Bunge linapitisha mambo mimi kama mtanzania nikiangalia naingia huzuni

saidoo25

JF-Expert Member
Jul 4, 2022
602
1,407
MWANAHABARI nguli na anayeheshimika nchini Tanzania, Pascal Mayala amelitupia lawama Bunge la Tanzania kwa kupitisha baadhi ya mambo ambayo kuna wakati yanampa huzuni na hasira kubwa.

"Kuna baadhi ya mambo ambayo Bunge letu limefanya ni mambo ndivyo sivyo,hakuna anayejua mambo haya ni ndivyo sivyo kwa sababu hata baadhi ya wabunge wenyewe hawazijui kanuni za Bunge"amesema Pascal

Pascal amesema wako wanasheria nguli kule bungeni na wazuri kabisa kuliko yeye lakini anasikitishwa na namna wanavyopitisha mambo yanayoacha simanzi kwa wananchi.

"Mimi nimesoma Sheria ni kama sisimizi tu kwenye sheria wako wanasheria waliobobea wako bungeni miaka na miaka kuna vitu ambavyo Bunge linafanya wanaviacha vinapita mimi kama mtanzania nikiangalia naingia huzuni naingia hasira na kusema kwamba sasa bunge la tanzania linahitaji watu type yangu ambao tutalisaidia Bunge letu" asema Mayalla.
.................................................................................................................

MOJA YA MFANO AMBALO BUNGE LETU TUKUFU NI KUPITISHA SHERIA YA KUWASAMEHE KODI WAWEKEZAJI MAHIRI SEPTEMBA 2022 HUKU WALALAHOI WAKIANDAMWA KULIPA KODI NA TRA

BUNGE LAPITISHA MUSWADA WA MAREKEBISHO YA SHERIA MBALIMBALI ZA FEDHA WA MWAKA 2022​

23 Sep, 2022​

BUNGE LAPITISHA MUSWADA WA MAREKEBISHO YA SHERIA MBALIMBALI ZA FEDHA WA MWAKA 2022

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepitisha Muswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali za Fedha wa mwaka 2022 (The Written Laws (Financial Provisions) Amendment Act, 2022), ambao unalenga kufanya marekebisho ya Sheria 6 za kodi, mirahaba na uwekezaji.

Akiwasilisha Muswaha huo bungeni jijini Dodoma, Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba alisema Lengo la Muswada huu ni kufanya marekebisho kwenye Sheria zinazosimamia kodi na mrabaha kwa kubadili viwango vya kodi na mrabaha.

Aliongeza kuwa Muswada huo unalenga kuweka taratibu za utoaji vivutio kwa wawekezaji ili kuhamasisha uzalishaji kwa viwanda vya ndani ya nchi vinavyozalisha mbolea na maguni ya mkonge, pamoja na kuondoa changamoto zilizopo katika utekelezaji wa Sheria ya uwekezaji Tanzania, Sura 38.


Mhe. Nchemba alizitaja Sheria zinazopendekezwa kufanyiwa marekebisho kupitia Muswada huo kuwa ni Sheria ya Ushuru wa Bidhaa Sura 147, Sheria ya Kodi ya Mapato Sura 332, Sheria ya Madini Sura 123, Sheria ya Ushuru wa Barabara na Mafuta Sura 220 na Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani Sura 148.

“Sehemu ya Pili ya Muswada yenye ibara za 3 hadi 5 inapendekeza kurekebisha Sheria ya Ushuru wa Bidhaa, Sura ya 147, ambapo kifungu cha 128 kinapendekezwa kurekebishwa ili kumpa mamlaka Waziri mwenye dhamana na masuala ya fedha, baada ya kupata idhini ya Baraza la Mawaziri kusamehe ushuru kwenye bidhaa zitakazotumika katika utekelezaji wa miradi ya uwekezaji mahiri na mahiri maalumu itakayoidhinishwa na Kamati ya Taifa ya Uwekezaji (NISC)”, alifafanua Dkt. Nchemba.
 
MOJA YA MFANO AMBALO BUNGE LIMEWAKOSEA SANA WATANZANIA NI KUPITISHA SHERIA YA KUWASAMEHE KODI WAWEKEZAJI MAHIRI SEPTEMBA 2022 HUKU WALALAHOI WAKIANDAMWA KULIPA KODI NA TRA
Pascal Mayalla unaposema Wawekezaji Mahiri,, hili ni kundi la wawekezaji wapi..? Yaani Muwekezaji Mahiri ni yupi katika taifa hili.?

Maana Juzi Kijana wa WCB alilalamika anavamiwa na TRA na wamemuibia Pesa kwenye Acc zake, na kuna yule wa Zanzibar nae alilalamika.. Hao Wawekezaji Mahiri ni wapi sasa?..
 
Pascal Mayalla unaposema Wawekezaji Mahiri,, hili ni kundi la wawekezaji wapi..? Yaani Muwekezaji Mahiri ni yupi katika taifa hili.?

Maana Juzi Kijana wa WCB alilalamika anavamiwa na TRA na wamemuibia Pesa kwenye Acc zake, na kuna yule wa Zanzibar nae alilalamika.. Hao Wawekezaji Mahiri ni wapi sasa?..
Walipa kodi wakubwa wamefutiwa kulipa kodi kwa mujibu wa sheria ya Bunge.
 
Back
Top Bottom