Bungeni: Wabunge wapingana juu ya Hoja Binafsi ya Mhe. Mbatia, wengine wamfuata nje ya ukumbi!

Aisee, kumbe lengo la CCM ni kuhakikisha elimu duni inaendelea kutolewa nchini ili vijana wetu wasiwe na uwezo wa kuhoji madudu ya serikali, lol

Ndio maana waziri wa elimu alisema Tanzania ni muungano wa Zimbabwe na ___!
Aibu

hivi sisi watanzania ni nani aliyetuloga mungu tuokoe....
 
Kumbe mnatazama bunge lenye kula sahani moja na serikali ah ah ili si bunge la wananchi wandugu ni bunge la chama cha majambazi ccm upuunzi mtu watoto hata sisi tumelishwa sumu long time will see
 
haya ndio mambo ya kutuingiza barabarani.nasubiri maandamano maana tuliandamana kwa ishu za watoto mbagala,tukaweka mgomo wa kutokula nyama Mwanza,mambo ya ajabu ajabu tu!sasa hili la kitaifa,watoto wetu wanateketea kwa kunyimwa elimu nzuri ili huko mbele waje kuwa watumwa wa wenzao wanaosomeshwa ulaya huko..je,tulikalie kimya hili?nasema hivi..NASUBIRI MAANDAMANO!

uko smart sana mkuu!
 
Mhe. Mbatia anasema amefuatilia suala la mitaala mpaka wizarani "amenyimwa nakala." Ukisema umenyimwa nakala ina maana wanayo, lakini anaongeza kusema waziri amedanganya bunge, mitaala haipo, sasa sijui amenyimwa vipi wakati anasema haipo.

Tundu Lissu nae anasema alichokuwa amekishikilia waziri wakati anaonyesha kwamba mitaala anayo mikononi sio mitaala ni rasimu ya 2005. Tundu Lissu na wenzie wamejuaje makaratasi aliyokuwa ameshika waziri ni kitu gani? Hatuelezwi.

Lakini kingine, wengi, kama sio wote hapa, tumepita katika mfumo huu wa elimu Tanzania. Ninachofahamu mimi kwa sisi shuleni tulikuwa hatuna walimu, tulikuwa tunajisomea wenyewe (shule zenye walimu nakumbuka zilikuwa Mzizima, Jitegemee, Shaaban Robert, Saint Anthony) kwa hiyo kitabu cha kwanza kabisa ambacho tulikuwa tunakitafuta sio cha Historia wala cha Physics, bali ilikuwa ni kitabu cha mtaala, na vilikuwepo, kutoka Wizara ya Elimu. Sasa sielewi wanaposema mitaala hakuna toka 1961, mitaala gani hiyo wanayoiongelea?
 
Mtaala ulibinafsishwa kwa mr Nyambari Nyangwine, ndio maana hata sisi walimu tunatumia vitabu vyake pekee kufundishia, na Kama mnavyoona, kupitia vitabu hivi kuna shule "zinafaulisha" darasa zima na wengi wao sasa hivi wapo "vyuo vyetu vikuu vya Tanzania"
 
Hivi watoto wa Ndugai wanasoma wapi? I have nothing person with please, maana naona inataka ujasiri usio wa kawaida kutumia cheo chake kuhakikisha watoto wetu hawapati elimu inayoendana na kasi ya mabadiliko duniani!
dhurma wafanyayo haitawasaidia kitu kwa jamii watachukiwa kwa Mungu na Wanadamu
 
Hakuna wizara aliyopitia kuingoza ikawa salama jamaa(kawambwa) sijui anaogopwa kwa lipi,na tusipoangalia kwa wizara nyeti ya elimu kuongozwa na watu wasio na nia njema na vizazi vyetu tutaelekea shimo la vilaza,hoja ya mbatia isiishie njian kawambwa resign
 
Wenzetu wana elimu ya magunduzi sie tuna elimu ya kusoma magunduzi yao Mbavu Pu
 
Tumejenga majengo yanayoitwa shule lakini si shule kwa maana ya shule. CCM wanalijua hilo ndiyo maana watoto wa viongozi wanasoma nje ya nchi.
 
tatizo la ccm ni chama cha kishikaji na serikali ya washikaji, upuuzi kama huo wa Kawambwa haujaanza leo toka Kapuya na sera zake mbovu za kuondoa somo la biashara secondary na kuunganisha masomo eti Physics na chemistry liwe somo moja. how cms?au ndio akili za Madokta zilivyo? Suluhisho ni kuipiga chini ccm tu!
 
Wanaonishangaza na kunisikitisha sana ni wale wanaopost kwenye thread hii wakiunga mkono tabia za spika na naibu wake kuliburuza bunge!! Mbunge ni mwakilishi wa jamii kubwa na sioni kwanini apuuzwe na mtu mmoja tu. Tuna safari ndefu kujua DEMOKRASIA.
 
curriculum mzazi akiiona haitomsaidia kitu. hata syllabus haina manufaa kwa mzazi. tuache kupapatikia mambo. watu ambao wanauwezo wa kuchanganua curriculum ni watu wenye fani ya curriculum development. kuna watu wana phd katika fani hii.

Acha -----. Huwezi kusema syllabus haina manufaa kwa mzazi. Eti haitomsaidia kitu.

Nani ina mfaa sasa? Walimu? Wabunge? Mawazir? Raisi?

Eti watu wenye uwezo kuchanganua --curriculum ni watu wenye fani-curriculum development? What is so special kwenye-curriculum sisi wengine tushindwe kuelekezwa kuichanganua na kuielewa?
 
Waziri wa elimu ni lazima aachie ngazi. Wananchi tuingie mitaani kuwaunga mkono wabunge wetu wa vyama vya upinzani katika hili jambo.
 
Ninamshukuru Mbatia inagawaje watoto wake wanasoma nje ya nchi lakini bado anatupigania sisi...
 
Niliwahi kumsikia mwanamama mmoja ITV akisema kuwa Tanzania haina mtaala, binfisi ili jambo lilinishangaza. Kwamba inakuwaje baada ya miaka 50 ya uhuru nchi inaendeshwa kihuni, kama gari lisilo na taa. Jana Mbatia alipohoji kuhusu mtaala uko wapi, nikaona jinsi spika anavyo angaika kuzima hilo swali nikaamini kweli hii nchi ni gari lisilo na taa, kwa maana muda wowote linaweza pamia mabonde. Watanzania tujiulize, hivi kweli serikali ya CCM iko serious?, bado kweli wanaheshima ya kutawala nchi hii?. Ifuatayo ni nukuu kutoka gazeti la mwananchi

“Tumewaita kuzungumzia sababu za kutoka nje na hatua za kuchukua. Kama mlivyosikia, Mbatia alisema kuwa hakuna mitaala wala hakujawahi kuwa na mitalaa tangu mwaka 1961 na kama ipo atajiuzulu. Alipomtaka Waziri ampe japo nakala, waziri alikataa,”
 
huyo lukuvi nae hajasoma kazi yake kutetea ujinga tuu hapo bungeni. kwa vile watoto wao wanasoma shule nje ya nchi wanaona haina maana

Tatizo la hawa viongozi co kutokusoma tu coz wapo waliosoma lakini wapo kimya tu..Tatizo kubwa ni kwamba hawana uzalendo kabisa na nchi yetu..what they care is just their abdomen....But one day GOD will answer our prayers..yes am sure of this..
 
Hali ya hewa inaelekea kuchafuka bungeni. Ni wazi kawambwa kadanganya na inaonekana mtaala haupo
Kawamba==FastJet==Vasco Dagama======?????????????????????????????????????????
Malizia wenyewe,ole wenu 2015 mchague wauza sura mtakiona cha moto.
 
Acha -----. Huwezi kusema syllabus haina manufaa kwa mzazi. Eti haitomsaidia kitu.

Nani ina mfaa sasa? Walimu? Wabunge? Mawazir? Raisi?

Eti watu wenye uwezo kuchanganua --curriculum ni watu wenye fani-curriculum development? What is so special kwenye-curriculum sisi wengine tushindwe kuelekezwa kuichanganua na kuielewa?

mitaala (curriculum) haina manufaa kwa mwalimu. kilicho muhimu kwa mwalimu ni muhtasari wa somo husika (syllabus). huyo mzazi ndiyo usimtaje kabisa. mtaala akaufanyie nini!? muhtasari akaufanyie nini!? tuache ushabiki wa kisiasa. penye ukweli usemwe. watu wanashindwa kutofautisha kati ya sera ya elimu (education policy), mitaala (curriculum) na mihutasari (syllabuses). hapa mzazi hana chake. hou ndiyo ukweli. cha mzazi ni kitabu cha somo (subject book) na daftari la mwanae, basi.

mimi kama mwalimu, zana kubwa inayonisaidia ni muhtasari (syllabus) ambao lazima niutumie kuandaa skimu (scheme of work) ya mwaka mzima. skimu hunisaidia kuandaa log book ya mwezi. log book hunisaidia kuandaa daily lesson plan. lesson plan hunisaidia kuandaa notes. sihitaji mtaala hata chembe.

syllabus books zipo tele pale taasisi ya elimu na katika maduka ya vitabu nchini kote zinauzwa. mtaala auziwe nani? ndugu yangu nchi hii ina sera ya elimu ya mwaka 1995, ina mitaala, ina mihutasari na vitabu. nakiri kuna mapungufu ya hapa na pale lkn elimu inayotolewa hapa tanzania ni nzuri sana. hatuna zana za kufundishia hilo ndiyo tatizo kubwa. hatuna maabara za kutosha! hata hivyo elimu ni nzuri.

mbatia hakujiandaa vizuri. suala la elimu linahitaji utafiti wa kina na uwezo mkubwa kielimu. kama mbatia bungeni alisema kuwa kuandika juu ya syllabus book kuwa "Advanced Mathematics Syllabus for Advanced Level" ni kosa, utasema ni msomi huyo!? ana shahada ya chuo kikuu lkn alisisitiza kuwa kurudia neno advanced mara mbili ni kosa. haelewi kuwa kuna branch ya mathematics inaitwa advanced mathematics.

namalizia kwa kusema kuwa tuache ushabiki wa kisiasa kwenye mambo ya msingi. mbatia mwenyewe huo mtaala hawezi kuuelewa vizuri.
 
Niliwahi kumsikia mwanamama mmoja ITV akisema kuwa Tanzania haina mtaala, binfisi ili jambo lilinishangaza. Kwamba inakuwaje baada ya miaka 50 ya uhuru nchi inaendeshwa kihuni, kama gari lisilo na taa. Jana Mbatia alipohoji kuhusu mtaala uko wapi, nikaona jinsi spika anavyo angaika kuzima hilo swali nikaamini kweli hii nchi ni gari lisilo na taa, kwa maana muda wowote linaweza pamia mabonde. Watanzania tujiulize, hivi kweli serikali ya CCM iko serious?, bado kweli wanaheshima ya kutawala nchi hii?. Ifuatayo ni nukuu kutoka gazeti la mwananchi

"Tumewaita kuzungumzia sababu za kutoka nje na hatua za kuchukua. Kama mlivyosikia, Mbatia alisema kuwa hakuna mitaala wala hakujawahi kuwa na mitalaa tangu mwaka 1961 na kama ipo atajiuzulu. Alipomtaka Waziri ampe japo nakala, waziri alikataa,"

naamini mitaala ipo. ipo kwenye mafaili na katika mtindo wa pamphlet. haijachapwa na kusambazwa kwa sababu haina umuhimu kwa wananchi na hata kwa walimu

mitaala (curriculum) haina manufaa kwa mwalimu. kilicho muhimu kwa mwalimu ni muhtasari wa somo husika (syllabus). huyo mzazi ndiyo usimtaje kabisa. mtaala akaufanyie nini!? muhtasari akaufanyie nini!? tuache ushabiki wa kisiasa. penye ukweli usemwe. watu wanashindwa kutofautisha kati ya sera ya elimu (education policy), mitaala (curriculum) na mihutasari (syllabuses). hapa mzazi hana chake. hou ndiyo ukweli. cha mzazi ni kitabu cha somo (subject book) na daftari la mwanae, basi.

mimi kama mwalimu, zana kubwa inayonisaidia ni muhtasari (syllabus) ambao lazima niutumie kuandaa skimu (scheme of work) ya mwaka mzima. skimu hunisaidia kuandaa log book ya mwezi. log book hunisaidia kuandaa daily lesson plan. lesson plan hunisaidia kuandaa notes. sihitaji mtaala hata chembe.

syllabus books zipo tele pale taasisi ya elimu na katika maduka ya vitabu nchini kote zinauzwa. mtaala auziwe nani? ndugu yangu nchi hii ina sera ya elimu ya mwaka 1995, ina mitaala, ina mihutasari na vitabu. nakiri kuna mapungufu ya hapa na pale lkn elimu inayotolewa hapa tanzania ni nzuri sana. hatuna zana za kufundishia hilo ndiyo tatizo kubwa. hatuna maabara za kutosha! hata hivyo elimu ni nzuri.

mbatia hakujiandaa vizuri. suala la elimu linahitaji utafiti wa kina na uwezo mkubwa kielimu. kama mbatia bungeni alisema kuwa kuandika juu ya syllabus book kuwa "Advanced Mathematics Syllabus for Advanced Level" ni kosa, utasema ni msomi huyo!? ana shahada ya chuo kikuu lkn alisisitiza kuwa kurudia neno advanced mara mbili ni kosa. haelewi kuwa kuna branch ya mathematics inaitwa advanced mathematics.

namalizia kwa kusema kuwa tuache ushabiki wa kisiasa kwenye mambo ya msingi. mbatia mwenyewe huo mtaala hawezi kuuelewa vizuri.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom