Bungeni: Wabunge wapingana juu ya Hoja Binafsi ya Mhe. Mbatia, wengine wamfuata nje ya ukumbi!

ujinga unaoendekezwa na CCM haupaswi kuendekezwa ikiwezekana tuandamane ili kupinga ujinga huu

haya ndio mambo ya kutuingiza barabarani.nasubiri maandamano maana tuliandamana kwa ishu za watoto mbagala,tukaweka mgomo wa kutokula nyama Mwanza,mambo ya ajabu ajabu tu!sasa hili la kitaifa,watoto wetu wanateketea kwa kunyimwa elimu nzuri ili huko mbele waje kuwa watumwa wa wenzao wanaosomeshwa ulaya huko..je,tulikalie kimya hili?nasema hivi..NASUBIRI MAANDAMANO!
 
Hata kama hiyo mitaala ingepatiakana bado tuna changamoto nyingi zinazokabili namna ya kuitumia mitaala hiyo kuanzia

walimu,wanafunzi,vifaa vya kufundishia vikiwemo vitabu,madaftari,karamu,vifaa vya alama kwa ajili ya walemavu,nyumba za

walimu,madarasa,maabara,vyoo kwa wanafunzi,viwanja vya michezo n.k

Kwa mtazamo wangu ningefikiri labda wabunge wagejikita zaidi katika."Elimu ina gharama kubwa kwa sasa,nini kifanyike kupunguza

gharama za elimu kama walivyofanya TCRA na ikiwezekana shule zote za binafsi ama ziingie ubia na serikali au kushusha gharama za ada"
 
Hawa
wapuuz
i walishaamua kujenga taifa la
wapuuzi kwa kutumia
upuuzi wakiandaa upuuzi
katika kuleata elimu ya kipuuzi ili baadaye tuwe

wapuuzi
wengi na tuongozane
wapuuzi tu. Wanataka
upuuzi wao wa
kipuuzi ujenge Tanzania ya

kipuuzi....

Kila mahali ni upuuzi upuuzi.
 
Nchi ya ajabu sana hii!
Waziri Kawambwa kagoma kuwasilisha nakala ya mitaala kwa Spika, lakini anadai atawasilisha nakala 300 bungeni tarehe 6!
Si kwamba wana mpango wa kuchakachua hizo nakala mpya zitakazochapwa?
 
Nashukuru wenyewe sasa mmeona. wakifeli watoto wa kubebeshwa lawama ni mwalimu. Kumbe serikali imeandaa sumu kwa watoto. Halafu jitu na akili zake linakaa kusifu sumu ambazo hata mtoto wake atakuja kuzipata tu. Damn them.
 
Serikali imegoma kuonyesha Mitaala ya Elimu hapa nchini, mitaala hiyo iliombwa tangu bunge lililopita na serikali iliahidi kuileta bungeni lakini baada ya Mh. James Mbatia kuombwa ahitimishe hoja yake binafsi. Mbatia alikumbushia ahadi hiyo na kuiomba serikali kuigawa mitaala hiyo kwa wabunge.

Kilichotokea ni Naibu Spika Job Ndugai kuanza kuikingia kifua serikali na kujaribu kumlaghai Mbatia ahitimishe hoja yake alafu yeye Ndugai atafakari kama inafaa ataitaarifu serikali kuileta mitaala hiyo bungeni.

Kilichoshagaza zaidi Mbatia alipoambiwa ahitimishe hoja yake; aliomba mwongozo wa Spika lakini ghafla Naibu Spika alimgeuka na kumwabia muda wanaoutumia kuombea miongozo ndio muda wake wa kuhitimisha hoja.

Lakini Mbatia aligoma na kulieleza bunge kuwa jana alimwandikia Waziri wa Elimu kuwa anaiomba Mitaala hiyo lakini hakupata jibu, alishakwenda Wizara ya Elimu kuomba mitaala hiyo lakini hakupewa na kuhoji kama mbunge anadanganywa kiasi hiki itakuwaje kwa mtanzania wa kawaida?

Kinachotia moyo ni pale wabunge wa CHADEMA walipoungana na wa NCCR Mageuzi katika kuibana serikali na kuomba miongozo mbalimbali lakini Ndugai alijaribu kuwakwepa na kujigamba kuwa yeye ndiye mwenye maamuzu ya kuiomba serikali au la.

Baada ya Ndugai kuona serikali imebanwa akaamua huhitimisha hoja kibabe na kuanza kusikilizwa kwa hoja ya Hamisi Kigwangalla

Ndipo hapo wabunge wa upinzani walipoamua kutoka nje ya ukumbi wa bunge!

swali ni je? Nini kifanyike wakati watoto wetu wanaendelea kulishwa sumu?.

Ndugai kwa kweli unalilidhalilisha taifa na bunge ,.... heshima ya bunge inazidi kushuka... na si kwamba unakilinda CCM bali unazidi kuchochea upinzani kuimarika zaidi.............
 
Kwa mara ya kwanza Leo nimefurahishwa nakuridhishwa na maamuzi ya wabunge kutoka vyama pinzani kutokana na sababu kuu mbili 1.maamuzi ya mh.NGUGAI yalikuwa yakibabe na kejeli sidhani kama mtuu yoyote mwenye akili ungeweza kuendelea kukaa kwenye kikao kama kile hata kama anaeongea ni boss wako. 2.hoja iliyokua mezani ni ya msingi na haikutolewa na mtu WA CDM .angetoka CDM ingesemwa kua ni Fujo na mtoaji hoja alikua mstaarabu na maombi yake hayakua kutaka kujiuzulu kwa spika au waziri..pongezi kwa MBATIA
 
me nashangaa sana coz kuna baadhi ya watu wamelaumu sana wabunge kuchomewa mali zao kule mtwara. ila sasa uhasidi wao nadhani mumeuona. i wish jengo la bunge lingejengwa masasi, mtwara sasa lingebakia maji.u tu
 
mbona unanitia kinyaa! jibu hoja la sivyo kaa kimya. fanya hivi we mtoto. acha nikupeleka shule. quote utumbo niliyouandika kisha unielimishe kuwa usahihi wa jambo hili ni huu. hapo nitakuona una akili na ni msomi. najua umri ndiyo unakusumbua. ukikua upeo wako wa kuelewa tunayo yaandika utaongezeka. kwa sasa naamini huwezi kujibu. subiri ukue kwanza

Nimekuambia endelea ku- scramble
 
Ubabe wa Ndugai waunganisha wapinzani

KWA mara ya kwanza tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa 2010, wabunge wa vyama vya upinzani jana waliungana pamoja na kumsusia Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai, wakipinga hatua yake ya kupindisha hoja binafsi ya Mbunge wa kuteuliwa na Rais, James Mbatia (NCCR-Mageuzi) na kuitetea serikali bila maelezo yanayoeleweka.

Kwa pamoja, wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), National Convention for Construction and Reform (NCCR- Mageuzi), United Democratic Party (UDP) na Chama cha Wananchi (CUF) walitoka nje ya ukumbi wa Bunge wakaenda ukumbi wa kambi ya upinzani kufanya kikao cha dharura juu ya hatua za kuchukua dhidi ya ubabe wa Ndugai.

Hatua kama hiyo ya kutoka nje ya ukumbi wa Bunge, imekuwa ikitumiwa na wabunge wa CHADEMA ambayo inaunda kambi rasmi ya upinzani bungeni kupinga baadhi ya masuala kadhaa. Hata hivyo, kwa mara mbili tofauti CHADEMA waliposusia Bunge, wenzao wa vyama vingine hawakuwaunga mkono, hatua iliyotafsiriwa kama kutokuwapo kwa mshikamano.

Kwa mara ya kwanza, CHADEMA walisusia hotuba ya Rais Jakaya Kikwete ya kufungua Bunge, wakipinga matokeo ya uchaguzi mkuu uliyomleta madarakani na mara ya pili walitoka nje ya ukumbi wakipinga kupitishwa kwa sheria ya mabadiliko ya katiba mpya. Hali hiyo ni tofauti na jana ambapo wabunge wa vyama hivyo vya CHADEMA, CUF, UDP, TLP na NCCR-Mageuzi waliungana kwa kutoka nje ya ukumbi wa Bunge, kupinga hatua ya Ndugai kuwaburuza katika kupitisha hoja ya Mbatia.

Hoja hiyo binafsi iliyoainisha udhaifu katika mfumo wa elimu nchini, iliwasilishwa juzi na kuibua mjadala mzito bungeni, huku kambi ya upinzani ikikubali hoja ya Mbatia kutaka kuunda kamati teule wakati wabunge wa CCM wakipinga. Mzozo wa jana ulianza baada ya Mbatia kufunga hoja yake na kutaka Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa ampe nakala ya mitaala ya elimu aliyoionesha bungeni kwamba anayo.

Mbatia alitaka kupata nakala hiyo ya mitaala akidai Tanzania haijawahi kuwa na mitaala ya elimu tangu mwaka 1961, huku Waziri Kawambwa akidai anayo. Baada ya Kawambwa kushindwa kukabidhi nakala ya mitaala hiyo kwa Mbatia, mbunge huyo aliacha kuendelea kufunga hoja yake, akasema waziri amelidanganya Bunge. Tangu Bunge lililopita serikali ilikuwa imeombwa, na nayo ikaahidi kuleta mitaala hiyo bungeni. Mbatia alishauri serikali iwagawie wabunge nakala ya mitaala hiyo.

Kwa sababu anazojua mwenyewe, Ndugai, badala ya kuitaka serikali itekeleze ahadi yake, akaitetea kijanja, akimtaka Mbatia ahitimishe hoja yake kwanza, kwa madai kuwa mwenyewe angetafuta namna ya kuieleza serikali ilete mitaala hiyo baadaye.
Ndipo Mbatia alipoomba mwongozo wa spika, na Ndugai akagoma kuruhusu mwongozo utolewe, huku akimsuta mbunge huyo, kama vile anamlazimisha, kwamba muda huo anaotumia kuomba mwongozo ndio muda wake kuhitimisha hoja yake binafsi.

Mbatia akasema haikuwa mara yake ya kwanza kuomba mitaala hiyo, kwani hata jana yake alikuwa amemwandikia waziri wa elimu kuomba mitaala hiyo; na kwamba alishafika hata wizarani akanyimwa nakala ya mitaala. Akahoji iweje mbunge adanganywe hivyo, tena katika suala nyeti kama hili? Wakati Mbatia akiendelea kushikilia msimamo wake, wabunge kadhaa wa CHADEMA na NCCR-Mageuzi nao wakaingilia kati kuomba mwongozo wa spika, lakini Ndugai akawagomea, akisema yeye ndiye mwenye uamuzi wa mwisho kuomba nakala ya mitaala serikalini.

Baada ya kibano cha wapinzani, Ndugai akatumia ubabe kuhitimisha hoja ya Mbatia, akamwita Mbunge wa Nzega, Hamis Kigwangalla awasilishe hoja yake. Kutokana na ubabe huo, wabunge wote wa upinzani wakatoka nje ya ukumbi wa Bunge na kufanya mkutano na waandishi wa habari. Wakizungumza katika mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa Pius Msekwa, kambi hiyo ya upinzani ilimtaka Waziri Kawambwa kujiuzulu kwa sababu amelidanganya Bunge kwamba anayo mitaala ya elimu wakati hana.

Mbali ya hayo, walimwomba Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kukagua hesabu za Wizara ya Elimu hususani katika miradi ya uchapishaji vitabu. Pia walisema watatumia kanuni ya 14 ya Bunge kuandaa hoja ya kuwaondoa madarakani, Spika Anne Makinda na Naibu wake, Ndugai kwa sababu wameshindwa kuendesha Bunge hilo kwa haki bila upendeleo. Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu (CHADEMA), alisema katika Bunge lililopita Dk. Kawambwa aliahidi kuleta hadharani mitaala ya elimu ya shule za msingi na sekondari, lakini hakufanya hivyo.

Alisema kwa mara ya pili jana, wakati akijibu hoja za Mbunge wa kuteuliwa, Mbatia aliahidi kuileta, lakini hakufanya hivyo. "Kama mnakumbuka, jana mheshimiwa Mbatia alisema yuko tayari kujiuzulu kama waziri angeweza kuleta hiyo mitaala, lakini waziri alizidi kusisitiza kwamba mitaala ipo wakati si kweli, pia kibaya zaidi waziri alisimama na kuonyesha kwamba alikuwa na mitaala hiyo mkononi kumbe kile alichokuwa akikionyesha ni muhtasari na si mtaala.

"Hii ina maana kwamba, alichokionyesha waziri hiyo si mitaala bali rasimu ya mwaka 2005, kwa maana hiyo ni wazi Waziri Kawambwa amelidanganya Bunge," alisema. Lissu alisema wapinzani kuanzia sasa wanaanza kuandaa taarifa kwa mujibu wa kanuni za Bunge hilo kumtaka Waziri Kawambwa kujiuzulu na asipofanya hivyo, wataiomba mamlaka ya uteuzi imfukuze kazi. Aliongeza kuwa yasipofanyika hayo yote, watapeleka hoja bungeni ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

Aidha, katika mkutano huo, wapinzani hao walidai kuwa Spika Makinda pamoja na naibu wake, Ndugai wanaongoza Bunge hilo kibabe na kuwazuia wabunge kuisimamia serikali sawasawa.

"Spika na naibu wake, wamefanya kila jitihada kuikinga serikali na kulizuia Bunge kuisimamia na kuiwajibisha serikali kuhusu uchafu huu wa mitaala kwa shule zetu. "Sisi wabunge wa upinzani pia tumeazimia kuandaa hoja bungeni ya kuwaondoa Spika wa Bunge na naibu wake madarakani," alisema Lissu.

Aidha, Lissu alisema watatumia fursa zilizopo ili kuhakikisha mjadala wa mitaala kwa shule za Tanzania unapata nafasi ya kujadiliwa na Bunge kwa uwazi na kwa haki. Naye Mbatia alisema ameshangazwa na hoja yake kutoungwa mkono na wabunge wa CCM kwa sababu Tanzania haijawahi kuwa na mitaala tangu mwaka 1961.

"Naibu Spika alipata kigugumizi gani kunipa hiyo mitaala ili niweze kujiridhisha na pengine kuondoa hoja yangu ili kuweka sawa hansadi za Bunge? "Nasema suala hili hatutaliacha hadi watueleze fedha zilizotolewa na taasisi za kigeni kugharamia vitabu vya watoto wetu zilifanya kazi ipi, wanafichaficha ili pia watumie fedha (chenji) za rada kutengeneza tena uchafu huo wa vitabu," alisema Mbatia.

Chanzo: Tanzania daima
 
Wabunge walitakiwa kuchukua hatu hii siku nyingi tu.Ila ni bora wachukue hatua sasa kuliko kuendelea kukaa kimya na kulalamika tu.
 
...dah!...hii sasa kali mimi nilidhani wanaficha mikataba tu kumbe hadi mitaala?...kama hata mitaala inafichwa je nikipi sasa kitakuwa wazi kwa wananchi?...
 
hapa naona Mbatia alikuwa amemshika pabaya waziri na ndo maana naibu spika imejitoa mhanga kumuokoa waziri. ila huu ushirikiano wa upinzani sina imani nao. siutofautishi na urafiki wa mashaka.
 
ccm wameonyesha kila dalili ya kuondoka madarakani 2015,tunachosubiri ni muda wa kupiga kura ufike watuachie nchi yetu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom