Intelligence Justice
JF-Expert Member
- Oct 23, 2020
- 3,102
- 3,553
Wakuu wa Jukwaa
Kama mada ilivyo hapo juu, miaka kadhaa iliyopita kwenye awamu ya tano wavamizi wote wa bonde la Msimbazi na Jangwani waliondolewa, nyumba kuvunjwa ikielezwa walikiuka sheria hivyo kusababisha uchafuzi wa mazingira uliokithiri.
Baada ya muda zoezi hilo kufanyika uoto wa asili kama ilivyo kuwa mwaka 1961 ulirejea kwa kasi huku kijani kibichi na unyenyevu mwaka mzima kutamalaki.
Hata hivyo ukipita sasa hivi bonde hilo na Jangwani, uoto wa asili unafyekwa kwa kasi ya ajabu huku shughuli za kibinadamu zikiendeshwa wazi wazi kila mmoja akiona bila hatua zozote kuchukuliwa.
Kilimo cha mboga mboga, mahindi na migomba ndizo zimepamba moto lakini hakuna mtu yeyote mwenye mamlaka anayeona na kuchukua hatua.
Je, walioondolewa mwanzoni na wengine kupewa maeneo huko Mabwe-pande walionewa kuondoshwa an kwamba uharibifu wa mazingira katika bonde hilo kwa sasa ni ruksa?