Bungeni: Mjadala wa dharura juu ya mgomo wa wauza mafuta

Wabunge wanajadili hali ya dharura bungeni! Hoja imetolewa na Mh January Makamba! Ameanza kuchangia hoja atafuata Zitto na wabunge wengine
 
naibu spika amerudi kutoka kwenye kikao cha dharura kutokana na hoja ya dharura aliyoitoa january makamba mbunge wa bumbuli,ameanza january kuwasilisha hoja yake akifuatiwa na zitto kabwe,
 
Mkamba anasema mtaani kumekuwa balaa mafuta sasa hakuna na pale yalipo yanauzwa hadi sh 4,000/ umeme hakuna watuwanajitutumua kutumia jenereta na bado mafuta sasa hakuna.

Siku ya 7 sasa hakuna tamko lolote lilitolewa kana kwamba nchi haina viongozi hivyo anaomba tamko la serikali na utekelezaji.

Pia amegusia serikali kushindwa kusimamimia sheria wanazotunga wabunge
.
 
Nimemsikia Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini akiomba mwongozo wa Spika, kwa kutumia kanuni ya 45 ya Kanuni za Bunge, kuhusiana na kadhia ya mafuta ambayo imesababishwa na wamiliki wa vituo na makampuni ya mafuta. Matokeo ya ombi hili la Makamba ni Kamati kukutana na Naibu Spika kwenye kikao cha ghafla ambacho nadhani bado kinaendelea (maana hapa nilipo wenye umeme wao wameshachukua).

Tunasubiri kusikia kitakachoibuliwa baada ya mkutano huu wa dharura.
 
hii list ya watu wanaotaka kuchangia.....sijui kama watatoka na muafaka wowote.....makamba january kamwambia waziri mkuu na waziri wa nishati walau waseme neno/tamko///but what can they actually say?
 
Zito asema serikali haipaswi kuwa na maneno matamu dhidi ya wanaopindisha sheria
 
Ina maana kile kikao cha kamati kuu ya NEC kilichoanzisha zogo lote hili hakikutosha?

Hivi hii hoja ya kugeuza bunge kukaa kama kamati ya dharua ingetolewa na upinzani hasa CHADEMA Ndugai angekubali?
 
Ingekuwa ni wanafunzi wamegoma kuingia darasani basi wangevurumishiwa mabomu ya machozi, risasi za moto na maji ya kuwasha.....lakini muuza mafuta ANAIPA SERIKALI 24hrs na "serikali" inachekacheka tuuuu...

Mkuu, hapo penye rangi ni kweli TUMETHUBUTU,TUMEWEZA NA TUNARUDI NYUMA!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Poor Ngeleja, the guy doesnt deserve this post
Zitto anaua kabisa, EURA lazima iagize mafuta yawe released soon leo hii
 
Hongera zitto bungeni kwa kutoa maamuzi magumu juu ya kadhia ya mafuta wapatao wananchi
 
Mh. Mbunge Zitto kabwe aongea kwa uchungu sana kwamba wafanyabiashara wauze mafuta na anaekataa anyang'anywe leseni mara moja
 
Poor Ngeleja, the guy doesnt deserve this post
Zitto anaua kabisa, EURA lazima iagize mafuta yawe released soon leo hii
Hivi huyu Ngeleja alizaliwa awe waziri, kwa nini asiachie ngazi kuliko kuendelea na uwaziri ambao unamfanya achukiwe hata na watoto? Umeme ukikatika unasikia watoto wanasema Ngeleja huyo anatugaia giza
 
dah! Ngereja hali ni mbaya.......mgao wa umeme bado na hili la mafuta tena
 
Back
Top Bottom