Bunuasi

Bunuasi hakuwa Juha bali alikuwa na akili nyingi. Ni bora tupate hadithi zake kuona ukweli na uhondo wake!

Hadithi ni ncha saba! Hadithii hii hii imetolewa kwa mitindo na majina tafauti likiwemo la kile kitabu tulichosoma cha Abdul. Hivi kuna tafauti gani ya hadithi hii na ile ya "Mfalme yuko u*hi" au "Koti la Mfalme"?
Cha msingi hapa ni kuwa hadithi hizi nyingi zilikuwemo katika visa vya "Arabian Nights" na "Alfu Leila Uleila" na "Hadithi za Esopo", ambapo kimsingi makusanyo ya hadithi hizi asili yake ni fasihi simulizi kwa hiyo kila mtu anachukua, anafinyanga, anabadilisha kwa mujibu wa matakwa au jamii yake.
 
mkubwa Globu we ndio umechemsha, abunuas sio jitu jinga bt janja sana, lilikuwa linafanya mambo ambayo mtu mwenye akili za kawaida, kama akili zako hawawezi kufanya na ikitokea umefanya bas utatafakali pasibo majibu ya kirahisi. Abunuas ni noma!
 
dah!kweli mkuu hiki kitabu umekisoma vizuri sana,nadhani nili confuse jina la abdul na abunuasi!

Hapa vinazungumziwa vitabu viwili tofauti
1. Kitabu chenye jina la Abdul kilikuwa ni kitabu cha kiingeleza sikumbuki jina vizuri lakini ilikuwa kama "East Africa ... Book 4" na
2. Kitabu chenye jina la Abunuas kilitwa "Hekaya za Abunuasi", kilikuwa na stori nyingi na sina uhakika kama hii story ilikuwemo.
 
Abunuas hajawahi kuwa mjinga siku zote ni mwerevu na hushinda kwa logic nenda na hii;

siku moja abunuasi alinunua punda lakini hakuwa na sufuria kubwa ya kumwekea maji ya kunywa punda wake
ikabidi akaazime kwa jirani,akapata akaitumia,wakati anairejesha akachukua sufuria yake ndogo pia akampa jirani akamwambia wakati unanipa sufuria yako kumbe ilikuwa inamimba imejifungua kwa hiyo nimeona si uungwana kukudhurum nimekuletea na mtoto wake.jirani alifurahi sana na kumshukuru abunuas
baada ya siku mbili abunuas akaenda kuazima tena jirani akampa bila hiyana akijua kwa abunuas sufuria itazaa!
Baada ya siku akaenda kwa jirani akiwa na huzuni akamwambia jiran nasikitika kukutaarifu ile sufuria yako imekufa!jirani akabisha sufuria haiwezi kufa akaenda kushtak kwa sultan
kwenye baraza la sultan,abunuas alisema chochote kizaacho hufa,sufuria ilizaa sasa imekufa haoni sababu ya kushtakiwa!jirani alipoulizwa kama sufuria yake ilizaa akakubali ilizaa na mtoto aliletewa na abunuas
kesi ikaamuliwa kwa sheria ya kizaacho hufa,ikawa imekula kwa jiran!
 
Nakumbuka Abunuasi alipewa adhabu ya kutengeneza nyumba hewani (angani), basi kwa utalaam wake aktengeza kitu kama box akaweka na kengele. Baada ya hapo aliifunga kamba nyumba yake na kuirusha juu, ikiwa juu ile kengele ilikuwa inaendelea kugonga na Abunuas akamweleza Mfalme kuwa wale ni mafundi wako kazini, baada ya kengele kuishiwa nguvu na kuacha kugonga Abunuas akamwambia Mfalme awatume watu wawapelekee mafundi misumari kwani imewaishia.

Hapo tene nyumba ilishindikana kuisha baada ya mafundi kutopelekewa misumari.
 
Basi bwana,maskini mmoja alienda nyuma ya jiko la tajiri mmoja akiwa na ugali wake mkavu.kutokana na harufu nzuri iliyokuwa ikitoka jikoni,jamaa akawa anamega tonge,analielekezea kule inakotoka harufu,then anameza tonge.Basi tajiri alipomkuta,akampeleka mahakamani ili alipe harufu aliyokula.Mtetezi wa mtuhumiwa alikuwa abdul.Abdul akasema haina shaka tutamlipa hiyo harufu yake.Abdul alichukua sarafu,akawa anadondosha chini,sarafu ikitoa mlio,abdul anamuuliza tajiri,'umeisikia hiyo sauti?kama umeisikia,nimeshakulipa kwa mlio wa sarafu.Abdul aliendelea na mchezo huo mpaka pesa anayodai tajiri ikatimia lakini ndo hivyo,abdul alilipa harufu ya nyama kwa sauti za sarafu.
 
Huyu sasa alikuwa Abunuwasi...
 
Dah, hii ni kali!
 
Dah! Safi sana kwa hizi simulizi atleast tumeburudika na kupumzika na hekaheka za siasa hapa.
 
Kama vipi, ziwekwe hadithi za wahusika tofau kama vile Juha, Ali baba na wengineo. Maana Juha nae anafurahisha
 
Kama haitoshi vile,maskini alikopa pesa kwa bwana mmoja.Yule bwana mkopo alitoa ila alimpangia muda wa kulipa lile deni.Yule maskini aliambiwa kama hatalipa lile deni ndani ya ule muda,basi nyama kilo moja itakatwa toka mwilini mwake.Kutokana na dhiki yake,yule maskini alikubali yale masharti.Ule muda ulipita na yule maskini hakufanikiwa kulipa lile deni.Yule bwana tajiri akampeleka mahakamani kumshtaki ili apewe ruhusa ya kukata nyama kutoka kwa jamaa.Abdul hakuchelewa,akaenda mtetea yule maskini.Abdul akasema ndio,lazima mdaiwa akatwe hiyo kilo moja ya nyama kama walivyokubaliana,lakini hiyo nyama ikatwe kwa mkato mmoja tu,isizidi na wala isipungue kilo moja na pia ulisema utakata nyama tu,basi kata nyama tu ila damu usichukue,ukikosea tutakukata wewe.Kwa masharti haya,tajiri aligwaya na kujiweka pembeni kuepusha malumbano.
 
Basi bwana,maskini mmoja alienda nyuma ya jiko la tajiri mmoja akiwa na ugali wake mkavu.kutokana na harufu nzuri iliyokuwa ikitoka jikoni,jamaa akawa anamega tonge,analielekezea kule inakotoka harufu,then anameza tonge.Basi tajiri alipomkuta,akampeleka mahakamani ili alipe harufu aliyokula.Mtetezi wa mtuhumiwa alikuwa abdul.Abdul akasema haina shaka tutamlipa hiyo harufu yake.Abdul alichukua sarafu,akawa anadondosha chini,sarafu ikitoa mlio,abdul anamuuliza tajiri,'umeisikia hiyo sauti?kama umeisikia,nimeshakulipa kwa mlio wa sarafu.Abdul aliendelea na mchezo huo mpaka pesa anayodai tajiri ikatimia lakini ndo hivyo,abdul alilipa harufu ya nyama kwa sauti za sarafu.

Abunuwasi alikuwa mshairi maarufu katika mahakama ya khalifa Haruni Rashidi. Siku moja Khalifa alimteua Abunuwasi kuwa Kadhi mkuu wa jiji, Asubuhi moja mpishi wa keki akaenda kuonana na Kadhi na kulalamika kuhusu bwana mmoja masikini.

Mpishi analalamika
: 'huyu ombaomba anasimama tuu karibu ya kibanda changu pale sokoni ninapo oka keki zangu tamu. ananusa tuu harufu nzuri bila kunilipa, kwahiyo mimi ninakuwa nikifanya kazi bure.'

Abunuwasi kama Kadhi mwenye busara akalifikiria swala hili kwa muda kidogo, kisha akatoa hukumu: akamwambia mpishi...

''unachosema ni kweli kabisa. huyu ombaomba amefaidi harufu ya keki zako na kwa kufanya hivyo ametumia matunda ya kazi yako. Kwa hilo itabidi akulipe fidia. Nafikiri dinari mbili za dhahabu zitakuwa ni fidia inayofaa kabisa.''

Macho yampishi yakang'aa aliposikia dinari mbili, lakini masikini akalalamika:

"Mungu mkubwa, mimi ni masikini, sina pesa, hata ukinitingisha hutasikia mlio wa njuga. Unaweza ukakamua maji ya matunda kwenye zabibu lililo kauka?

Abunuwasi akalifikiria tena hili kwa muda alafu akasema:

ikiwa wewe ni masikini, nitakulipia hii fidia toka mfukoni kwangu.' Abunuwasi akatoa sarafu mbili, mpishi akanyoosha mkono wake wa kulia kwa shauku kubwa ili apokee fidia yake.
Mara moja Abunuwasi akabadilika na kuanza kumuhoji mpishi...!

Abunuwasi: Je huyu masikini alikula keki zako?

Mpishi: Hapana Mkuu

Abunuwasi: Je alizinyofoa?

Mpishi: Hapana Mkuu

Abunuwasi: Labda aliziharibu kwa kuzipumulia?

Mpishi: eeh, Hapana Mkuu

Abunuwasi: Kwa hiyo unaweza ukaziuza ama umeshaziuza?

Mpishi: Ndio Mkuu ninaweza nikaendelea kuziuza na zingine nimeshauza

Abunuwasi: Kwa hiyo basi kama huyu bwana hajala, hajanyofoa wala kuzipumulia keki zako, zaidi ya kuvuta harufu, nawe basi utafidiwa na sauti. fungua masikio yako kwa makini ili nawe ufurahie sauti za dinari mbili za dhahabu.

Ikabidi mpishi afanye hivyo kwa sababu hii ndio ilikuwa fidia pekee ambayo angeweza kupata.
 
Katika mwaka mmoja, Juha aliamua kuwa mfugaji mbuzi. Alinunua mbuzi na akanza kufuga na huku akiwa na tamaa ya kumuongezea kipato chake pindi tu mbuzi huyo atapoanza kuzaa watoto, naye atawafuga hadi wawe wengi na kuwa tajiri mji mzima kwa mbuzi wake hao.

Siku moja Juha akipokuwa anampeleka malishoni mbuzi wake njiani alikikuta kiatu kimoja kizuri sana kati kati ya njia. Alisimama na akakingalia na kilimpendeza na alisema "kiatu hiki ni kizuri lakini mbona kipo kimoja tu" alitafuta kiatu chengine pembezoni mwa ile njia hakukiona. Akaona hakina maana kukichukua kwani hawezi kuvaa kiatu kimoja.

Juha akachukuwa mbuzi wake na akakiwacha kile kiatu pale pale. Aliposonga mbele kidogo akakikuta kiatu chengine kama kile ambacho kilikuwa ni cha mguu mwengine wa kile cha mwanzo. Juha alishangaa na akaona bora angelikichukua kile cha mwanzo na kwa sasa vingelikuwa tayari vishatimia pea moja. Ndipo alipoamua kumfunga mbuzi wake pembeni ya njia na akakiweka kiatu kile pale pale alipomfunga mbuzi ili arudi akakichukuwe kiatu kile cha mwanzo.

Aliporudi pale kilipokuwepo kiatu cha mwanzo hakukikuta tena kiatu kile, alijaribu kukitafuta lakini hakukiona. Basi akaona kuwa ametokea mtu amekiokota. Akarudi haraka alipomfunga mbuzi wake. Nako pia hakumkuta mbuzi wala kile kiatu kimoja. Ikawa amemkosa mbuzi na pia viatu hakuvikuta, Juha ndoto zake zote za utajiri ziliruka na akabaki na umasikini wake kwa ubaya wa tamaa zake.
 
safi sana mkuu! Mi namfananisha juha na viongoz waböngo ma MBUMBUMBU design ya waziri mkuu ktk hadithi ya abunuas!
 
safi sana mkuu! Mi namfananisha juha na viongoz waböngo ma MBUMBUMBU design ya waziri mkuu ktk hadithi ya abunuas! Big up sana!
 
Back
Top Bottom