Haioneshi picha nzuri kwa viongozi kunawiri/kunenepeana ilhali raia wakikondeana kwa sababu ya ugumu wa maisha

Burkinabe

JF-Expert Member
Feb 12, 2023
1,893
3,200
Leo wakati namsikiliza Mh. Aikael Freeman Mbowe, amegusia jambo ambalo kwa kweli kwa maoni yangu naona yuko sahihi kwa 100%.

Hii Serikali ukiangalia maisha wanayoishi Viongozi na Raia, utafikiri wanaishi katika nchi 2 tofauti!

Viongozi wengi wa sasa wanazidi kunenepeana huku raia walio wengi wakikonda kwa sababu ya hali ngumu ya maisha.

Hii kwa kweli siyo sawa kabisa! Kwanini kama ni kunawiri tusinawiri wote?! Na kama ni kukonda kwa nini tusikonde wote?!

Hebu chukulia hata kwenye familia, baba anenepeane hovyo, huku mke na watoto wengine wakikondeana! Kwa maoni yangu, hii itakuwa ni dharau na kutokujali kwa baba wa familia. Kwangu, ni vizuri akonde baba, wanawiri watoto na wanafamilia wengine!

Leo Mh. Mbowe kasema Serikali ya sasa inaishi maisha ya anasa sana kutokana na utitiri wa kodi na tozo ambazo hata hatuoni zinafanya nini zaidi ya kutusababishia tu raia wa kawaida maisha kuzidi kuwa magumu, huku viongozi wao wakiishi kama wako PEPONI!

Nimalizie bandiko langu kwa kuiomba Serikali ifanye kila linalowezekana kufanya yafuatayo:
1. Kufanyia kazi ushauri wa Mh. Mbowe
2. Kudhibiti mfumko wa bei
3. Kupunguza bei za nauli kwa daladala na mabasi ya mikoani ibaki ilivyokuwa.
4. Kupunguza matumizi ya Serikali yasiyo ya lazima ikiwemo safari na sherehe zisizo na tija
5. Ajirini vijana maana wengi wako mtaani hawana kazi
6. Imarisheni na kuboresha huduma kwa jamii ikiwemo Afya, elimu, usafiri n.k
7. Wasikilizeni raia na mfanyie kazi malalamiko yao.
 
Leo wakati namsikiliza Mh. Aikael Freeman Mbowe, amegusia jambo ambalo kwa kweli kwa maoni yangu naona yuko sahihi kwa 100%.

Hii serikali ukiangalia maisha wanayoishi Viongozi na Raia, utafikiri wanaishi katika nchi 2 tofauti!

Viongozi wengi wa sasa wanazidi kunenepeana huku raia walio wengi wakikonda kwa sababu ya hali ngumu ya maisha.

Hii kwa kweli siyo sawa kabisa! Kwa nini kama ni kunawiri tusinawiri wote?! Na kama ni kukonda kwa nini tusikonde wote?!

Hebu chukulia hata kwenye familia, baba anenepeane hovyo, huku mke na watoto wengine wakikondeana! Kwa maoni yangu, hii itakuwa ni dharau na kutokujali kwa baba wa familia. Kwangu, ni vizuri akonde baba, wanawiri watoto na wanafamilia wengine!

Leo Mh. Mbowe kasema serikali ya sasa inaishi maisha ya anasa sana kutokana na utitiri wa kodi na tozo ambazo hata hatuoni zinafanya nini zaidi ya kutusababishia tu raia wa kawaida maisha kuzidi kuwa magumu, huku viongozi wao wakiishi kama wako PEPONI!

Nimalizie bandiko langu kwa kuiomba serikali ifanye kila linalowezekana kufanya yafuatayo:
1. Kufanyia kazi ushauri wa Mh. Mbowe
2. Kudhibiti mfumko wa bei
3. Kupunguza bei za nauli kwa daladala na mabasi ya mikoani ibaki ilivyokuwa
4. Kupunguza matumizi ya serikali yasiyo ya lazima ikiwemo safari na sherehe zisizo na tija
5. Ajirini vijana maana wengi wako mtaani hawana kazi
6. Imarisheni na kuboresha huduma kwa jamii ikiwemo Afya, elimu, usafiri n.k
7. Wasikilizeni raia na mfanyie kazi malalamiko yao.
Kosa ni kwa waliopanga foleni kuipigia kura CCM na kwa walimu waliokubali kuhujumu upinzani kipindi cha uchaguzi
 
Back
Top Bottom