Bunge lajigeuka: Tutaendelea kurusha 'LIVE' vikao vya Bunge...

Tujikumbushe Naibu Spika akiwashukia waandishi wa habari kwa kuwabeba 'wapinzani':

Published on 24 Aug 2012Naibu Spika wa Bunge Job Ndugai akifungua warsha ya waandishi wa habari za Bunge mjini Dodoma na kuwashukia waandishi wa habari, twitter, mitandao ya jamii kuwabeba wabunge 'wapinzani' na pia kugusia 'mabadiliko ya kanuni' za Bunge, Pia anasifia kupigiwa simu na wapiga kura/wananchi kupewa mrejesho walete hoja ya kuzuia kurusha Bunge 'live' au 'matusi toka kwa wananchi kwa njia ya simu !?? endelea kusikia maneno ya Naibu Spika
!?! Sasa ni kipi kimebadilika mpaka


video kwa hisani ya absalom kibanda wa youtube
 
Last edited by a moderator:
Bado kuna kitu inabidi tukielewe vizuri hapo!kama Bunge ni la demokrasia na huru,kwa nini wachuje waandishi na vigezo vyao?hapo ndio uhasama na kulipizana visasi kutaanza!Media ni vyombo huru na katiba inasema hivyo kwa nini Kashilila anataka nae ufalme wake utukuzwe?ina maana wakiona umerusha live kitu wasichokipenda,wanakufungia usirushe matangazo yao!hivi bado tuko chama kimoja au?si warudishe mfumo wa chama kimoja tu?
 
Hakika Chadema Inatisha.Tamko la John Mnyika tu la Jana wamesalimu Amri.Ahsanteni sana Chadema.Mungu awabariki kututetea wanyonge.

Ujue hizi propaganda za watawala sio dili eeh!
Ama Kashilila alitumwa kupima upepo ili watathmini kama utapita ama lah?

yale yale
 
Nimekukubali kuwa we nae ulishayaona pj na j kuwa ni mabwege yaliyokubuhu hawa walitakiwa kuimba taarabu utangazaji siyo fan yao
 
This paper is undated, no headed, no muhuri? hata sielewi kama hii ni safa ----- ama vipi. huwa hawachelewi kugeuka.
 
Taarifa yenyewe inamdhalilisha aliyetia signature (Dr.) Editing haikufanywa kwa taarifa muhimu hivi!
Pia kuandikaRTD inanesha jinsi mwandishi anavyofikiri kizamani na ndipo walikotaka kutupelekaktk zamani za kutopata vipindi vya bunge live. Hamieni digitali kweli.
 
na Waandishi wetu


amka2.gif
WAKATI Jukwaa la Wahariri Tanzania likiazimia kususia kuripoti mikutano yote ya Bunge kutokana na kukerwa na uamuzi wa kupiga marufuku kurushwa moja kwa moja kwa vikao, Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashililah ameibuka na kukana kutoa kauli hiyo.
Katika hatua isiyokuwa ya kawaida, jana Jukwaa la Wahariri lilisema kuwa limepokea kwa mshangao mkubwa kauli ya Kashililah ya Jumatano wiki hii, ya kutaka kuzuia kurushwa kwa mikutano ya Bunge, badala yake itaruhusu kurekodi vipindi hivyo na kuvirusha baadaye vikiwa vimehaririwa, na kwamba ofisi yake inawasiliana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kupata njia ya kurusha matangazo hayo.
Mwenyekiti wa jukwaa hilo, Absalom Kibanda aliwaambia waandishi wa habari kuwa: “Tunashangaa Bunge la Tanzania limejifunza wapi siasa hizi za kufunika mambo yanayowahusu wananchi, huku likijua kwamba wanaofuatilia vikao hivyo ndio walipa kodi na wapiga kura wa wabunge ambao uongozi wa Bunge unataka kuwalinda.”
Alisema kuwa tamko la Katibu wa Bunge linaenda kinyume na la Haki za Binadamu, Desemba 10, 1948 ambapo Kifungu cha 19 cha tamko hili (kifungu cha 19) kinatoa uhuru wa mtu kutoa na kupokea mawazo bila kujali mipaka ya nchi na haki hii ya kutoa mawazo haipaswi kuingiliwa.
Kibanda alisisitiza kuwa kutokana na kuridhia tamko hilo la kimataifa Bunge lilifanya mabadiliko ya tano ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1984 ambayo kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hii, yaliliingiza tamko hili la Haki za Binadamu hivyo kuwezesha Ibara ya 18 ya katiba hiyo ya 1977 kuakisi kifungu cha 19 cha tamko hiko kwa kutoa uhuru wa mawasiliano na haki ya kupewa taarifa.
Alisema jitihada zozote za kuwafungia wabunge ndani na kuhariri kazi wanazofanya na matamko wanayotoa, ni ishara kwamba Bunge linataka kuficha maovu au udhaifu wa mhimili huo au mihimili mingine inayowajibishwa na wabunge, na kwamba hatua hiyo itakuwa inawachimbia kaburi la kisiasa wabunge kwani ndio wanaomulikwa kwa majibu ya maswali wanayoulizwa na hatua wanazochukua.
“Jukwaa la Wahariri limesisitiza kwamba utaratibu huu unaoandaliwa sasa na Dk. Kashililah ni wa kidikteta na ni mbaya kuliko udikteta wowote uliowahi kutokea hapa nchini kwa miaka yote ya uhuru wa Tanzania. Na kusema kuwa harakati hizi za uongozi wa sasa wa Bunge zinaonekana kama hatua za kufuta yaliyofanywa na uongozi wa Bunge la tisa.
“Jukwaa limetahadharisha kuwa katika mazingira haya, linaamini kwamba iwapo hili litatokea, jitihada ndogo za uwazi zilizokuwa zimefanywa na Serikali ya Rais Jakaya Kikwete, zitafutika na kumfanya aonekane mbele ya jumuiya ya kimataifa kuwa kiongozi dhalimu na dikteta asiyevumilia kukosolewa, na itaifanya serikali na Bunge visiaminike kwa umma na itasababisha zogo na vurugu zisizomithilika kwani waliojifungia ndani watatoka na kusema hadharani kwa jinsi watakavyoona inafaa hivyo kuharibu kabisa mfumo wa taarifa za chombo hicho,” alisema Kibanda.
Bunge lakana
Wakati Jukwaa la Wahariri likitoa mashambulizi hayo mazito, Dk. Kashililah amekana kutoa matamshi hayo akidai kunukuliwa vibaya na vyombo vya habari.
Katika taarifa yake ya jana kwa vyombo vya habari, ofisi ya Bunge imesema imepokea kwa masikitiko taarifa kuhusu tafsiri ya kusitisha matangazo ya shughuli za bungeni na kamati, kinyume na jinsi ilivyoakisiwa katika mazungumzo ya pamoja kati ya wanahabari na katibu wa ofisi hiyo Dk. Kashililah.
Katika taarifa hiyo jana, Dk. Kashililah pamoja na kuomba radhi kwa wananchi kwa taarifa hizo, alisema Bunge halina mpango wa kusitisha matangazo yake wala kamati zake, ambazo kwa mahitaji ya sasa nazo zinapaswa kurushwa moja kwa moja kama sehemu ya mpango kabambe wa kuwapasha wananchi yanayojiri katika uendeshaji bora wa shughuli zake.
“Dhamira ya Bunge ni kuhakikisha kuwa mpango kabambe uliopo ni kumfikia kila Mtanzania alipo na kwa uwezo alionao aweze kupata na kushiriki katika uendeshaji wa shughuli za Bunge… hivyo mpango mkakati uliopo utakuwa kuboresha mawasiliano ya kawaida kupitia teknolojia ya mawasiliano,” ilisema taarifa ya Bunge.
Aidha, taarifa hiyo ilisema kwamba kwa wale watakaokuwa na uwezo wa kupata huduma za mtandao, wataweza kuona picha za video kupitia tovuti ya Bunge.
Ilisema kwa wale watakaokuwa na uwezo wa kushika mawimbi ya redio, wataweza kufuatilia majadiliano katika redio ya Bunge inayotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni katika masafa yanayopatikana nchi nzima kama redio zingine zinazotoa huduma hiyo hapa nchini.
“Hivyo utaratibu uliopo sasa utaendelea kutumika ambapo vituo vyote vya televisheni vitapewa fursa ya kurusha matangazo kwa utashi wao bila kuwekewa mipaka ya aina yoyote sambamba na matangazo yatakayotolewa na mitandao ya Bunge,” ilisema.
Kwamba utaratibu huo unatokana na uamuzi wa pamoja kati ya Bunge na Tume ya Mawasiliano Nchini (TCRA) kwamba vipindi vyote vya Bunge vitakuwa vinarushwa bila kudhaminiwa na taasisi yoyote zaidi ya hiyo.
“Hivyo basi kwa maelezo hayo ni dhahiri kuwa Bunge halina mpango wa kusitisha matangazo ya TV wala yale ya redio au teknohama bali linatarajia kuboresha upatikanaji wa huduma kwa utaratibu ulio rahisi na unaoweza kusimamiwa na pande zote, yaani Bunge na wananchi,” ilisema taarifa hiyo.
Kashililah alisema televisheni zote zinazorusha matangazo ya Bunge hupata toka katika mitambo yake na pale wanapoona yafaa basi huomba kutumia mitambo yao na hivyo kutumia fursa hiyo kuingiza kamera na wanahabari ndani ya kumbi za Bunge.
“Kuzingatia mabadiliko tajwa, utaratibu huo umepewa ukomo ila sasa hapatakuwa na fursa ya kuingiza kamera ndani ya kumbi za Bunge, bali wote watakaotaka kurusha matangazo ya Bunge kwa utashi wao, watapata clear feed toka katika mitambo yake hivyo kurusha live vipindi vyote vya Bunge bila kuhaririwa kama ilivyonakiliwa katika makala mbalimbali.
“Hata hivyo utaratibu huu wa kutumia camera katika kumbi utaendelea katika kamati za Bunge, hadi hapo mitambo mipya ya mawasiliano itakapofungwa katika kumbi zote za kamati.
“Hivyo basi, ili kwenda sawia na taratibu hizo, Bunge litaendesha zoezi la kuwatathmini waandishi wote wa habari za Bunge na kuwasajili kwa vigezo vitakavyoafikiwa kati ya Baraza la Habari, hivyo basi, wakati zoezi la maboresho hayo likiendelea, wananchi watajulishwa kila hatua na matarajio tajwa,” ilisema taarifa hiyo ya Bunge.
Tangu kutolewa kwa tamko hilo la vikao vya Bunge kutorushwa ‘live’, makundi mbalimbali na wanasiasa walilaani wakisema kuwa limelenga kuisaidia serikali kutoumbuka. Walisema takriban mwaka sasa, serikali imekuwa ikivuliwa nguo hadharani na wabunge hususan wa kambi ya upinzani, na pia kushuhudia jinsi kupitia kiti cha spika jinsi wapinzani walivyokuwa wakidhibitiwa kwa uonevu mkubwa.


source: tanzania daima
 
Hawa wanajikanyaga,jana ndugai kasema wanampango huo wa kuzuia tbc1 kurusha bunge litakua na tv yake ya kuchakachua halafu station zingine zinunue rights.TUMWAMINI NANI?hii haina tofauti na lile sakata la posho za wabunge
 
nchi ya Mazingaombwe...siji kuiamini tena kauli ya serikali ya jk.!

Nilijua tu atasema amenukuliwa vibaya kwani sauti yake iliyorekodiwa nayo ilirekodi vibaya?Dr kuomba radhi ni uungwana usipindishe pindishe maneno
 
Nilijua tu atasema amenukuliwa vibaya kwani sauti yake iliyorekodiwa nayo ilirekodi vibaya?Dr kuomba radhi ni uungwana usipindishe pindishe maneno
mkuu nashangaa hata waandishi wa habari wamekaa kimya, kwa nini wasimkanushe kuwa walichokinukuu ndicho alichokisema.?
 
Naomba kuuliza, hii ni taarifa rasmi ya ofisi ya Bunge? kwa sababu naona inamakosa ya kiuandishi sana, mfano, je ni kweli kwamba redio kama RTD ambayo ni TBC, BBC na STAR ambayo sijui kama kuna redio hiyo, zinarusha matangazo ya Bunge live? na makosa mengine ya kiuandishi yanayonipa wasiwasi na taarifa hii... nijuzeni.
 
Kuzingatia mabadiliko tajwa, utaratibuhuo umepewa ukomo, ili sasa hapatakuwa na fursa ya kuingiza Camera ndani yaKumbi za Bunge, bali wote watakaotaka kurusha matangazo ya Bunge kwa utashiwao, watapata clear feed toka katikamitambo ya Bunge na hivyo kurusha livevipindi vyote vya Bunge bila kuhaririwa kama ilivyonakiliwa katika makala mbalimbali. Hata hivyo utaratibu huu wa kutumia Camerakatika Kumbi utaendelea katika Kamati za Bunge, hadi hapo mitambo mipya ya mawasilianoitakapofungwa katika Kumbi zote za Kamati. Hivyo basi, ili kwenda sawia nataratibu hizo, Bunge litaendesha zoezi la kuwatathmini Waandishi wote wa habariza Bunge na kuwasajili kwa vigezo vitakavyoafikiwa kati ya Baraza la Habari,Idara ya Habari na Bunge lenyewe.

Aidha ili kulinda heshima na maadiliya utangazaji, Bunge litatoa utaratibu (
Codeof Conducts for Media broadcasting) wa namna ya kunakili na kurushamatangazo ya Bunge bila kujali yanarushwa kwa utaratibu upi. Hili litasaidia kuweka misingi bora yamawasilaino na hivyo kuwapa fursa Wananchi kujua hali halisi ya matukio yotendani ya Bunge na katika Kamati, bila kuegemea upande wowote (Non Partisan).


Tunasikitika kwa usumbufu uliowasibuwote walioakisiwa na taarifa hiyo.


Dr. Thomas D.Kashililah

KATIBUWA BUNGE

Kama hii taarifa imeandikwa na PhD, basi tuna matatizo makubwa. Hii mambo ya kuingilia kazi za watu na kuanza ku-'type' wakati siyo fani yako, inatugharimu.. 'Spacing'-balaa.., maneno ya kiswanglish, hakuna saini.. Sidhani hata kama ilikuwa kwenye 'headed paper'. Bado umakini ni tatizo...
Hii taarifa bado ina harufu ya 'censorship', 'muda utasema'..
 
Kama hii taarifa imeandikwa na PhD, basi tuna matatizo makubwa. Hii mambo ya kuingilia kazi za watu na kuanza ku-'type' wakati siyo fani yako, inatugharimu.. 'Spacing'-balaa.., maneno ya kiswanglish, hakuna saini.. Sidhani hata kama ilikuwa kwenye 'headed paper'. Bado umakini ni tatizo...
Hii taarifa bado ina harufu ya 'censorship', 'muda utasema'..
Wala kuchapa si kazi ngumu ya kusomea ikamshinda PhD,inakuwaje PhD mzima hajui hata kuchapa taarifa ya kiofisi,ama kweli Tanzania ni nchi ya ajabu sana.Ndo hasara ya PhD za online na vyeo vya kupeana.Zama hizi na kipindi tumeshuhudia watu wakipenda kuitwa PhD wakati competence yao ni level ya Diploma.Ama kweli safari ni ndefu maana hata taarifa za ikulu nazo huna zina makosa ya kiuandishi.WE NEED CHANGES OF THE WHOLE SYSTEM.
 
Ina maana KASHILILAH ULINUKULIWA VIBAYA?

Hajanukuliwa vibaya. Kila aliyesikiliza TBCCM siku hiyo alimsikia "Live" akisema kitendo cha kusitisha matangazo hayo ni kujenga "Maadili" kwa vijana wetu ....... (Dr (wa Kichina) Kashillilah, 2013)
 
JAMHURI YA MUUNGANO WATANZANIA

BUNGE LA TANZANIA

__________

TAARIFA MAALUM KUHUSU BUNGE NA KAMATI

______________

Ofisi ya Bunge imepokea kwa masikitiko taarifa kuhusu tafsiri ya kusitisha matangazo ya Shughuli za Bunge na Kamati, kinyumena jinsi ilivyoakisiwa katika mazungumzo ya pamoja kati ya Wanahabari na Katibuwa Bunge.



Dr. Thomas D.Kashililah

KATIBUWA BUNGE


..............

UNAFIKI wa nini Dr KASHILILAH !!!!!!!!!!!!!!!!!! SISI SIO WATANZANIA WA ZAMA za CHAMA KIMOJA KUSHIKA HATAMU
 
huo ni mpango wa kuanzisha bunge kusimamia yenyewe urushaji wa matangazo ili waweze kufanya jambo lolote endapo wamebanwa na upinzani mf. kukatisha matangazo, kutoonesha wabunge wanaosinzia bungeni na kupendelea zaidi chama tawala
 
Back
Top Bottom