Boti yalipuka

Itakuwa hako kaboti kalikuwa kabovu lakini kakaachiwa kabebe roho za watu. Wamiliki wabanwe ili iwe fundisho kwa wengine.
 
Itakuwa hako kaboti kalikuwa kabovu lakini kakaachiwa kabebe roho za watu. Wamiliki wabanwe ili iwe fundisho kwa wengine.
nania abanwe? haipo hio tanzania....kesho kikwete anatuma rambi rambi na kutoa ubani wa buku 20 kwa kila mfiwa imetoka tunasahau tunasubiri jingine
 
Hiyo boti ndogo ilikuwa inasafirisha bidhaa bandia usiku huo nyingi ya hizo zina mazoea na bandari bubu ya tegeta vitu vingi sana feki toka nchi za asia vinapitia katika bandari bubu na nyingi vinapatikana katika maduka haswa ya watu wenye asili ya visiwani
 
nania abanwe? Haipo hio tanzania....kesho kikwete anatuma rambi rambi na kutoa ubani wa buku 20 kwa kila mfiwa imetoka tunasahau tunasubiri jingine

mkuu yoyo ulisema utaowa mwaka huu naona umeamua kusogeza mbele umeshatia mimba nini au mambo ya mporomoko wa uchumi duniani
 
Hiyo boti ndogo ilikuwa inasafirisha bidhaa bandia usiku huo nyingi ya hizo zina mazoea na bandari bubu ya tegeta vitu vingi sana feki toka nchi za asia vinapitia katika bandari bubu na nyingi vinapatikana katika maduka haswa ya watu wenye asili ya visiwani

Tupe picha ya usafiri halisi wa pemba! Kunaboti ngapi, nauli yake ni kiasi gani, ratiba zake zikoje. Na aina zingine zinazopatikana ili tuelewe hizo bidhaa bandia na bandari bubu
 
Poleni Wafiwa... Nimejiweka katika nafasi ya Abiria kwa kweli wahanga walikuwa na wakati mgumu sana maana kwenye chombo kuna Moto mkali nje kuna kina kirefu cha bahari... Wengi kwa mujibu wa Kamanda Sirro wamekufa maji... No life jackets,No Fire Extinguishers... Kesho tutasikia mengi...
 
Hiyo boti ndogo ilikuwa inasafirisha bidhaa bandia usiku huo nyingi ya hizo zina mazoea na bandari bubu ya tegeta vitu vingi sana feki toka nchi za asia vinapitia katika bandari bubu na nyingi vinapatikana katika maduka haswa ya watu wenye asili ya visiwani

Inashangaza raia wa kawaida una taarifa nyeti kama hizi, lakini vyombo vyetu vya usalama hata havijui. Watasema hawajaandikiwa barua ya kuchunguza? maana hayo ndiyo majibu yao, au wao wenyewe ni wahusika? Hii ndio nchi yetu bwana!!
Nawapa pole wote walioondokewa na ndugu zao na kama kuna waliopona. R.I.P
 
Huyu Kamanda ni mwongo manake katika maelezo yake anasema kwamba watu 7 wameogelea kutoka sehemu boti ilipoungua hadi wakafika juu na walikuwa hai,, sasa hivi jamani boti inaweza kushindwa na watu ambao waliogelea na kufika wakiwa hai kuliko hilo Boti lao? hawajaenda popote waongo kabisa!! Eti asubuhi wakenda tena ,wanenda kutafuta chaza?
_________________________________________
Date::4/15/2009
Watu 20 wahofiwa kufa baharini baada ya boti kushika moto
Burhani Yakub,Tanga na Salim Said, Dar
ZAIDI ya watu 20 wanasadikiwa kufa maji katikati ya bahari ya Hindi na wengine 13 kuokolewa baada ya boti walilokuwa wakisafiria kutoka Tanga kuelekea Kisiwani Pemba kushika moto.
Kwa mujibu wa habari zilizopatikana na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Nyakoro Sirro, ajali hiyo ilitokea saa 7.00 usiku wa kuamkia jana katikati Bahari ya Hindi wakati.
Taarifa zilizolifikia gazeti hili zinasema boti hiyo ambayo ni mfano wa jahazi ililopata ajali hiyo ni la kubeba mizigo linalojulikana kwa jina la ‘Amana Pemba”, ambayo hufanya safari zake kati ya Pemba ,Unguja, Dar es saalam na Tanga.
Kamanda Siro alisema boti hilo lilikuwa na kibali cha kuondoka katika Bandari ya Tanga saa 11.00 jioni kwenda Pemba, lakini haikuondoka hadi saa 3.30 usiku ndipo ikaanza safari yake ya kuelekea Pemba likiwa na mizigo na abiria 40.
Kamanda Sirro alisema kwa mujibuwa taarifa alizopata, ajali hiyo ilisababishwa na godoro ambalo lilishika moto baada ya kugusa injini na kisha kulipukuka.
Alisema mmoja wa abiria waliokuwa ndani ya boti hiyo aliuona moto huo akapiga kelele na wengine wakaanza kutapatapa huku baadhi yao wakichupa majini ili kujiokoa.

“Abiria mmoja alitupigia simu kututaarifu juu ya tukio hilo na kuomba msaada, ndipo Boti ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) ikaondoka usiku huo kwenda kuwaokoa, lakini ilipofika katikati ilishindwa kuendelea na safari kutokana mawimbi kuwa makubwa hivyo ikarejea Tanga,” alisema Sirro.
Alisema abiria sita kati yao waliokolewa na jahazi lijulikanalo kwa jina la ‘Amana Tanga’ likitokea Pemba kuelekea Tanga ambao waliwasilishwa jijini hapa jana alfajiri na kukimbizwa katika Hospitali ya Mkoa ya Bombo.
Kwa mujibu wa melezo ya Sirro watu wengine saba wakiwamo wafanyakazi wa boti hiyo waliogelea na kufanikiwa kufika pwani katika eneo la Kigombe wakiwa hai.
Alisema jana alfajiri timu ya waokoaji wa kikosi cha wanamaji cha Jeshi la Polisi kutoka Bandari ya Tanga na kikosi cha Zimamoto viliondoka kwa boti kuelekea eneo la tukio kwa ajili ya uokoaji.
Abiria waliookoka katika ajali hiyo wamesema kuwa kuna uwezekano kuwa wenzao wengi wamekufa maji kwa kuwa waliwaacha wakitaptapa na wengine walishindwa kuogelea kutokana na kukosa nguvu.
“Wenzetu wengi tu watakuwa wamekufa. Kama Boti ya uokoaji ya Bandari ya Tanga ingefika usiku ingewakoa lakini kama wameenda asubuhi watakuwa wamechelewa kwani kulikuwa na wanawake na watoto ambao hawakuwa na uwezo wa kuogelea kwa muda mrefu,” alisema mmoja wa abiria hao ambaye alinusurika, Jumaa Idd Jumaa mkazi wa Chake chake, Pemba.
Hata hivyo, Kamanda Sirro aliwaambia waandishi wa habati kuwa atatoa taairfa kamili ya idadi ya abiria walikufa kikosi cha waokoaji kitakaporejea.
Jijini Dar es Salaam Salim Said anaripoti kuwa Kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni, Hamad Rashid ametoa salamu za pole kwa ndugu, jamaa, marafiki na famili za marehemu na walioathirika katika ajali hiyo iliyowaka moto baharini.
Akizungumza na Mwananchi jijini Dar es Salaam jana, Rashid alisema amepata mshtuko baada ya kupata taarifa za ajali hiyo na kwani katika boti hiyo kulikuwa na baba yake mdogo.
 
roho inayokaribia kupoteza nafsi inaujasiri zaidi wa kujiokoa, kuliko iliyonzima, kwani inawoga wa maafa. yawezekana kabisa walijaribu kwenda na mawingu yakawatisha
 
Muhutasari wa Kamanda Ziro.

"Abiria mmoja alitupigia simu kututaarifu juu ya tukio hilo na kuomba msaada, ndipo Boti ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA)ikaondoka usiku huo kwenda kuwaokoa, lakini ilipofika katikati ilishindwa kuendelea na safari kutokana mawimbi kuwa makubwa hivyo ikarejea Tanga,"

Baadae kidogo, Kamanda huyu huyu anaripotiwa wakisema kuwa:
watu wengine saba wakiwamo wafanyakazi wa boti hiyo waliogelea na kufanikiwa kufika pwani katika eneo la Kigombe wakiwa hai.

Hiki ni kioja kikubwa sana! Ni boti gani hiyo inayoshidwa kufika mahala ambabo binadamu anaweza kuvuka kwa kuogelea? Maelezo ya Kamanda huyu yanajaribu kuficha ukweli ambao kwa hakika hauwezi kufichika.
Ni aibu gani hii kusema kuwa jeshi la polisi, Navy na vikosi vyengine vyote wameshindwa kufika eneo la ajali mahali penye umbali wa mtu kuweza kuogelea, ati mawimbi makubwa!!
Anaendelea kupayuka bila aibu kwa kukiri kuwa alishindwa kutekeleza wajibu wake kuanzia wakati alipopata taarifa ya ajali mpaka ikafika asubuhi. Yaonesha hakuweza kukatisha usingizi wake kushughulikia hali ya dharura ya kuokoa roho za binadamu wenzake.
Alisema jana alfajiri timu ya waokoaji wa kikosi cha wanamaji cha Jeshi la Polisi kutoka Bandari ya Tanga na kikosi cha Zimamoto viliondoka kwa boti kuelekea eneo la tukio kwa ajili ya uokoaji.

Kwa nini haikuwezekana kupleka hii timu tokea wakati wa usiku alipopata taarifa za ajali? Nashangaa mtu anasimama kudhihirisha uzembe wake na kushindwa kufanya wajibu wake bila ya aibu. Na nashangaa zaidi kuwa viongozi wa kitaifa na wengineo wote wamekaa kusikiliza habari hizi bila kumrudi na kumuwajibisha.
Ningekuwa Raisi ningewafukizilia mbali na kuwavurumisha jela wote kwa uzembe. zimamoto wanenda asubuhi dah hii kali ya mwaka kama si uzembe wa Sultani CCM hawa wote wangekuwa hawana kazi waliporejea
 
Dadisi zaidi, inawezekana hiyo boti ya uokoaji haina uwezo wa kufanya kazi usiku ama hata dira haina. Kwahiyo lazima walihitaji mwanga wa asili na hisi tu!
 
roho inayokaribia kupoteza nafsi inaujasiri zaidi wa kujiokoa, kuliko iliyonzima, kwani inawoga wa maafa. yawezekana kabisa walijaribu kwenda na mawingu yakawatisha
Sasa hilo jahazi lililowaokoa ,au pale bandarini kuna uajiri wa mtoto wa shangazi na mjomba hawana elimu wala uzoefu ni showing off tu ,kwa inavyotakiwa wawepo watu wenye uzoefu well trainning so far ni wanaojua kunyoosha mkono mwisho wa mwezi kuna tofauti gani na waajiriwa hewa .

Hivi wamekiri kuwa walipokea simu huoni kama hawa watu wamefedheheka kwa kauli zao ,au pia hapo panahitaji tume kujua uzeme wa watu waliopewa dhamana mkuu anasema amepokea simu ila walikwenda na kurudi kutokana na mawimbi makali yaani walishindwa kufanya hata patrol katika kina wanachoweza kuzurura na kupata japo waliojitahidi kuelekea pwani ,hapa pana uzembe tu hakuna lolote ,inaonyesha wazi kuwa waajiriwa hawa ni watu wa kupachikwa tu ,unaweza kulinganisha na wale waajiriwa wa BOT ambao walipatiwa kazi kwa umaarufu wa wazazi wao bila ya kuzingatia taaluma husika ya sehemu wanayofanya kazi ,ndio maana yake ,uchunguzi ufanywe tu

Au kwa vile waliokufa ni WAPEMBA watazunguushwa huku na kule ,kama hakuna uchunguzi tunaliongeza kwenye rekodi hilo mlijue wazi ,tunataka open inquires kwa toka aliepokea simu aidha wafutwe kazi au kushushwa vyeo moja lazima lifanyike haya mambu si ya kuyaachia yapite hivi hivi ,tunaona meli zinazama kwenye Lake victoria ,matreni yamegongana juzi ,nini kimefanywa ? Sasa kama hakuna zinazochukuliwa na kuwa mfano hai nani atawajibika kama si kuzidisha dharau ,this is too much MR KIKWETE.
 
Mkuu badilisha heading pia, sio unaungaunga tu mengine si ya kuunga japo yamefanana ,sasa tupo kwenye ukurasa wa kukandamiza hivyo headingi endane na wakti vilevile.Mkandamize mkuu wa polisi hapo ili ijulikane tunapoelekea. Kulipuka kwa boti kumeshapitwa na wakati sasa tupo kwenye utetezi wa wananchi we have to deal accordingly
 
Last edited:
Dadisi zaidi, inawezekana hiyo boti ya uokoaji haina uwezo wa kufanya kazi usiku ama hata dira haina. Kwahiyo lazima walihitaji mwanga wa asili na hisi tu!
Sasa kama haina uwezo waliendakwa kupapasa huko walikofika baharini na kuliona wimbi ni la size ya mtu anejua kuogelea na kurudi nchi kavu ,wakiwawacha watu wachape mikono. Unajua polisi wakikupiga risasi ya mguu wakikuweka ndani ya gari wanakumaliza kabisa kwa kukuongezea nyingine ili kufuta ushahidi na masuali ila huyu mkuu wa Polisi Amelaniwa na Mwenyezi Mungu inawezekana waliowaona wanaopigania kujiokoa lakini walishindwa kuwavuta kwa sababu walikuwa hawana nyenzo za kuwavutia hivyo wakaona warejee na wale watamalizika mmoja mmoja kwa kuishiwa na nguvu na wote watapoteza maisha ,ole wao mmoja aseme aliiona boti yao na ikiwapita kuwazidi kuwasukumizia mawimbi unauonaje huu mstari ? Japo hakutafanywa lolote.
 
roho inayokaribia kupoteza nafsi inaujasiri zaidi wa kujiokoa, kuliko iliyonzima, kwani inawoga wa maafa. yawezekana kabisa walijaribu kwenda na mawingu yakawatisha
Tunazungumzia trained people hapa hivyo uelewe they are trained for the job ,unafundisha ukomando kwa special job na WaTanzania wamewaweka pale bandarini ikiaminika waweze kutoa suluhisho katika hali kama hizo sasa unasema wanaogopa kufa mbona hawaukatai mshahara ,hivi wanalipwa bure au mpaka bahari iwe shwari ndio sababu zilizotufanya tukakodi meli za kigeni kutulindia mipaka ya baharini wengine wasiibe samaki kwa wajanja watafunga dili huko huko baharini na kulipwa na huku wakirudi wanahakikisha feza ya mkataba inaingia ,ile kesi imeishia wapi tuliona magufuli kifua mbele lakini hatujasikia tena hatima yake baada ya siku mbili ya magazeti ya mafisadi kuandika mashairi ya kuwazuga WaTanzania.
 
Nilishapost humu naona post yangu imeyeyuka!
Anyway nilikua nasema mtu anaweza akaogolea kwenye bahari ambayo boti inashindwa kwenda hasa kama amevaa life jacket.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom