Bungeni Dodoma..

paul makuli

Member
Oct 21, 2010
39
34
Nimeshuhudia wajumbe wa ccm katika bunge la katiba wakimsikiliza Jaji Warioba,wakiwa wamenuna na wengi wakionyesha nyuso za huzuni,kunyong'onyea na wengine wana hasira kweli.Ni dhahiri kuwa ccm hawana nia njema na upatikanaji wa katiba mpya..Nawashauri tu wawe wapole hayo ndiyo maamuzi ya Wantanzania!!
 
Leo wamepata za uso kweli kweli na imebidi wawe wapole.Ninawasiwasi na waheshimiwa kutoka Zanzibar nadhani hawa wameshaungana na CUF na kuwaacha wabunge wenzao waCCM njia panda,maana yale makofi siyo ya kwaida.
 
CCM wasinune wala wasikasirike.Aliye wakirishi maoni ya wananchi ni mwanaccm damudamu waliotoa maoni ni wananchi wanaotawaliwa na CCM.
 
Leo wamepata za uso kweli kweli na imebidi wawe wapole.Ninawasiwasi na waheshimiwa kutoka Zanzibar nadhani hawa wameshaungana na CUF na kuwaacha wabunge wenzao waCCM njia panda,maana yale makofi siyo ya kwaida.

Kwa uhalisia linapokuja suala la Zanzibar, Wazanzibar wote huwa wamoja, hakuna cha CUF wala CCM. Wote wanatetea maslahi ya nchi yao.. Sisi huku bara Wabunge wa CCM ndiyo maadui wetu, badala wasimame kidete kutetea maslahi ya Tanganyika wao wamekaa kulinda maslahi ya CCM...

Lakini hebu wajiulize si CCM hata wale wenye kutetea serikali mbili,, ni nani yupo nyuma ya kuhakikisha Serikali tatu hazipiti ili tuendelee na Serikali mbili wakati taasisi nyeti kama Baraza la Wawakilishi, Bunge la Tanzania na Ofisi ya Waziri Mkuu walipendekeza Serikali Tatu..

Kuna watu wanatumika bila kujua wanatetea kwa maslahi ya nani.. Wanaotaka kuendelea na Serikali mbili ni watu wachache wenye kutaka kuendelea kuifisidi nchi hii wao pamoja na watoto wao.

Kwa darasa alilolitoa Mhe. Jaji Joseph Sinde Warioba, sioni mantiki ya mapendekezo ya CCM ya Serikali mbili zilizoboreshwa...

CCM wakubali tu na wajipange upya!!
 
Na haya ndiyo manejo yao ya mzaha mzaha katika hoja sensitive. Sijui Sendeka ana hali gani hivi sasa, siajabu bunge limehairishwa kwa ajili yao ili wakalie na kujaribu kujipanga upya.

January Makamba ‏@JMakamba 10m Kilichofanyika Bungeni leo ni kuorodhesha matatizo ya ndoa (ambayo ni ya kweli) halafu kisha kusema kwamba kuongeza mke ndio jawabu lake.
 
Kwa uhalisia linapokuja suala la Zanzibar, Wazanzibar wote huwa wamoja, hakuna cha CUF wala CCM. Wote wanatetea maslahi ya nchi yao.. Sisi huku bara Wabunge wa CCM ndiyo maadui wetu, badala wasimame kidete kutetea maslahi ya Tanganyika wao wamekaa kulinda maslahi ya CCM...

Lakini hebu wajiulize si CCM hata wale wenye kutetea serikali mbili,, ni nani yupo nyuma ya kuhakikisha Serikali tatu hazipiti ili tuendelee na Serikali mbili wakati taasisi nyeti kama Baraza la Wawakilishi, Bunge la Tanzania na Ofisi ya Waziri Mkuu walipendekeza Serikali Tatu..

Kuna watu wanatumika bila kujua wanatetea kwa maslahi ya nani.. Wanaotaka kuendelea na Serikali mbili ni watu wachache wenye kutaka kuendelea kuifisidi nchi hii wao pamoja na watoto wao.

Kwa darasa alilolitoa Mhe. Jaji Joseph Sinde Warioba, sioni mantiki ya mapendekezo ya CCM ya Serikali mbili zilizoboreshwa...

CCM wakubali tu na wajipange upya!!

well said mkuu only stupidity can run always from the truth
 
Najiuliza tu, hivi hawa majaji wote (Nyalali, Nyalali, Warioba na hata Augustino Ramadhani) ni kweli wote wamekuwa "hamnazo" kiasi hicho mpaka wote, hawa kwa nyakati tofauti, waje na mapendekezo ya serikali tatu?
 
Lisendeka halijalia humo bungeni? Maana sijapata koona masai toto la mama kama huyu. Safi sana Warioba.
 
Back
Top Bottom