Bunge lakanusha Kauli ya Mbowe kuwa Mshahara wa Wabunge umepanda kutoka Tsh Milioni 13 hadi 18

Maneno ya kukana hoja Hizo yametolewa na Kitengo cha mawasiliano na uhusiano wa kimataifa Bungeni..

Jana Ijumaa tarehe 22 Machi, 2024 alipokuwa anahutubia mkutano wa hadhara Mjini Babati Mkoa wa Manyara na kisha Video yake kusambaa kwenye Mitandao ya Kijamii Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe. Freeman Mbowe amedai kwamba mishahara ya Waheshimiwa Wabunge imeongezwa mwaka 2023 kutoka shilingi milioni kumi na tatu (sh.13,000,000/=)
hadi shilingi milioni kumi na nane (sh.18,000,000/=)


View attachment 2942304
Kama wanakanusha waweke hadharani wanalipwa kiasi gani na mchanganuo wake watuwekee
 
Kinachomuumiza mbowe sio mishahala ya wabunge ni yeye kutokuwa sehemu ya huo ulaji
 
Maneno ya kukana hoja Hizo yametolewa na Kitengo cha mawasiliano na uhusiano wa kimataifa Bungeni..

Jana Ijumaa tarehe 22 Machi, 2024 alipokuwa anahutubia mkutano wa hadhara Mjini Babati Mkoa wa Manyara na kisha Video yake kusambaa kwenye Mitandao ya Kijamii Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe. Freeman Mbowe amedai kwamba mishahara ya Waheshimiwa Wabunge imeongezwa mwaka 2023 kutoka shilingi milioni kumi na tatu (sh.13,000,000/=)
hadi shilingi milioni kumi na nane (sh.18,000,000/=)


View attachment 2942304
Hakuna sehemu wanaonesha kukana zaidi wameweka maneno tuu! Nilitegemea waseme mishahara ilikuwa kiasi fulani hadi mwaka huu na hakuna ongezeko cha kiasi hiki….

Hakuna kanusho hapo zaidi ni wazi wabunge wameongezewa mishahara kuto million kumi na mbili hadi million 18 na ni ongezeko la million 6 ! Yani unawaongeza watu million sita tena wasio katwa kodi yeyote ile…hii nchi ina laana…
 
97.5% ya wabunge wapo mjengoni kwa ajili ya maokoto.

Hizo 2% ni wale wafanya biashara wakubwa wapo pale kufanikisha mambo yao.
0.5% wapo pale kusaidia majimbo yao.

Ubunge unachukuliwa ni kama sehemu ya kutafuta maisha zaidi kuliko kutatua kero za wananchi.

Bongo wanasiasa wengi waneingia kwenye mifumo kwa sababu ni chawa wazuri au ndugu za vigogo na akili hawana, wenye akili wapo mtaani.
Wengine kuiba kura kumewafanya waingie kwenye uongozi, je hio nchi kuna maendeleo?
Aiseee,ni hatari sana.
 
Ni million 18 kwa sasa kama hujui jambo bora unyamaze mimi mwenyewe nimepata uthibitisho wa habari hii na waliosema ndio wanaolipwa hiyo hela
Duh yaani inamaana wamejiongezea du napiga hesabu tu kwa haraka haraka..
Wabunge wapo 393..

So kwa mwezi ni 393x18 Mil = 7,074,000,000

Bilion 7
Kwahiyo kwa Mwezi Taifa linatoa Tsh bilion 7 na milion 74 kulipa wabunge...

Ambayo ni sawa na Tsh 84,888,000,000 Kwa mwaka..
Yaani serkali inapoteza Tsh Bilion 84 na Milion 888 kwa ajili ya kulipa.watu wanaokaa na kusifia
 
Wanajionaga wao ndo wanaakili nasisi ni wakudanganywa kipuuzi??! Mbowe ashindwe kumuuliza hata Mdee walivyo washkaji!!
Hii nchi Maviongozi hawana huruma ndomana wakianza kumsifu mkuu wao wanatumika nguvu zao zooote!! Unashangaa kunamaskini nao husifu hovyo
Milioni 18 huku watoto na walimu wao wanaanguka njaa kwakukosa chakula shuleni alafu mpuuzi anakwambia mama anaupigia mwingi
Halafu wanaomba msaada wa mchele marekan daaah hii nchi inaviongoz wa ovyo kabsaaa

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Kumbe waheshimiwa wetu wanapewa mishahara kidogo hivyo mil13 ni ndogo sana ukilinganisha na majumu mazito wanayoyafanya kwaajili yetu.Waongeze angalau mil 29 Kwa mwezi ili kuendana na maisha ya sasa.Mishahara Yao ikiwa midogo hata utendaji kazi unapungua.Waheshimiwa kwanza sisi baadae.
 
Bunge limetudanganya. Mbowe hajawahi kusema nyongeza ya mshahara bali alisema kuhusu nyongeza ya marupurupu na posho za wabunge. Siku zote wabunge wamekuwa wakilipwa mshahara kidogo sana na kujilipa maposho na marupurupu kufuru. Na hapa ndipo serikali ya kifisadi ya CCM inapopiga fedha za umma. Nchi hii ina mijitu ya ajabu sana. Ni bora hata ife ili nchi ipate kupona. Mipuuzi mikubwa!
The Green Mambas Parliament!!
 
Back
Top Bottom