TAWA
JF-Expert Member
- Jun 23, 2013
- 3,667
- 1,566
Unakaribia mwaka sasa toka tuzindue sera mpya ya elimu ambayo inatafsiriwa kwamba ni mpya, utekelezaji wake tunaambiwa utakuwa ni kuanzia mwakani, siyo mbaya yote ni heri. Yaloliolyomo ndani ya sera yenyewe machache ni ya kuchekesha na yanaonesha kabisa kwamba yanakwenda kuua elimu yetu. Kwa mfano:
1. Kuunganisha elimu ya msingi na ile ya srkondari (form one to four) kuwa moja na kuitwa elimu msingi. Hii maana yake hakutakuwa na mkwamo kutoka darasa la saba kwenda sekondari, kwamba yeyote aliyefika la saba huyo anayo sifa ya kujiunga na sekondari. Sasa najiuliza,
. tuna shule za kutosha za sekondari kupokea idadi hiyo ya wanafunzi?
. walimu nao wanatosheleza kama ile ya msingi?
. mfumo wa ufundishaji umeboreshwa vya kutosha na hao wakufunzi wamepewa elimu?
2. Elimu msingi Bure.
Sina tatizo katika hili na hasa kwa huyu raisi wetu. Maana hata yeye amesisitiza "ninaposema bure ni bure kweli". Ila na penyewe pana maswali mengi sana ya kujiuliza lakini kubwa kuliko yote ni "kama tunahitaji elimu bora au bora elimu". Naona kabisa serikali sijui kama itamudu kupeleka Capitation grants za kutosheleza katika haya mashule ya sekondari nchi nzima. Hapo ndiyo mwisho wa elimu yetu, elimu yetu inakufa tukiwa tunaitazama tena kwa sisi tusiojua kilichopo kapuni tunashangilia na kuwasifu wana siasa kwamba wamepunguza ukali wa maisha kwa kuondoa michango ya shule.
Poleni sana watanzania, BURIANI ELIMU YETU, LALA SALAMA.