GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 56,689
- 109,117
"Nimepigwa na huyu Bondia Golola kwakuwa nimegundua ni Mganga wa Kienyeji, kwani nilikuwa naona mauzauza tupu ulingoni. Leo mnaniletea Mganga wa Kienyeji ipo siku mtaniletea hata majini ili kupigana nami sitaki jamani." Amesema Bondia Mandonga jana baada ya kupigwa kwa KO na Bondia Fundi Moses Golola kutoka nchini Uganda.
GENTAMYCINE huko nyuma (hapa hapa JamiiForums) niliwahi kuonya kuwa hii tabia ya Bondia Mandonga kupigana kila wiki Kinyume na utaratibu, kuna siku ama atapigwa vibaya au hata kufia ulingoni. Kama kawaida Mfalme wa Maono mimi sikueleweka ila taratibu naanza kukiona kwa mbali kile ambacho nilikiona (nilikitabiri) kinaenda kutokea.
Halafu nimejiuliza sana, hivi hawa Waandishi wa Habari wanaopenda kumhoji huyu Bondia muhuni na wa Hovyo Karim Mandonga ni Professionals na wamepita Vyuoni kweli?
Hii kauli yake ya kihuni na isiyo ya Kimchezo ambayo inaweza pia kudhoofisha juhudi za kuuridisha katika kiwango chake Mchezo wa Ndondi ilipaswa kupelekwa hewani au hata tu kupewa kipaumbele kwa Afya ya Mchezo?
Endeleeni tu kumlea hovyo Mandonga huku mkionyesha kupenda kauli zake za uvutaji wa bangi/bange zilizomuathiri ubongo kisha augharimu na mchezo wenyewe.