Nchi ya vichaa hii
Mwigamba mchochezi. na hii mvua nayo , mchochezi ni nani , Mungu?.hapa bado tuna mengi yatatupata hapa dar.GreatThinkers,
Hali ni tete ktk Bonde la Msimbazi daraja la Segerea maji yanapitia Pomoni tokea Pugu na Kinyerezi,Njoo hadi vingunguti hali ni Mbaya sana. Kigogo Polisi wapo kule wanajaribu kuokoa wananchi?
2006/7 kulikuwa na Elnino hayo majumba yaliyopo bonde la msimbazi hayakuwepo mengi kama sasa muulize Mzee Makamba ex-Mkuu wa Mkoa wa Dar.
Tulipata fundisho gani uongozi wa mkoa/taifa ulijifunza, hii mvua iliyokesha inanyesha usiku wa kuamkia leo ni kama tano ktk mia ya Elnino tuliyoshuhudia mwaka ule
Ndg. wana Dar Es Salaam mnaoaminika kunywa maji ya Bendera mnadhani CCeM inathamini tena mtu mlalahoi?
Kama wana nia njema nanyi na hawataki kesho baadhi ya miili ikaokotwe baharini kwa nini wanawaruhusu kujenga?
Je mmewahi kwenda TANESCO kuomba kuunganishiwa huduma mkaambiwa kule ni bondeni hawaweki? Maji Je?
Je serikali inamchoro wowote uliosambazwa kwa wanamitaa jirani na bonde kuwaarifu waishie wapi kujenga makazi hayo yanayoitwa holela?
Mfano. Pale Matumbi ukitokea Buguruni kuna matajiri wameziba bonde kwa Kujaza vifusi na kujenga kuta kubwa na kuweka viwanda serikali iko wapi? au ndiyo Umbwe(vacuum) la Uongozi linalosemwa kwa lipo kwa sasa?
Yangu ni hayo ila maafa yapo.
Bado tatizo lipo.Hili swala toka 2011 tunalipigia kelele lakini hakuna action