuyatatue...
 
kwahiyo leo ndo mmejua mlikua mkila nyama kinyume na mafundisho yenu?.
Anyway,hulazimishwi ila ukitaka kufanya biashara ya nyamafu hakikisha hata kwenye mahoteli inapoenda unaweka tangazo ili wasiokula nyamafu wasije kununua sawa.maana usipofanya hivo na wakagundua umewalisha nyamafu lazima pataleta shida

shida ndo iko hapo,maana hiyo NYAMA haiishii machinjion,jaman hata ulaya kuna mzozo wa nyma za faras,
muislam kula nyama isiyochinjwa na muislam ni kharam mutlakha,
na hata huyo alochinjwa na muislam lazima awe amechinjwa kwa misingi maalum
 
Inabidi tuwe makini sana na hizi Redio na Televisheni za madhehebu ya dini kwani nazo zinachochea sana vurugu hii.

kwa hatua tuliyofikia ndg.hakuna haja ya kuwa na hivi vituo kwa upande mwingine wa sarafu,hakuna msimamizi kabisa wa vyombo vya habari labda kama unaandika mambo ya kisiasa ndiyo utafuatiliwa mno lakini mengine ongea uwezavyo,tukana dini nyingine uwezavyo wasimamizi wameuchapa usingizi wa pono lakini mpaka kesho hawatastuka mpaka wasikie kituo fulani cha tv/radia kimechomwa ndiyo uwasikie hapo watakwambia wanayafungia magazeti ata ambayo hayajawahi kuandika aina yoyote ya uchochezi,TUMUOMBENI SANA MUNGU ATUPE BUSARA AMBAYO SI TU KWAMBA INATAKA KUPOTEA BALI ISHAPOTEA SIKU NYINGI.
 
Huu moto ulioanza hauwezi kuzimwa kwa wingi wa askari na mitutu ya bunduki. Kama walidhani sisi hatuna akili basi waelewe kuwa tunazo. Mkristo m1 akiuawa wajiandae kuchinjwa w3. Kanisa 1 likibomolewa wajiandae kujenga misikiti kumi.

Yale ya kupigwa shafu unageuza la 2 yamepitwa na wakati. Yesu mwenyewe alipoona wabishi aliwachapa wakiwa hekaluni!

Genekai!
 
maandiko yako mengi lakini hata nikikuwekea hautaamini, utaanza kuleta sababu nyingine nyingi tu. hadi msahafu unautambua ukristo sembuse biblia? si zaidi sasa? jitahidi ufaham maana ya ukristo mkubwa.

kabla hujapewa aya toka kwenye biblia, soma kwanza hii

SURA 2. SURA AL- BAQARA 62. Hakika Walio amini, na Mayahudi na Wakristo, na Wasabai; yeyote atakaye
muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho na akatenda mema basi watapata malipwa
yao kwa Mola wao Mlezi, wala haitakuwa khofu juu yao, wala hawatahuzunika.



hivi unajua ni kwanini UYAHUDI HAUUTAJI UKRISTO WALA HAWAMTAJI YESU.
Kwanini ukristo unautaja uyahudi lakini hautaji uislamu.
Na kwanini Uislamu imeutaja uyahudi na ukristo na manabii wake.
 



4.jpg





TAARIFA kutoka kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) zilizotumwa katika mitandao ya Kijamii na Bi Hellen Kijo bisimba mchana huu zinapasha kuwa kuzuka vurugu na kusababisha majeruhi huko Wilayani Chato.





Tumepokea taarifa za masikitiko kuhusu vurugu zilizotokea huko Buselele Chato kuhusu uchinjaji wa nyama unaobishaniwa na Waislam na Wakristo.

Chanzo cha Habari hizi kimetueleza kuwa baada ya mivutano kuhusu uchinjaji wa nyama.

Baaadhi ya Wakristo waliamua kuanzisha bucha ya ili wachinje na kununua hapo ili wasishiriki kula nyama zilizochinjwa kama sehemu ya ibada ya Kiislamu kwa vile uchinjaji kwa Waislam ni ibada.

Baada ya kufungua Bucha hiyo leo asubuhi taarifa inasema watu wanaosadikiwa kuwa waislam walifika kutaka kuifunga hiyo Bucha na baadaye Polisi nao walifika na walitaka wamchukue mwenye bucha hiyi.

Suala hili likazua tafrani na pakatokea mapigano kati ya pande mbili yaani waislam na wakristo na kuna watu wameumizwa.

Taarifa imezidi kueleza kuwa pia mali za aliyehamasisha ufungwaji wa bucha nazo zimeharibiwa.

Baada ya kupokea taarifa hii tumewatuma waangalizi wetu wa haki za binadamu kwenda kutuletea kwa kina hali halisi kama watakavyoweza.

Tunahabari kuwa kikosi cha kuzuia fujo kilifika na kutuliza hizo vurugu.Jambo tunaloliona kwa haraka ni kuwa kunaelekea kukosekana kwa uongozi wa kuyatazama masuala kama haya na kuyawekea msimamo na maelekezo kabla vurugu kama hizi kutokea.

Pili tunaona kuwa hali ya kukosa stahamala za kidini inajengeka nchini jambo ambalo ni hatari sana kwa usalama na amani hapa nchini.Wakati tunasubiri taarifa zaidi tunapenda kutoa angalizo kwa viongozi wetu maana tumesikia mkuu wa wilaya tayari ameshafika katika eneo la tukio.

Masuala kama haya yatazamwe kwa mujibu wa sheria na sheria zifuatwe lakini pia kwa kuzingatia haki za binadamu na hususani haki za kiraia na kiutamaduni ambazo zinatoa uhuru wa ibada na kila mtu asiingiliwe katika haki hizi.

Lakini pia njia za utatuzi wa migogoro ya aina hii isifanywe kijuujuuu bali pawe na nafasi yamaongezi ya kina ya uchambuzi wa kiini cha mgogoro.

Tutaweza kutoa taarifa zaidi tutakapopokea taarifa kutoka kwa waangalizi wetu wa kiini na matokeo ya mgogoro au vurugu hizi


Chanzo Juma Mtanda Blog

Mimi sitaki hata kusikia masuala ya viongozi,kwa sababu hawa ndio chanzo cha mambo haya yote,wamekuw wakicheka tu watu wanapoto maonyo,hili la Buselesele na Katoro sio la kwanza lilianza tangu mapema mwezi wa kwanza,lakini Ma DC,wa pande zote mbuili na RC wamekuwa wakicheka tu,na cha ajabu sasa leo Mkuu wa wilaya ya Chato Lodrick Mpogoro amewapiga marufuku wananchi kuzungumza na vyombo vya habari pamoja na mashirika mbalimbali zikiwemo asasi za kiraia eti mpaka kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya na Mkoa zikae na kujadili vurugu hizo,sasa huyu mtu huyu unadhani yuko sawa kweli?!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom