Bunge kusimamisha Shughuli zake zote za kawaida Kuujadili Mgomo wa Madaktari!

Inaonekana issue itajadiliwa jioni maana this morning ''Mtoto wa Mkulima'' anakutana na ma Dr huko DSM.

Ila kuliita Bunge la TZ eti ni tukufu naona ni kuwadhihaki Watanzania

Hata wakipiga kelele vipi hao wabunge mwisho wa siku wenye maamuzi ni serikali,acha pinda aendelee na mazungumzo na hao madaktari kwanza,porojo za wabunge tulishazizoea,hawana jipya wanaongea lakini jambo halifiki mwisho.
 
Inaonekana issue itajadiliwa jioni maana this morning ''Mtoto wa Mkulima'' anakutana na ma Dr huko DSM.

Ila kuliita Bunge la TZ eti ni tukufu naona ni kuwadhihaki Watanzania
Kwa hilo naunga mkono hoja mkuu, utukufu upi wa kuangamiza maisha ya watanzania na kujadili insignificant things?

  • :nerd:
 
Nchi yangu Tanzania...

Siku zote alikuwa wapi anakuja kukubali leo? Yaani baada ya vifo na mateso mengi kwa wagonjwa?

Au ameikubali kwa kuwa hoja imetolewa na Peter Serukamba Lowassa?

Issue sio Lowassa issue ni kuwa Ameona ni busara tu pale maana hata wao wana ndugu wanakufa kama kuku wenye mdondo hivy2 sasa lazima aguswe, tatizo ni uoga wa magamba opale kila mtu anamwogopa aliyemweka juu pale sasa wanashindwa kufanya maamuzi hadi wapewe order
 
Hivi Bunge,wabunge au Jengo ndio tukufu?Nakerwa sana na hili neno la Binge tukufu na Mheshimiwa,sielewi maana yake ni nini,Je wabunge wetu tu ndio waheshimiwa?au ni Madiwani tu nao ndio waheshiwa?na je kweli wabunge wetu ni waheshimiwa?wanaheshimika kwa matendo yepi?Hivi kwa muda wote tangu bunge hili la 10 mkutano wa sita na mpaka leo kikao cha 8 kuna wabunge wangapi wamejivunjia heshima?hivi hata Speaker nae ni mweshimiwa kwa kitendo alichokifanya cha kuendelea kuzima hoja ya Mgomo wa nadaktari?

Kimsingi,nachukia kusikia Bunge Tukufu na Mweshimiwa kwa wabunge wetu hapa TZ
 
Pasco, hebu karekebishe uzi kwanza, halafu mwambie invizibo arekebishe Title as well,
Usisahau kuondoa neno takatifu,
Na usiseme bunge limejadili taarifa, walausiseme tume imefikisha taarifa kwa bunge,....

Sema taarifa ta tume imefikishwa kwa speaker, speaker ameifanyia maamuzi, na kama kuna mbunge hajaridhika na maamuzi hayo, akajinyonge!!!
 
BREAKING NEWS:
Wanaharakati wanaelekea barabara ya Fire na au Salender...inaarifiwa walio tayari wawe maeneo hayo majira ya saa 7 hivi. Chanzo kiaminifu.
 
Wanabodi,

Baada ya vuta nikuvute ya wiki mbili sasa, hatimaye Bunge letu tukufu, leo litasimamisha shughuli zake zote za kawaida na kuijadili hoja ya dharura ya mgomo wa madaktari unaoendelea karibu nchi nzima!.

Mjadala huo, umefuatia Naibu Spika, Mhe. Job Ndugai, kuikubali hoja ya Mbunge wa Kigoma, Mhe. Peter Serukamba, akiwa ni mbunge wa 6 kuomba muongozo spika kwa jambo hilo hilo.

Japo mimi ni miongoni mwa tuliolaani udikiteta wa Job Ndugai, nilipomsikia jana, nakiri Mhe. Job Ndugai is better 100times than madame spika!.

Wanabodi,

Hata hivyo leo asubuhi, bunge lilisitisha shughuli zake zote na kuanza kwa taarifa ya spika kuhusu mgomo wa madaktari na kwa vile bunge limependekeza maamuzi makubwa ya ajabu, Spika amempigia simu rais Jakaya Kikwete na Waziri Mkuu Pinda muda wa usiku wa manane (bila kujali kama viongozi hao wamejipumzikia au la!), na kuwaeleza mapendekezo ya kamati hiyo ya bunge, hivyo I was very right!. Mengine yote yanafuatia kauli hiyo ya Spika!.

Hata hivyo, hoja yangu niliileta na kuiconfirm mimi mwenyewe kufuatia uzoefu wangu wa shughuli za bunge. Kwa vile huu mgomo wa madaktari ni dharura zaidi, kamati ya bunge imekamilisha kazi yake jana usiku nilitegemea hoja ya mgomo ndio ingetangulia na kufuatiwa na hoja ya marekebisho ya katiba, lakini sasa mambo yamekwenda vice versa, mjadala wa marekebisho ya katiba ndio umetangulia, hivyo shughuli badala ya kisimama leo, leo shughuli zinaendelea!. Hivyo nakiri kosa la kulazimisha mgomo wa madaktari kuwa ni dharura kihivyo kwa bunge letu.

Nimekubali makosa, nawaombeni minisamehe sana!.

Mtu mzima akishakiri kosa na kuomba msamaha, sio busara kuendelea kumshutumu, kwani wengine tunajifunza kwa makosa hata mara sabaini fii sabaa!.

Samahanini Sana!.

Na Natanguliza shukrani kwa walionielewa!.

Asanteni na tuendelee na mada nyingine!

Pasco.
 
KWa posti hii ya Pasco, naona ni vema shutuma zikafa, tukendelea na mjadala!!! Pasco viongozi wetu wangekuwa na tabia kama yako ya kuona kosa na kukiri ili mambo yaendelee tungekuwa mbali sana!!

Kuna mambo mengi sana yamesabishia taifa hasara isiyo kifani kwa kiburi cha vingozi wetu weengi tu!! Nadhani sasa serikali imeona jinsi Dr. mponda na wasaidizi wake wasivyo na weledi katika uongozi and so they must go ili muafaka na madaktari uje...
 
sasa limebaki pango la wanyang'anyi, ndio maana wanajipandishia posho hovyo, wanalala bungeni, hawahudurii vikao, wanapitisha sheria kandamizi, wakao kwa maslahi ya kichama zaidi na wanaongoza kwa kula starehe

.
Wakati mijadala inaendelea baazi ya wabunge wa sisiem wako bize ndani ya bunge na YOUPORN.
.
 
Wanabodi,

Baada ya vuta nikuvute ya wiki mbili sasa, hatimaye Bunge letu tukufu, leo litasimamisha shughuli zake zote za kawaida na kuijadili hoja ya dharura ya mgomo wa madaktari unaoendelea karibu nchi nzima!.

Mjadala huo, umefuatia Naibu Spika, Mhe. Job Ndugai, kuikubali hoja ya Mbunge wa Kigoma, Mhe. Peter Serukamba, akiwa ni mbunge wa 6 kuomba muongozo spika kwa jambo hilo hilo.

Japo mimi ni miongoni mwa tuliolaani udikiteta wa Job Ndugai, nilipomsikia jana, nakiri Mhe. Job Ndugai is better 100times than madame spika!.

Update:

Wanabodi,

Hata hivyo leo asubuhi, bunge lilisitisha shughuli zake zote na kuanza kwa taarifa ya spika kuhusu mgomo wa madaktari na kwa vile bunge limependekeza maamuzi makubwa ya ajabu, Spika amempigia simu rais Jakaya Kikwete na Waziri Mkuu Pinda muda wa usiku wa manane (bila kujali kama viongozi hao wamejipumzikia au la!), na kuwaeleza mapendekezo ya kamati hiyo ya bunge, hivyo I was very right!. Mengine yote yanafuatia kauli hiyo ya Spika!.

Hata hivyo, hoja yangu niliileta na kuiconfirm mimi mwenyewe kufuatia uzoefu wangu wa shughuli za bunge. Kwa vile huu mgomo wa madaktari ni dharura zaidi, kamati ya bunge imekamilisha kazi yake jana usiku nilitegemea hoja ya mgomo ndio ingetangulia na kufuatiwa na hoja ya marekebisho ya katiba, lakini sasa mambo yamekwenda vice versa, mjadala wa marekebisho ya katiba ndio umetangulia, hivyo shughuli badala ya kisimama leo, leo shughuli zinaendelea!. Hivyo nakiri kosa la kulazimisha mgomo wa madaktari kuwa ni dharura kihivyo kwa bunge letu.

Nimekubali makosa, nawaombeni minisamehe sana!.

Mtu mzima akishakiri kosa na kuomba msamaha, sio busara kuendelea kumshutumu, kwani wengine tunajifunza kwa makosa hata mara sabaini fii sabaa!.

Samahanini Sana!.

Pasco.

UTAKULA MATAPISHI YAKO! Usituzuge hapa..tunayo michango hasi, matusi, kebehi na mbwe mbwe ulizokuwa ukimwaga hapa!
 
BREAKING NEWS:
Wanaharakati wanaelekea barabara ya Fire na au Salender...inaarifiwa walio tayari wawe maeneo hayo majira ya saa 7 hivi. Chanzo kiaminifu.

Niko taslim hapa... lete data vzuri kwani nasi tunataka tuwe kwenye kumbukumbu ya UKOMBOZI WA TANGANYIKA dhidi ya wanyonyaji na wafilisi(MAGAMBA)
 
hii ni vurugu mechi tupu...sasa nini ndo nini hapa?

Wakati mwingine ni ngumu sana kufuatilia mijadala ya mambo ya maana kama haya, taarifa hazieleweki eleweki halafu zinaandikwa kwa mtindo wa kutuaminisha . You end up being more confussed
 
Mkuu vurugu mechi ipi?.
1. Nlisema bunge litasimama kujadili hoja ya dharura.
2. Bunge likaanza kwa taarifa ya spika kuhusu mgomo wa madaktari bila kujadili
3. Sasa bunge halikusimama kudadili, hili nimeliombea radhi, sasa vuruge mechi ni ipi?.
 
Nipo interiour sana sina TV vipi kuhusu uvumi wa waziri na naibu waziri wa afya kufukuzwa kazi ni za kweli?
 
Mkuu vurugu mechi ipi?.
1. Nlisema bunge litasimama kujadili hoja ya dharura.
2. Bunge likaanza kwa taarifa ya spika kuhusu mgomo wa madaktari bila kujadili
3. Sasa bunge halikusimama kudadili, hili nimeliombea radhi, sasa vuruge mechi ni ipi?.

Vurugu mechi iliyopo kaka yangu Pasco ni kuwa hii si mara yako ya kwanza kutupatia information ambayo ni confirmed only by your experience!Utawekaje kitu as if umepewa taarifa in advance kumbe ni 'foreseeing' yako?Jinsi unavyowaza na kuona muelekeo wa mambo sio lazima iwe ndivyo hivyo mambo yataenda,sasa confirmation inatoka wapi mkubwa?We don't confirm issues by just experience,but experience is an added advantage to predict righty.Kwahiyo ni bora useme kuwa unapredict itakuwa so and so kuliko kutupatia taarifa ambayo kumbe ni prediction yako na bila kusema kuwa ni prediction.Wengi tunakutegemea hapa jukwaani mkubwa wangu lakini kwa siku za karibuni you have been not the same Pasco I used to admire here in JF.
 
Back
Top Bottom