Buriani Rashid Mbuguni, Mzalendo aliyedhulumiwa kiwanda amekufa hajaona haki

Rashid Mbuguni mimi nakumbuka kawapa kazi za kuanzia maisha na muelekeo rafiki zangu vijana wengi sana wa Dar. Wengine waliishi maisha ya Kinyamwezi, mtu ndiyo kwanza kamaliza sekondari na hapo hapo anafanya kazi nzuri tu by our standards hapo Business Times.

Aliwajali sana vijana wadogo wanaoanza maisha, wengine wakiwa chini sana kwake kidaraja kazini, akiongea nao wakiwa wageni kazini, na kuwapa ushauri mzuri, mara nyingi wakiwa hata hawamjui kuwa huyu ni bosi mkubwa kabisa, kwa jinsi alivyojiweka simple

Kwenye circle yangu tu kuna vijana wengi wanasimulia alivyokuwa mtu poa.

Live clean and let your work be seen.
-Peter Tosh

Ametimiza kazi hiyo.

Pole sana kwa wafiwa.
 
Kwa ufupi, Mengi, E. Massawe, Mbuguni na Nyaulawa walikua National Auditing kwa wakat mmoja na inasemekana utajiri wao waliutoa huko haswa kipindi cha maandalizi ya zoezi la ubinafsishaji.
Mkuu liilikuwa shilika gani Tanzania Auditing Corporation (TAC) au National Auditing?
 
Rashid Mbuguni Afariki Dunia.

Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya kuondoka duniani kwa Ndugu Rashid Mbuguni.
Apumzike Kwa Amani.

Maggid

Luqman Maloto anaandika:
Luqman Maloto

“MZALENDO ALIYEDHULUMIWA KIWANDA AMEKUFA HAJAONA HAKI

NAKUMBUKA mwaka 1999. Mara ya kwanza naingia chumba cha habari. Business Times Ltd (BTL).

Newsroom yenye hadhi. Nilivutiwa na chumba kikubwa cha wachoraji. Kizuri sana, kiliundwa kwa vioo. Kila kijana mwenye kipaji cha kuchora, alipaona nyumbani.

BTL, nyumba ya magazeti ya Business Times, Majira, Spoti Starehe, Sanifu, Dar Leo na Maisha. Mamia ya Watanzaia waliajiriwa direct. Maelfu indirect.

Kila kitu kilianza na fikra zilizoishi mbele ya muda, za wazalendo Richard Nyaulawa na Rashidi Mbuguni. Hatimaye, wote sasa ni marehemu.

Nyakati sekta binafsi ikitafsiriwa kuwa mtoto wa haramu, Nyaulawa na Mbuguni walithubutu na waliibeba kwa ujasiri na mawazo yenye ujazo mkubwa.

Kampuni yao, Business Care Limited (BCS), ikazaa BTL, iliyosajili na kuchapa gazeti la kwanza binafsi Tanzania, Business Times. Mwaka 1989.

Wakati wowote, historia ya vyombo vya habari binafsi Tanzania ikiandikwa, majina ya Nyaulawa na Mbuguni, yanastahili wino wa dhahabu.

Gazeti la Business Times, lilizaa Majira mwaka 1992. Baada ya hapo, magazeti zaidi ya kampuni binafsi yalizaliwa, kisha redio na televisheni. BTL ya Nyaulawa na Mbuguni, ilifungua njia.

Nyaulawa na Mbuguni, walianzisha kampuni ya uchapaji ya Business Printers Limited (BPL). Kiwanda cha BPL kilikuza mno tasnia ya habari.

BPL, haikuchapa magazeti ya BTL pekee, bali yote ya kampuni binafsi wakati huo. Vilevile vitabu, majarida na machapisho mbalimbali. Nyaulawa na Mbuguni ni wazazi na walezi wa kila gazeti lililozaliwa miaka ya 1990.

Uchaguzi Mkuu 1995, Nyaulawa na Mbuguni, waliandaa mdahalo wa kihistoria wa wagombea urais. Tukio hilo halijawahi kujirudia nchini.

Nyaulawa na Mbuguni ni Watanzania wa kwanza kuonesha kuwa sekta binafsi inaweza kushirikiana na Serikali, kutatua changamoto za wananchi.

Kupitia BCS, walianzisha miradi ya kushughulikia kero za maji, mikoa mbalimbali nchini. Baadaye, kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Sweden (Sida), Nyaulawa na Mbuguni, waliendesha Mpango wa Afya kupitia Maji Salama (Hesawa) kwa zaidi ya miaka 10.

Kupitia Hesawa, Nyaulawa na Mbuguni, waliwezesha Watanzania zaidi ya milioni tano wa vijijini, hususan Kanda ya Ziwa, kupata maji safi na salama.

Nyaulawa na Mbuguni, walijenga hamasa ya mtaji kwa Watanzania, na wakashawishi wachache kutoka nje, wakaanzisha Benki ya Biashara ya Akiba – Akiba Commercial Bank (ACB), mwaka 1997.

Desemba 1998, Nyaulawa na Mbuguni, walifanikisha kuileta Tanzania, taasisi ya kimataifa ya Junior Achievement Worldwide, yenye makao yake makuu, Colorado, Marekani.

Junior Achievement (AJ), hufundisha vijana elimu ya biashara na uwekezaji. Tangu kuwasili Tanzania, AJ imetengeneza maelfu ya vijana kuwa wafanyabiashara stadi.

Vicoba ni maarufu hivi sasa. Asili yake ni Vibindo. Nyaulawa na Mbuguni, walianzisha Vibindo mwaka 2002, kuwezesha Watanzania kuweka, kukopa na kusaidiana katika vikundi. Vibindo ndio sasa Vicoba.

Nyaulawa na Mbuguni ni waasisi wa Taasisi ya Utafiti na Kuondoa Umaskini (Repoa), ambayo tafiti zake zimekuwa mwanga kwa Serikali, Bunge na taasisi za kimataifa, katika kukabili umaskini Tanzania.

Mwaka 1990, Nyaulawa na Mbuguni, waliratibu mafunzo ya kilimo cha mwani (seaweed) kwa mara ya kwanza, kwa akina mama wa Zanzibar. Wataalamu hao walitoka Ufilipino.

Hivi sasa, mwani inashika nafasi ya tatu Tanzania kwa usafirishwaji nje ya nchi, ni namba tatu kwa mapato Zanzibar, na inachukua hadi asilimia 90 ya huduma za usafiri wa maji Zanzibar kwenda nje.

Nyaulawa na Mbuguni ndio waasisi wa biashara za kutembeza mkononi, yaani umachinga. Waliasisi hilo kupitia kuuza magazeti mikononi. Wakawa na mtandao wa vijana waliozunguka Dar es Salaam. Mtindo huo ukaitikiwa kwa ukubwa. Hivi sasa, mtindo huo umekuwa mtandao mpana wa ajira.

Kwa tafsiri yoyote, Nyaulawa na Mbuguni ni wazalendo wa nchi. Ni nuru ya sekta binafsi. Mageuzi ya ujamaa hadi uchumi wa soko, yana kurasa nyingi za Nyaulawa na Mbuguni. Bila swali, Nyaulawa na Mbuguni ni historia ya Tanzania.

Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Anthony Mtaka, amewahi kunieleza kuwa partnership ya Nyaulawa na Mbuguni haina mfanowe Tanzania. Walifanya mengi kibiashara na kwa nchi, kwa upacha wa hali ya juu.

Mzalendo Nyaulawa alifariki dunia mwaka 2008, akamwacha Mzalendo Mbuguni, akiendeleza waliyoyaanzisha pamoja.

Mwaka 2016, BPL chini ya Mbuguni, ilichukua mkopo benki za NMB na ECO. Fedha hizo zilitumika kununua mitambo na kufanya uwekezaji mkubwa kwenye kiwanda chake cha uchapaji. Kiwanda kikawa kipya kabisa.

Mwaka 2017, task force ya Rais wa Tano, Dk John Magufuli, ilivamia BPL. Wamiliki waliondolewa. Kiwanda kikawa chini ya usimamizi wa Idara ya Usalama wa Taifa.

Kuanzia hapo, magazeti ya CCM, Uhuru, Mzalendo na Burudani, ya Serikali, Daily News, Sunday News na Habari Leo, kwa nyakati tofauti, yalichapwa bure BPL.

Magazeti mengine, Tanzanite, Fahari Yetu, La Jiji, Tanzania Perspective, The Echo, Observer na mengine mengi, yaliyoitwa ya kimkakati, yalichapwa bure BPL.

Kura za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019 na Uchaguzi Mkuu 2020, zilichapwa BPL.

Wakati yote yakifanyika, Mbuguni na familia ya Nyaulawa, walipitishwa kwenye moto unaounguza. Mali zao, ikiwemo nyumba, kupigwa minada. Presha kubwa ya mikopo ya NMB na ECO.

Haitoshi, task force ya Magufuli, ilimtishia Mbuguni kumfungulia mashitaka ya uhujumu uchumi, vinginevyo alipe mamilioni kwa kushirikiana na familia ya Nyaulawa.

Kwa hofu ya kesi ya uhujumu uchumi, walikubali kulipa kwa awamu. Ajabu, wakaelekezwa kulipa benki kwenye akaunti ya mtu binafsi. Na wakalipa.

Nilimshuhudia Mbuguni akiwa kwenye mahangaiko, akipigania kiwanda chake. Panda shuka bila mafanikio.

Jana, Julai 15, 2023, Mzalendo Mbuguni, aliitikia wa wito wa mauti. Naam, kila nafsi itaonja mauti.

Mbuguni amefariki dunia akiwa bado anasotea haki yake. Kiwanda chake ambacho hakurudishiwa tangu kilipoporwa mwaka 2017.

Mtanzania aliyetenda mengi kwa nchi. Aliyebadili maisha ya maelfu kupitia mipango na ajira za moja kwa moja, nyakati za mwisho za uhai wake, zilijaa maumivu makali kwa sababu ya dhuluma. Amekufa maskini na mufilisi.

Kesho (Julai 17, 2023), Mzalendo Mbuguni atazikwa makaburi ya Kisutu. Sala ya maiti, itafanyika Msikiti wa Maamur, Upanga, Dar es Salaam.

Sisi Sote ni wa Mwenyezi Mungu na Kwake Tutarejea.

Ndimi Luqman MALOTO”
Wapumzike kwa Amani! Katiba mpya muhimu!
 
Magufuli uendelee kulaanika wewe binafsi watoto wako na mama Janeth hawana hatia ila wewe magufuli KWA uliyoyafanya duniani ulaaniwe milele.
Na mdau wake Samia bado anaendeleza kazi!
 
Mkuu, namnukuu mtu mmoja hapa.

Anasema kuna mfanyabiashara mmoja alikuwa na deals zake ku supply nyama kwenye mahoteli. Alikuwa na shilingi bilioni 4 benki. Magufuli akazikomba zote. Jamaa mpaka leo kachanganyikiwa anaongea mwenyewe njiani, karudi kuajiriwa.

Kuna wafanyabiashara kibao wamefanya biashara za mazao miaka na miaka, Magufuli kaja kakomba hela zao zote.

Halafu, hizo hela na zile za plea bargaining, zimeingia katika akaunti binafsi, si akaunti za serikali. Hili hata Samia kalisema.

Sasa mpaka hapa hatuoni U Mafia wa Magufuli tu?

Mpaka leo, Magufuli ameangusha sana imani kwenye banking system ya Tanzania.

Halafu watu wanajitoa akili kumsifia?
Mkuu mimi pana mtoto mdogo nashuka Kilimanjaro Airport alitaka kunisumbua eti anauliza mbona nasafiri mara kwa mara alikua uhamiaji nilimuuliza hizi passport mnatoa za nini na pia hayo maswali huwezi kuniuliza wewe mtoto mdogo miaka naanza kusafiri hata shule haujaanza alikua na vinyotanyota vyake eti atanionyesha nilimwambia na wiki ijayo nasafiri njoo unizuie kila mjinga alijifanya anaweza kufanya kitu chochote kwa cheo chake nilimkariri yule dogo baadae kidogo mzee alivyofariki sikumuona pale nilisikia alikua ndio risasi kidole wao ili mambo ya Bank yanaanzia kwake kwa wasafiri niliumia sana aisee ila sijakaona tena kale kapuuzi nikikaulizia sipati majibu kapo wapi?..
 
...Sijaona Popote Marehemu Mbuguni alifariki akiwa na Miaka Mingapi au alizaliwa Mwaka Gani??
Ninaomba Kujuzwa....
 
Tatizo la Masikini wengi huwa hawapendi kujua upande wa giza wa tajiri,hata Kama anauuza viuungo vya Binaadamu wao hawajali,na wanacho angalia wao ni ule msaada wanaopata kutoka kwa Mafisadi!!

Hivi huo uuzaji wa viungo vya binadamu unaosema na unasemwasemwa ulishawahi kuuona na kuuthibitisha wapi?
Kwa akili zako unaamini kabisa ipo biashara ya kuuza viungo vya binadamu? Hivi viungo vinauzwa kwa ajili ya nini na wapi lilipo soko lake...?!
Itapendeza pia ukitoa mifano ama majina ya matajiri/watu wanaofanya/waliowahi kufanya biashara hiyo!
 
Usitumie nguvu unajua mtu hawezi from no where achukue pesa ya mtu bila sababu, mi mwemyewe kuna nyumba yetu ilipitiwa na hayati kipindi cha upanuzi wa barabara ya morogoro, niliumia sana ila hua simlaumu maana kiuhalisia mzee wetu alikula sehem hifadh ya barabara ili kujenga shule siku za usoni so kuna hisia na hualisia wa jambo.

Mi nafikiri mnapokua mnasema vitu vibaya alivyofanya kuweni waungwana mseme na sababu zilizomfanya kufanya vile ziwe nzuri ama mbaya, naamini hakua chizi kuzichukua izo fedha labda kama ni wasadizi wake ndani ya serikali yake na sio yeye.
Mtetee, na hizo hela kuziweka ktk account binafsi je, inamaanisha nini?
 
Rashid Mbuguni Afariki Dunia.

Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya kuondoka duniani kwa Ndugu Rashid Mbuguni.
Apumzike Kwa Amani.

Maggid

Luqman Maloto anaandika:
Luqman Maloto

“MZALENDO ALIYEDHULUMIWA KIWANDA AMEKUFA HAJAONA HAKI

NAKUMBUKA mwaka 1999. Mara ya kwanza naingia chumba cha habari. Business Times Ltd (BTL).

Newsroom yenye hadhi. Nilivutiwa na chumba kikubwa cha wachoraji. Kizuri sana, kiliundwa kwa vioo. Kila kijana mwenye kipaji cha kuchora, alipaona nyumbani.

BTL, nyumba ya magazeti ya Business Times, Majira, Spoti Starehe, Sanifu, Dar Leo na Maisha. Mamia ya Watanzaia waliajiriwa direct. Maelfu indirect.

Kila kitu kilianza na fikra zilizoishi mbele ya muda, za wazalendo Richard Nyaulawa na Rashidi Mbuguni. Hatimaye, wote sasa ni marehemu.

Nyakati sekta binafsi ikitafsiriwa kuwa mtoto wa haramu, Nyaulawa na Mbuguni walithubutu na waliibeba kwa ujasiri na mawazo yenye ujazo mkubwa.

Kampuni yao, Business Care Limited (BCS), ikazaa BTL, iliyosajili na kuchapa gazeti la kwanza binafsi Tanzania, Business Times. Mwaka 1989.

Wakati wowote, historia ya vyombo vya habari binafsi Tanzania ikiandikwa, majina ya Nyaulawa na Mbuguni, yanastahili wino wa dhahabu.

Gazeti la Business Times, lilizaa Majira mwaka 1992. Baada ya hapo, magazeti zaidi ya kampuni binafsi yalizaliwa, kisha redio na televisheni. BTL ya Nyaulawa na Mbuguni, ilifungua njia.

Nyaulawa na Mbuguni, walianzisha kampuni ya uchapaji ya Business Printers Limited (BPL). Kiwanda cha BPL kilikuza mno tasnia ya habari.

BPL, haikuchapa magazeti ya BTL pekee, bali yote ya kampuni binafsi wakati huo. Vilevile vitabu, majarida na machapisho mbalimbali. Nyaulawa na Mbuguni ni wazazi na walezi wa kila gazeti lililozaliwa miaka ya 1990.

Uchaguzi Mkuu 1995, Nyaulawa na Mbuguni, waliandaa mdahalo wa kihistoria wa wagombea urais. Tukio hilo halijawahi kujirudia nchini.

Nyaulawa na Mbuguni ni Watanzania wa kwanza kuonesha kuwa sekta binafsi inaweza kushirikiana na Serikali, kutatua changamoto za wananchi.

Kupitia BCS, walianzisha miradi ya kushughulikia kero za maji, mikoa mbalimbali nchini. Baadaye, kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Sweden (Sida), Nyaulawa na Mbuguni, waliendesha Mpango wa Afya kupitia Maji Salama (Hesawa) kwa zaidi ya miaka 10.

Kupitia Hesawa, Nyaulawa na Mbuguni, waliwezesha Watanzania zaidi ya milioni tano wa vijijini, hususan Kanda ya Ziwa, kupata maji safi na salama.

Nyaulawa na Mbuguni, walijenga hamasa ya mtaji kwa Watanzania, na wakashawishi wachache kutoka nje, wakaanzisha Benki ya Biashara ya Akiba – Akiba Commercial Bank (ACB), mwaka 1997.

Desemba 1998, Nyaulawa na Mbuguni, walifanikisha kuileta Tanzania, taasisi ya kimataifa ya Junior Achievement Worldwide, yenye makao yake makuu, Colorado, Marekani.

Junior Achievement (AJ), hufundisha vijana elimu ya biashara na uwekezaji. Tangu kuwasili Tanzania, AJ imetengeneza maelfu ya vijana kuwa wafanyabiashara stadi.

Vicoba ni maarufu hivi sasa. Asili yake ni Vibindo. Nyaulawa na Mbuguni, walianzisha Vibindo mwaka 2002, kuwezesha Watanzania kuweka, kukopa na kusaidiana katika vikundi. Vibindo ndio sasa Vicoba.

Nyaulawa na Mbuguni ni waasisi wa Taasisi ya Utafiti na Kuondoa Umaskini (Repoa), ambayo tafiti zake zimekuwa mwanga kwa Serikali, Bunge na taasisi za kimataifa, katika kukabili umaskini Tanzania.

Mwaka 1990, Nyaulawa na Mbuguni, waliratibu mafunzo ya kilimo cha mwani (seaweed) kwa mara ya kwanza, kwa akina mama wa Zanzibar. Wataalamu hao walitoka Ufilipino.

Hivi sasa, mwani inashika nafasi ya tatu Tanzania kwa usafirishwaji nje ya nchi, ni namba tatu kwa mapato Zanzibar, na inachukua hadi asilimia 90 ya huduma za usafiri wa maji Zanzibar kwenda nje.

Nyaulawa na Mbuguni ndio waasisi wa biashara za kutembeza mkononi, yaani umachinga. Waliasisi hilo kupitia kuuza magazeti mikononi. Wakawa na mtandao wa vijana waliozunguka Dar es Salaam. Mtindo huo ukaitikiwa kwa ukubwa. Hivi sasa, mtindo huo umekuwa mtandao mpana wa ajira.

Kwa tafsiri yoyote, Nyaulawa na Mbuguni ni wazalendo wa nchi. Ni nuru ya sekta binafsi. Mageuzi ya ujamaa hadi uchumi wa soko, yana kurasa nyingi za Nyaulawa na Mbuguni. Bila swali, Nyaulawa na Mbuguni ni historia ya Tanzania.

Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Anthony Mtaka, amewahi kunieleza kuwa partnership ya Nyaulawa na Mbuguni haina mfanowe Tanzania. Walifanya mengi kibiashara na kwa nchi, kwa upacha wa hali ya juu.

Mzalendo Nyaulawa alifariki dunia mwaka 2008, akamwacha Mzalendo Mbuguni, akiendeleza waliyoyaanzisha pamoja.

Mwaka 2016, BPL chini ya Mbuguni, ilichukua mkopo benki za NMB na ECO. Fedha hizo zilitumika kununua mitambo na kufanya uwekezaji mkubwa kwenye kiwanda chake cha uchapaji. Kiwanda kikawa kipya kabisa.

Mwaka 2017, task force ya Rais wa Tano, Dk John Magufuli, ilivamia BPL. Wamiliki waliondolewa. Kiwanda kikawa chini ya usimamizi wa Idara ya Usalama wa Taifa.

Kuanzia hapo, magazeti ya CCM, Uhuru, Mzalendo na Burudani, ya Serikali, Daily News, Sunday News na Habari Leo, kwa nyakati tofauti, yalichapwa bure BPL.

Magazeti mengine, Tanzanite, Fahari Yetu, La Jiji, Tanzania Perspective, The Echo, Observer na mengine mengi, yaliyoitwa ya kimkakati, yalichapwa bure BPL.

Kura za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019 na Uchaguzi Mkuu 2020, zilichapwa BPL.

Wakati yote yakifanyika, Mbuguni na familia ya Nyaulawa, walipitishwa kwenye moto unaounguza. Mali zao, ikiwemo nyumba, kupigwa minada. Presha kubwa ya mikopo ya NMB na ECO.

Haitoshi, task force ya Magufuli, ilimtishia Mbuguni kumfungulia mashitaka ya uhujumu uchumi, vinginevyo alipe mamilioni kwa kushirikiana na familia ya Nyaulawa.

Kwa hofu ya kesi ya uhujumu uchumi, walikubali kulipa kwa awamu. Ajabu, wakaelekezwa kulipa benki kwenye akaunti ya mtu binafsi. Na wakalipa.

Nilimshuhudia Mbuguni akiwa kwenye mahangaiko, akipigania kiwanda chake. Panda shuka bila mafanikio.

Jana, Julai 15, 2023, Mzalendo Mbuguni, aliitikia wa wito wa mauti. Naam, kila nafsi itaonja mauti.

Mbuguni amefariki dunia akiwa bado anasotea haki yake. Kiwanda chake ambacho hakurudishiwa tangu kilipoporwa mwaka 2017.

Mtanzania aliyetenda mengi kwa nchi. Aliyebadili maisha ya maelfu kupitia mipango na ajira za moja kwa moja, nyakati za mwisho za uhai wake, zilijaa maumivu makali kwa sababu ya dhuluma. Amekufa maskini na mufilisi.

Kesho (Julai 17, 2023), Mzalendo Mbuguni atazikwa makaburi ya Kisutu. Sala ya maiti, itafanyika Msikiti wa Maamur, Upanga, Dar es Salaam.

Sisi Sote ni wa Mwenyezi Mungu na Kwake Tutarejea.

Ndimi Luqman MALOTO”
Mifano kwq vijana kushirikiana ili kuleta mabadiliko kwenye jamii zetu. Hawa jamaa sijawahi waskia, lakini ni funzo zuri kwetu kujituma na kuona fursa za mbele zaidi. Mwenyezi mungu awapumzishe kwa amani
 
Kabla ya kumuhukumu Magufuli ingekua vizuri Kama tungepata na story za upande wa pili,ili tujuwe Nini zilikua sababu za kutaifishwa kwa hiyo mitambo! Unaweza kuta Mshikaji nae alikuwa fisadi, na ni kawaida sana fisadi kupendwa na Watanzania masikini kisa tu kuna visenti anatoa kwa walala hoi!!
Story ya upande mmoja hii, hata kama Magu alikua konyo ila lazima kuna sababu eidha za kipuuzi au za maana kufanya hivyo.
 
Unatetea vitu usivyovijua kwa logical non sequitur na mahaba uliyo nayo kwa Magufuli.

Kama nyie mmebomolewa nyumba iliyokuwa kwenye hifadhi ya barabara kwa uzembe wenu, hilo halina maana kwamba hakuna watu waliofanyiwa u Mafia bila sababu za msingi.

Magufuli alikuwa na sababu gani za kutaifisha mitambo ya Business Times zaidi ya kutaka kuminya uhuru wa habari tu?

Alikuwa na sababu gani?

Na kwa nini hela alizokuwa anachukua, kama za okea bargaining na za Bureaus, alikuwa anaweka katika akaunti binafsi ambazo hata serikalini hazijulikani?

Logical non sequitur it doesn’t work here,
Siwezi kujibu vile unavyotaka kama hatujameet kwenye point ya makubaliano ya kuweka kosa la uyo hayati bayana.

Sijatetea nimejaribu kuelabolate tukio na chanzo chake openly kwa mfano hai ili na wewe unipe deep data za chanzo cha hayati kufanya ivo.

Unaweza kuta hayati na uyo mzee walikua wanapersonal issues, hayati alipopata nasafi akaamua kumkomesha kitu ambacho sio sawa kutumia power ulonayo kwa mambo binafsi, huo ni mfano so wewe inatakiwa ulete chanzo sio unatuonesha tukio af unasema aliamka tuu hasbui kama mtu mwenye majini akafika aka chukua vifaa!!! Hell no,

Lastly, kuhusu kukandamiza vyombo vya habari unahisi ni kosa la hayati!? No, since vyombo vya habari vinaendeshwa kwa sheria na kanuni za nchi that means havipo huru, na ninachojua mimi hakuna uhuru usiokua na mipaka kwaiyo ukinimbia amekandamiza uhuru bado haingii akilini wakati kimsingi huo uhuru wenyewe haupo.

so badala ya kumlaumu mtu ungejikita kuelezea jinsi katiba yetu ilivyombovu hapo ningekuelewa maana yawezekana soon akazaliwa mwingine kama uyo alieondoka na akaja tena kufanya yaleyale alio yafanya mwendazake maana kikatiba anayo mamlaka ya kuamua ivo,

Inshot raisi anauhuru wakukupiga unapomkosea au kusamehe na anaweza tumia kisu,rungu au fimbo so ni mood yake na hekima ndo vitamwongoza akubamize na nini ama akusamehe, kwaiyo mkuu leta chanzo tuongee kama watu wazima.
 
Warithi wake lifikisheni hili suala kwa mama mpenda haki.
Mama mpenda haki alikuwa wapi kumrudishia kiwanda mpaka anakufa? Magufuli toka kufariki kwake mpaka leo hii aliondoka na mafaili ya kiwanda.. huu ujinga acheni....wao walikopa wakashindwa kurudisha fedha za ECO na NMB, Bank zikashika mali zao leo hii mnamsingizia JPM. Naawambia hata yule mjinga mwingine alidai Mbowe alikamatwa wakati wa JPM (uchawa ni laani mpya)... hata hili la DPW watasema JPM ndio aliwaleta.. takataka wahed.
 
Unatetea vitu usivyovijua kwa logical non sequitur na mahaba uliyo nayo kwa Magufuli.

Kama nyie mmebomolewa nyumba iliyokuwa kwenye hifadhi ya barabara kwa uzembe wenu, hilo halina maana kwamba hakuna watu waliofanyiwa u Mafia bila sababu za msingi.

Magufuli alikuwa na sababu gani za kutaifisha mitambo ya Business Times zaidi ya kutaka kuminya uhuru wa habari tu?

Alikuwa na sababu gani?

Na kwa nini hela alizokuwa anachukua, kama za okea bargaining na za Bureaus, alikuwa anaweka katika akaunti binafsi ambazo hata serikalini hazijulikani?
Ungejua kwanini mpaka nyumba zao ziliuzwa ungekuwa umetumia akili yako vizuri.
 
Acha kutetea upumbavu. Kama hukuwa na hela wakati wa Magu huwezi kuelewa kinachozungumzwa. Huyo mzee hakuwa na urafiki akiona akaunti imenona. Ubaya ni kuwa alikuwa haangalii sura CCM sijui CHADEMA akiona mpunga tu anakomba. Ilifika wakati kama unadaiwa kodi na akaunti ina hata 20m wanaikomba bila hata kukujulisha. Maskini peke yao ndo hawaujui muziki wa roho mbaya iliyokuwepo.

Mpaka umenichekesha, kwanza jua sina hasira na mtu, na hasa akinizidi nguvu au maarifa hua natuliza akili alafu nangalia jinsi yakucheza nae.

Binafsi yalinikumba mengi tuu hasa swala la machinga walipokua huru lilifanya nkafunga hadi duka maana kodi zilikua juu hasa vitu vya electronics na wakati chinga hawaachi ela tofauti na sisi tulio kwenye mfumo maalum na tunalipa kodi nyingi tuu.

*Ok naomba uniambie kama unadaiwa kod ulitaka na hujaenda kuclear installment zako ulitaka wakuchum ili ukatoe pesa yao!? Na je ushawahi kukaa ukasoma policy za benk unayotunzia pesa ziko?

Mi mpaka sasa nimkwepaji mzuri wa kodi ila nikikamatwa siwezi kulaumu serikali/kiongozi nitajilaumu mwenyewe kwa kushidwa kua smart mpaka nimekamatwa, na huo ndo ukweli mkuu, don’t hate the game hate how you play it.
 
Back
Top Bottom