Wanaopisha Ujenzi Bonde la Msimbazi Waanza Kulipwa Leo

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Serikali imesema Wananchi 2,400 wanaopisha uendelezaji Bonde la Msimbazi tayari wameanza kulipwa fidia zao leo, hatua hii inakuja baada ya jana Waziri wa TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa kuongea na Wananchi wanaoathiriwa na uendelezaji wa Bonde hilo kwenye eneo la Jangwani jijini Dar es salaaam na kuwapa ahadi kuwa leo wataanza kulipwa.

Amesema fidia hiyo inalipwa kwa Wananchi wote waliokubali kulipwa na kufanyiwa uhakiki wa taarifa zao za kibenki ili kupisha utekelezaji wa mradi huo na tayari Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ameshatoa fedha kwa ajili hiyo “Natambua kabisa wapo Wananchi asilimia 92 kati ya wote wanatakiwa kulipwa fidia wanasubiria fedha zao na sikatai wapo wengine wenye malalamiko Wataalamu wangu endeleeni kuyafanyia kazi na mkishindwa yaje kwangu nione hatua ya kuchukua”

Wananchi wa Mitaa 16 wameanza kulipwa malipo mbalimbali kutokana na thamani ya vitu walivyonavyo ambapo malipo hayo yanajumisha kifuta jasho, usumbufu, mali pamoja na kodi ya nyumba ya miaka mitatu kwa wale waliokuwa na nyumba eneo hilo na wanaishi ili wapate fedha za kulipia kodi ya nyumba kipindi wanaendelea na ujenzi,.

Ofisi ya Rais TAMISEMI inatekeleza mradi huo unaolenga kukabiliana na mafuriko na kuboresha matumizi ya ardhi katika eneo la chini la Bonde kwa ufadhili wa Benki ya Dunia (WB) wa takribani Tsh. bilioni 598 na Tsh. bilioni 60 nyingine zimetolewa na Hispania na Uholanzi.
 
Ona sasa, poor planning inafanya pesa itumike for wrong reasons. Billions of money wasted on compensations, wakati planning ingefanywa miaka hiyo hayo maeneo yangekuwa wazi na serikali ingefanya mambo mengine.

Sijui tunafeli wapi.
 
Ona sasa, poor planning inafanya pesa itumike for wrong reasons. Billions of money wasted on compensations, wakati planning ingefanywa miaka hiyo hayo maeneo yangekuwa wazi na serikali ingefanya mambo mengine.

Sijui tunafeli wapi.
Tuko kutatua kero zaidi sio kuzuia kero zisitokee
 
Kwenda kuishi bonde la msimbazi ni deal nzuri sana.

Kila mvua ikinyesha mavuno.

Hao watu washapewa viwanja Mabwepande miaka ya nyuma, wengi wameviuza tu na awataki kuama.

Kila baada ya miaka kadhaa mvua ikinyesha wanalamba fidia.

Marehemu angewaambia ampati kitu mnayataka wenyewe.

Aiwezekani zaidi ya miaka ishirini ya serikali kujaribu kutoa watu hapo bado wawepo.

Ujinga ni kuwalipa fidia watu wasiosikia.
 
Back
Top Bottom