Naanto Mushi
JF-Expert Member
- Oct 16, 2015
- 6,236
- 15,605
Nimeshtushwa na hatua za waziri Makamba na Ewura kukurupuka kwa kuongeza bei ya mafuta kwa kisingizio cha eti, ‘kuna uhaba wa dola nchini’. Nauita ni uamuzi wa kukurupuka kwasababu yeye Makamba na Ewura hawana mamlaka ya kisheria kuzungumzia uhaba wa dola kwenye uchumi, hiyo ni kazi ya benki kuu ya Tanzania.
Na mpaka sasa ninashangaa ni kwanini benki kuu wapo usingizini kuhusiana na hichi kitu na hawajatoa tamko lolote. Haiwezakani mtu tu unaamka huko kukurukukuru unaongeza bei kwa asilimia Zaidi ya 16, kwa kisingizio cha sababu ambazo huna utaalamu nazo. Ewura na Wizara ya Nishati na mambo ya uhaba wa dola, wapi na wapi jamani?
Nimemulika hili suala bila mihemuko, na nimejiridhisha kwamba kuna makosa makubwa na ubatili kwenye hili tamko la Makamba na Ewura, na nina hoja zifuatazo.
1. Huko duniani, mafuta bado yapo kwenye bei ya chini ikilinganishwa na bei ya mwaka mmoja uliopita.
Maana yake ni kwamba, hakuna any justification ya kuongezeka kwa bei ya mafuta kilichotokea huko duniani. Hivo inamaanisha, yale makampuni ya kuagiza mafuta hapa Tanzania bado wana agiza mafuta kwa bei ile ile ya awali kabla ya hili ongezeko la kukurupuka kwenye bei ya kuuzia sokoni. Maana yake ni kwamba, hii kupandisha bei kiholela itakuwa imewaongezea wauzaji na waagizaji wa mafuta faida ya Zaidi ya asilimia 16 kwasababu technically, cost of sales bado ni ile ile iliyokuwepo kwa kipindi cha miezi sita iliyopita.
Kwa mantiki hiyo, Ewura na Waziri Makamba, wanatuthibitishia vipi kwamba hakuna msukumo kutoka kwa wafanyabiashara wa mafuta wa Tanzania ili kupandisha bei ya mafuta kwa lengo la kutengeneza faida ya haraka?
2. Gharama za kuagiza mafuta kwa mwezi Tanzania ni pungufu ya asilimia 17 ya gharama za kuagiza bidhaa zote zinazotoka nje ya nchi (Imports), kwanini Makamba na Ewura wanadhani hiyo ndo njia sahihi ya kupambana na kukosekana kwa dola?
Kwasababu, haiingii akilini unaongeza bei ya kitu ambacho kinagharimu chini ya asilimia 17 ya gharama zote za kuagiza bidhaa nje ya nchi halafu zile imports nyingine zinazogharimu Zaidi ya asilimia 85 umeona kwamba hazichangii kwenye kuadimika kwa dola? Hiki kwangu pia ni kihoja.
Na hata ukiangalia hizo takwimu, unaweza kuona trend inaenda ikiboreka, maana yake situation ilikuwa worse kwa mwaka jana kuliko hata kwa wakati huu.
Lakini issue nyingine, ukiangalia volume ya mafuta inayoagizwa Tanzania kwa kipindi hiki ni ndogo kuliko hata ilivokuwa kwa mwaka jana, maana yake ni kwamba fedha za kigeni zinazotumia kununua mafuta nje ya nchi sio kwa kiasi kikubwa kama ilivokuwa mwaka jana.
So, hiyo inaamisha kwamba, kuongeza bei ya mafuta kwa gia ya kupunguza dola outflow haina mashiko kwa sababu so far, kiwango cha dola kinachonunua mafuta ni kidogo (less tha 17% of all imports) halafu pia, kiwango cha mafuta kinachoagizwa na nchi ni pungufu kuliko ilivokuwa mwaka jana.
Kwa hoja hizo hapo, ni wazi kabisa kwamba uamuzi wa Makamba na Ewura ni uamuzi wa hovyo kwangu mimi na hauna tija yoyote kwenye kukabiliana na upungufu wa dola kwenye uchumi.
Na ninauona ni uamuzi wa kukurupuka kwasababu hakuna nadharia yeyote ya uchumi inayosema kwamba, dola ikiadimika basi unaongeza bei ili watu waache kuagiza bidhaa kwa lengo la kuzuia matumizi ya fedha za kigeni.
Kwasababu kiuchumi, unavoongeza bei ya kitu, maana yake unataka kupunguza demand ya kile kitu na pia kupunguza demand ya fedha za kigeni kwenye kuagiza kile kitu.
Lakini sasa, wewe unatakaje kupunguza demand ya bidhaa muhimu kama mafuta ambayo matumizi yake yana drive uchumi wa nchi? Automatically, mi ambacho nakiona kikitokea ni kuongezeka kwa pressure ya vitu kuanza kupanda bei kiholela kitu ambacho kwa sisi wanauchumi matokeo yake itakuwa kuongeza pressure ya inflation ambayo ndo itachochea Zaidi kupanda kwa bei ya dola na kuadimika kwake maradufu.
Maana yake ni kwamba, hicho wanachoogopa Makamba na Ewura, kwamba ‘kukosekana kwa dola ya kuagiza mafuta’, ndicho haswa wanaenda kuchangia kukisababisha kutokea kwa haraka, kwa uamuzi wao huu wa kukurupuka.
Kama nasema uongo, ‘wait and see’. Mwezi wa kumi nitarudi hapa kwenye huu uzi.
Mwisho kabisa, ni kweli kuna vitu vina vinatokea kwenye uchumi wa Tanzania kwa sasa, na ambavyo vinapeleka shillingi ya Tanzania inapoteza kwa kasi thamani yake tangu huu mwaka uanze.
Ila siwezi nikapenyeza hii mada kwenye huu uzi, lakini nachoweza kusema, na kwa maoni yangu baada ya utafiti ambao naendelea kuufanya, ni kwamba, kuna uzembe Fulani Benki kuu ya Tanzania wanafanya kwasasa ambao nina uhakika kabisa ndio chanzo cha hili sakata la kuadimika na kupanda haraka kwa bei ya dola kwenye uchumi. Ndo maana naona ni kama, na wao wamelala usingizi wa pono, kama hawa waliokurupuka na kupandisha bei yao ya mafuta.
Nitaweka uzi hapa soon.
N.Mushi