Bashungwa aitaka TANROADS kupanda na kuhudumia miti katika maeneo ya barabara

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
666
835
BASHUNGWA AITAKA TANROADS KUPANDA NA KUHUDUMIA MITI KATIKA MAENEO YA BARABARA

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ameuagiza Wakala wa Barabara (TANROADS) kuendelea kupanda na kuhudumia miti iliyopandwa katika maeneo ya barabara kwa ajili ya kuendelea kupendezesha miji na kutunza mazingira ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Bashungwa amezungumza hayo katika Ofisi za Wizara zilizopo katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma leo Januari 29, 2024 wakati akiongoza zoezi la upandaji miti kwa ajili ya kuendeleza kampeni ya upandaji miti iliyozinduliwa na Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango.

Ameitaka TANROADS kuhakikisha inaendelea kuhudumia miti walioipanda katika barabara ya Chimwaga - St. Peter Claver (km 10), jijini Dodoma na kuwasisitiza kurudishia miti iliyokufa ili kuendelea kuboresha na kupendezesha eneo hilo.

“Hakikisheni TANROADS mnaihudumia miti mliyoipanda katika barabara ya Chimwaga - St. Peter Claver (km 10), mnaiangalia kwa ukaribu na kupanda miti mipya kwa ile iliyokufa kama mlivyoelekezwa na Mhe. Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango”, amesema Bashungwa.

Bashungwa ametoa wito kwa watanzania kuendelea na tabia ya kupanda miti na wasisubiri kupewa maagizo kutoka kwa viongozi wakuu wa Serikali.

“Tabia ya kupanda miti iwe ni ya hiyari, tusisubiri hadi viongozi wakuu kusisitiza kufanya hivyo muendele na tabia hii hata majumbani kwenu, ikiwa mti utakufa basi rudishieni mti mwingine tena”, amesema Bashungwa.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Mhandisi Aisha Amour, amesema kuwa zoezili hilo limeshirikisha upandaji wa miti tofauti zaidi ya 100 ikiwemo miti ya matunda na kivuli.

Balozi Aisha ameahidi kuendelea kuitunza miti hiyo na kuongeza miti mingine zaidi ili kuendelea kuifanya Ofisi hiyo kuwa ya kijani.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi
 

Attachments

  • IMG-20240129-WA0864.jpg
    IMG-20240129-WA0864.jpg
    780.4 KB · Views: 2
  • IMG-20240129-WA0884(1).jpg
    IMG-20240129-WA0884(1).jpg
    775.8 KB · Views: 2
  • IMG-20240129-WA0882(1).jpg
    IMG-20240129-WA0882(1).jpg
    821.4 KB · Views: 2
  • IMG-20240129-WA0880(1).jpg
    IMG-20240129-WA0880(1).jpg
    748.3 KB · Views: 2
  • IMG-20240129-WA0878(1).jpg
    IMG-20240129-WA0878(1).jpg
    694.5 KB · Views: 2
  • IMG-20240129-WA0876(1).jpg
    IMG-20240129-WA0876(1).jpg
    622.3 KB · Views: 1
  • IMG-20240129-WA0872(1).jpg
    IMG-20240129-WA0872(1).jpg
    786.2 KB · Views: 1
  • IMG-20240129-WA0870(1).jpg
    IMG-20240129-WA0870(1).jpg
    630.5 KB · Views: 1
Back
Top Bottom