Bunge lajigeuka: Tutaendelea kurusha 'LIVE' vikao vya Bunge...

Hiyo TV ya Bunge inalipiwa na nani?Ni huyu mlipa kodi?Au aliogopa meseji za wanatanzania?Katibu aanze na kushauri mabosi wake wajiuzuru akifuatia na yeye mwenyewe maana hii kasi ya vijana wameshindwa kwenda nayo
 
Bunge lasalimu amri


na Waandishi wetu
TANZANIA DAIMA



WAKATI Jukwaa la Wahariri Tanzania likiazimia kususia kuripoti mikutano yote ya Bunge kutokana na kukerwa na uamuzi wa kupiga marufuku kurushwa moja kwa moja kwa vikao, Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashililah ameibuka na kukana kutoa kauli hiyo.

Katika hatua isiyokuwa ya kawaida, jana Jukwaa la Wahariri lilisema kuwa limepokea kwa mshangao mkubwa kauli ya Kashililah ya Jumatano wiki hii, ya kutaka kuzuia kurushwa kwa mikutano ya Bunge, badala yake itaruhusu kurekodi vipindi hivyo na kuvirusha baadaye vikiwa vimehaririwa, na kwamba ofisi yake inawasiliana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kupata njia ya kurusha matangazo hayo.

Mwenyekiti wa jukwaa hilo, Absalom Kibanda aliwaambia waandishi wa habari kuwa: “Tunashangaa Bunge la Tanzania limejifunza wapi siasa hizi za kufunika mambo yanayowahusu wananchi, huku likijua kwamba wanaofuatilia vikao hivyo ndio walipa kodi na wapiga kura wa wabunge ambao uongozi wa Bunge unataka kuwalinda.”

Alisema kuwa tamko la Katibu wa Bunge linaenda kinyume na la Haki za Binadamu, Desemba 10, 1948 ambapo Kifungu cha 19 cha tamko hili (kifungu cha 19) kinatoa uhuru wa mtu kutoa na kupokea mawazo bila kujali mipaka ya nchi na haki hii ya kutoa mawazo haipaswi kuingiliwa.

Kibanda alisisitiza kuwa kutokana na kuridhia tamko hilo la kimataifa Bunge lilifanya mabadiliko ya tano ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1984 ambayo kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hii, yaliliingiza tamko hili la Haki za Binadamu hivyo kuwezesha Ibara ya 18 ya katiba hiyo ya 1977 kuakisi kifungu cha 19 cha tamko hiko kwa kutoa uhuru wa mawasiliano na haki ya kupewa taarifa.

Alisema jitihada zozote za kuwafungia wabunge ndani na kuhariri kazi wanazofanya na matamko wanayotoa, ni ishara kwamba Bunge linataka kuficha maovu au udhaifu wa mhimili huo au mihimili mingine inayowajibishwa na wabunge, na kwamba hatua hiyo itakuwa inawachimbia kaburi la kisiasa wabunge kwani ndio wanaomulikwa kwa majibu ya maswali wanayoulizwa na hatua wanazochukua.

“Jukwaa la Wahariri limesisitiza kwamba utaratibu huu unaoandaliwa sasa na Dk. Kashililah ni wa kidikteta na ni mbaya kuliko udikteta wowote uliowahi kutokea hapa nchini kwa miaka yote ya uhuru wa Tanzania. Na kusema kuwa harakati hizi za uongozi wa sasa wa Bunge zinaonekana kama hatua za kufuta yaliyofanywa na uongozi wa Bunge la tisa.

“Jukwaa limetahadharisha kuwa katika mazingira haya, linaamini kwamba iwapo hili litatokea, jitihada ndogo za uwazi zilizokuwa zimefanywa na Serikali ya Rais Jakaya Kikwete, zitafutika na kumfanya aonekane mbele ya jumuiya ya kimataifa kuwa kiongozi dhalimu na dikteta asiyevumilia kukosolewa, na itaifanya serikali na Bunge visiaminike kwa umma na itasababisha zogo na vurugu zisizomithilika kwani waliojifungia ndani watatoka na kusema hadharani kwa jinsi watakavyoona inafaa hivyo kuharibu kabisa mfumo wa taarifa za chombo hicho,” alisema Kibanda.

Bunge lakana
Wakati Jukwaa la Wahariri likitoa mashambulizi hayo mazito, Dk. Kashililah amekana kutoa matamshi hayo akidai kunukuliwa vibaya na vyombo vya habari.
Katika taarifa yake ya jana kwa vyombo vya habari, ofisi ya Bunge imesema imepokea kwa masikitiko taarifa kuhusu tafsiri ya kusitisha matangazo ya shughuli za bungeni na kamati, kinyume na jinsi ilivyoakisiwa katika mazungumzo ya pamoja kati ya wanahabari na katibu wa ofisi hiyo Dk. Kashililah.

Katika taarifa hiyo jana, Dk. Kashililah pamoja na kuomba radhi kwa wananchi kwa taarifa hizo, alisema Bunge halina mpango wa kusitisha matangazo yake wala kamati zake, ambazo kwa mahitaji ya sasa nazo zinapaswa kurushwa moja kwa moja kama sehemu ya mpango kabambe wa kuwapasha wananchi yanayojiri katika uendeshaji bora wa shughuli zake.

“Dhamira ya Bunge ni kuhakikisha kuwa mpango kabambe uliopo ni kumfikia kila Mtanzania alipo na kwa uwezo alionao aweze kupata na kushiriki katika uendeshaji wa shughuli za Bunge… hivyo mpango mkakati uliopo utakuwa kuboresha mawasiliano ya kawaida kupitia teknolojia ya mawasiliano,” ilisema taarifa ya Bunge.

Aidha, taarifa hiyo ilisema kwamba kwa wale watakaokuwa na uwezo wa kupata huduma za mtandao, wataweza kuona picha za video kupitia tovuti ya Bunge.

Ilisema kwa wale watakaokuwa na uwezo wa kushika mawimbi ya redio, wataweza kufuatilia majadiliano katika redio ya Bunge inayotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni katika masafa yanayopatikana nchi nzima kama redio zingine zinazotoa huduma hiyo hapa nchini.

“Hivyo utaratibu uliopo sasa utaendelea kutumika ambapo vituo vyote vya televisheni vitapewa fursa ya kurusha matangazo kwa utashi wao bila kuwekewa mipaka ya aina yoyote sambamba na matangazo yatakayotolewa na mitandao ya Bunge,” ilisema.

Kwamba utaratibu huo unatokana na uamuzi wa pamoja kati ya Bunge na Tume ya Mawasiliano Nchini (TCRA) kwamba vipindi vyote vya Bunge vitakuwa vinarushwa bila kudhaminiwa na taasisi yoyote zaidi ya hiyo.

“Hivyo basi kwa maelezo hayo ni dhahiri kuwa Bunge halina mpango wa kusitisha matangazo ya TV wala yale ya redio au teknohama bali linatarajia kuboresha upatikanaji wa huduma kwa utaratibu ulio rahisi na unaoweza kusimamiwa na pande zote, yaani Bunge na wananchi,” ilisema taarifa hiyo.

Kashililah alisema televisheni zote zinazorusha matangazo ya Bunge hupata toka katika mitambo yake na pale wanapoona yafaa basi huomba kutumia mitambo yao na hivyo kutumia fursa hiyo kuingiza kamera na wanahabari ndani ya kumbi za Bunge.

“Kuzingatia mabadiliko tajwa, utaratibu huo umepewa ukomo ila sasa hapatakuwa na fursa ya kuingiza kamera ndani ya kumbi za Bunge, bali wote watakaotaka kurusha matangazo ya Bunge kwa utashi wao, watapata clear feed toka katika mitambo yake hivyo kurusha live vipindi vyote vya Bunge bila kuhaririwa kama ilivyonakiliwa katika makala mbalimbali.

“Hata hivyo utaratibu huu wa kutumia camera katika kumbi utaendelea katika kamati za Bunge, hadi hapo mitambo mipya ya mawasiliano itakapofungwa katika kumbi zote za kamati.

“Hivyo basi, ili kwenda sawia na taratibu hizo, Bunge litaendesha zoezi la kuwatathmini waandishi wote wa habari za Bunge na kuwasajili kwa vigezo vitakavyoafikiwa kati ya Baraza la Habari, hivyo basi, wakati zoezi la maboresho hayo likiendelea, wananchi watajulishwa kila hatua na matarajio tajwa,” ilisema taarifa hiyo ya Bunge.

Tangu kutolewa kwa tamko hilo la vikao vya Bunge kutorushwa ‘live’, makundi mbalimbali na wanasiasa walilaani wakisema kuwa limelenga kuisaidia serikali kutoumbuka. Walisema takriban mwaka sasa, serikali imekuwa ikivuliwa nguo hadharani na wabunge hususan wa kambi ya upinzani, na pia kushuhudia jinsi kupitia kiti cha spika jinsi wapinzani walivyokuwa wakidhibitiwa kwa uonevu mkubwa.

 
Chezeya NGUVU YA UMMA weye!!! Eti alinukuliwa vibaya!!!...P......f!:target:
 
Kama tuna televisheni ya taifa inyoendeshwa kwa kodi zetu, kuna haja gani ya kukamua zaidi jasho la mtanzania kuanzisha televisheni ya bunge?
Kwa nini TBC isisimamiwe kuwa chombo kisichoegemea upande mmoja na ikatakiwa kuripoti matangazo yote ya bunge bila kukatisha?
 
Viongozi kama huyu Katibu wa bunge wakati mwingine unaweza ukafikiri wanafanya jambo makusudi ili kuibomoa serikali. Inashangaza kama hakufahamu backlash itakuwaje kwenye jamii kwa tamko lake hili la kipumbavu. Kama hakufikiria kitu kama hiki basi hapaswi hata kuwepo kwenye hiyo nafasi yake. He's just phoney.
 
dr. kashililla, mbona taarifa uliyoitoa kwa waandishi wa habari kuhusu kuminya matangazo ya bunge ilinukuliwa kama ulivyoitoa! how comes unasema ulikuwa misquoted? kama mtayachakachua matangazo hayo itawaathiri zaidi ccm kwani taarifa zitakazokuwa zinatolewa na wabunge wa upinzani dhidi ya ccm zitaaminiwa zaidi hata kama zitakuwa hazina ukweli, serikali pia itaathirika zaidi kwani chochote kibaya kinaweza kusemwa na upinzani kuwa kimeletwa na serikali hata kama jambo hilo halikutokea bungeni litaaminiwa na umma kwa sababu wanaamini kuwa upinzani unasema ukweli ndio maana umeamua kuminya matangazo hayo. vituko hivi sivishangai ni mambo ambayo hutokea katika chama tawala kinachokuwa katika mpito wa kuelekea kupoteza dola. wamekwishapoteza dira na hivyo 2015 watapoteza dola.
 
Lakini ukiisoma vema hiyo statement yao bado kuna mtego. Watakachokuwa wanafanya ni wao wenyewe Bunge kupiga picha na kurekodi sauti na kisha kuwapa waandishi link ya kurusha watakavyo. Trick ipo hapo kwenye kupiga p[icha na kurekodi, tuna uhakika gani watapiga picha zile ambazo watu watataka kuziona? Si ajabu Chadema watakapoamua kusimama tena kushinikiza hoja zao hatutaziona picha hizo, au Tundu Lissu atakapokuwa anampa Spika vidonge kwa kusigina kanuni, tunaweza tusiwekewe hiyo sauti

Yes, there is a point to note!
Tutayaona, na kama watakuwa wanakata wabunge wetu CDM watufahamishe na watupe namba za vilaza hao!
 
Back
Top Bottom