Bulembo: Hatutawaruhusu upinzani kwenda Ikulu

Kwa kweli kauli ya Bulembo imeusikitisha Umma wa Wapenda Amani! How come mtu na akili zako utamke maneno kama yale tena kwa kuweka msisitizo namna ile? Tusimpuuze jamani ile kauli huenda akawa amepandikizwa kutoka mamlaka zake! Atajilaumu sana kama wanalolitaka halitakuwa. Najiuliza tu itakuwaje kama wapiga kura watadai haki yao kwa nguvu endapo watagundua kuwa kuna goli la mkono ?
 
Hawa watu mbona wanakuwa kama wamevulugikiwa, kinini kimewapata? si wasubiri uchaguzi? kwani mtu kwenda ikulu ni hiyari au timu Fulani ya mpira kufungwa huwa ni hiari? Si kwa sababu inakuwa imezidiwa? Wasubiri uchaguzi wanainchi ndio watasema nani ataenda Ikulu kupitia sanduku za kura.

Kuna mambo Bulembo ana uwezo nayo kabisa kama kumwambia mkewe twende chumbani na siyo kumpeleka mtu Ikulu.Waliopo karibu naye wamweleze hili

Ha ha haaaaa
 
Mpuuzi tu huyu! Tuliokuwa karibu na CCM enzi hizo tunamfahamu kiundani! Hana chochote kipya zaidi ya kutingisha wowowo!

Hahahahahahahahaha mkuu, huyo ni mchumia tumbo wa longi, hana lolote ila tumsamehe tu elimu ndo tatizo.........
 
Ishhhhhh yaani ktk mambo ya kuongelea yoooooote tuanze kuongelea vuvuzela kama huyo?
 
Akiongea kwenye kampeni mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi CCM amesema chama hicho hakitawaruhusu wapinzani kwenda IKULU.

NB;Hivi CCM ndo inaruhusu watu kwenda IKULU kauli hii inaashiria kuwa hata kama upinzani utashinda hawatakubali washike madaraka.

Ninaomba wanasiasa wachunge ndimi zao wakati huu wa uchaguzi kwani hata CCM wakishinda wapinzani wataamini kuwa wameibiwa hali itayoleta machafuko na kupelekea mauaji acheni vitisho vyenu maana wanaoamua nani aende ikulu ni wananchi na sio CCM.

Huu ni uchaguzi wa kidemocrasia atakaye chaguliwa na wananchi huyo ndiye atakaenda ikulu,leo hii iweje chama kimoja kitoe kauli za vitisho kuwa hakitaruhusu chama cha upinzani kiende ikulu hata kama kimepewa ridhaa na wananchi?.hizo kauli angekuwa amezitoa Mbatia au Lowasa kesho yake ungesikia kuwa Nape au makamba wameitisha mkutano wa wandishi wa habari kulaani kauli hiyo.
 
Hivi Bulembo ana elimu gani?. Matamshi yake yanaonyesha kuwa shule yake ni ndogo sana.
 
Janja ya nyani hiyo anajaribu kukatisha tamaa raia kuwa hata wachague upinzani hawatatangazwa,uongo kapigeni kura
 
Kauli hii imenistua kidogo. Akihutubia umati wa wananchi waliofika kusikiliza kampeni za chama cha kijani, mwenyekiti huyo wa jumuiya ya wazazi amesema wao watakuwa tayari kufanya yote ispokuwa hawataruhusu mtu kuingia ikulu. Mimi ninavyojua wananchi kupitia kura zao ndio wenye mamlaka ya kuamua nani aende ikulu.

Kimsingi sijaelewa ana maana gani, kwa kuwa kauli hii ni tata. Wataalamu wa methani mjaribu kuidadavua kauli hii.

Source of the quote> ITV Habari

CCM ina watu wa ajabu sana kwenye team yao ya kampeni,Eti akina Bulembo watu ambao ni hamnazo.
USHAURI KWA CCM:
Fukuzeni watu wenye viburi kwenye kampeni wanamuharibia sana Magufuli.Bulembo akafanye kazi nyingine sio kufuatana na Magufuli sio size ya magufuli.
 
Ata mm pia nimeiskia bt sie watu wa kaskazini pia tumejipanga kupambana wacha amani upotee bt lazima tuingia ikulu kwa vovote
 
Aafu nna hasira na wale wanatengeneza Dawa feki wanasimama majukwaani...juzi katoto kangu kamemaliza doz ya quinine hakaponi tumekapa meta kamepona...ngoja ifike 25....tarwhe 1 nafile case ARV fake kwa kuanza
 
Huyo mzee ni kenge tu na hatuwezi kuongozwa na makenge maisha yetu yote na kama kuna mtu anabisha ujue huyo naye ni kenge na huu mwaka itafamika ni bora tuoneshane heshima hawa kenge wamezoea vibaya.
 
Huyo jamaa na timu yake ni hatari ktk harakati za mageuzi. Sioni wepesi wao wakukubali matokeo kama ikulu inaonekana kama ya magamba.
 
Hawa watu mbona wanakuwa kama wamevulugikiwa, kinini kimewapata? si wasubiri uchaguzi? kwani mtu kwenda ikulu ni hiyari au timu Fulani ya mpira kufungwa huwa ni hiari? Si kwa sababu inakuwa imezidiwa? Wasubiri uchaguzi wanainchi ndio watasema nani ataenda Ikulu kupitia sanduku za kura.

Kuna mambo Bulembo ana uwezo nayo kabisa kama kumwambia mkewe twende chumbani na siyo kumpeleka mtu Ikulu.Waliopo karibu naye wamweleze hili

Unajua mara nyingi najiuliza uwezo na uelewa wa sheria wa huyu bwana kwa matamko mengi tata anayotoa kuhusu chama chake. Nitaomba mchangiaji mwenye cv ya huyu mh pamoja na kibajaji aniwekee. Kwa kweli kwa tamko la leo ambalo nami nimelisikia toka taarifa ITV saa mbili usiku huu wanasheria wa nchi hii na hata hao wa the hague kwa kuwa wapo wenyewe hapa nchini na balozi zao zipo wasubiri kwa siku mbili tatu endapo chama chake au mwenyekiti wa tume ya uchaguzi wasipokemea kauli hizi zinazoashiria uchochezi apandishwe kizimbani atupe ufafanuzi unaokidhi. Endapo ukawa watashinda uchaguzi na kutoruhusiwa kuingia ikulu basi tutaamini Bulembo hayakuwa maneno yake bali alitumwa kuwasilisha ujumbe huo.
 
Hii nchi ni wananchi hakuna mtu mwenye hatimiliki na hii nchi viburi na kauli zenye maudhi zitawaponza hata mzee kingunge alishasema uongozi ni dhamana tu.
 
Akiongea kwenye kampeni mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi CCM amesema chama hicho hakitawaruhusu wapinzani kwenda IKULU.

NB;Hivi CCM ndo inaruhusu watu kwenda IKULU kauli hii inaashiria kuwa hata kama upinzani utashinda hawatakubali washike madaraka.

Ninaomba wanasiasa wachunge ndimi zao wakati huu wa uchaguzi kwani hata CCM wakishinda wapinzani wataamini kuwa wameibiwa hali itayoleta machafuko na kupelekea mauaji acheni vitisho vyenu maana wanaoamua nani aende ikulu ni wananchi na sio CCM.

Bulembo pamoja na upoyoyo wake, ana masikio, macho na mdomo.
Alichokisikia ndicho na kukiona ndicho anachoshuhudia,

Anaweza kuwa mjinga wa hoja na hekima, lakini kaona na kusikia mipango na mikakati yote, hata kama kajaliwa kuwa mwepesi kuropoka,
 
Kauli hii imenistua kidogo. Akihutubia umati wa wananchi waliofika kusikiliza kampeni za chama cha kijani, mwenyekiti huyo wa jumuiya ya wazazi amesema wao watakuwa tayari kufanya yote ispokuwa hawataruhusu mtu kuingia ikulu. Mimi ninavyojua wananchi kupitia kura zao ndio wenye mamlaka ya kuamua nani aende ikulu.

Kimsingi sijaelewa ana maana gani, kwa kuwa kauli hii ni tata. Wataalamu wa methani mjaribu kuidadavua kauli hii.

Source of the quote> ITV Habari

Hata me nimemsikia. Ila watambue umma ndo wenye kuhamua.
 
Back
Top Bottom