Bonde la Msimbazi na Jangwani Kilimo na Vibanda Vyarejea Kwa Kasi - Uchafuzi Mazingira Hatarini Tena!

Intelligence Justice

JF-Expert Member
Oct 23, 2020
3,081
3,525
Wakuu wa Jukwaa

Kama mada ilivyo hapo juu, miaka kadhaa iliyopita kwenye awamu ya tano wavamizi wote wa bonde la Msimbazi na Jangwani waliondolewa, nyumba kuvunjwa ikielezwa walikiuka sheria hivyo kusababisha uchafuzi wa mazingira uliokithiri.

Baada ya muda zoezi hilo kufanyika uoto wa asili kama ilivyo kuwa mwaka 1961 ulirejea kwa kasi huku kijani kibichi na unyenyevu mwaka mzima kutamalaki.

Hata hivyo ukipita sasa hivi bonde hilo na Jangwani, uoto wa asili unafyekwa kwa kasi ya ajabu huku shughuli za kibinadamu zikiendeshwa wazi wazi kila mmoja akiona bila hatua zozote kuchukuliwa.

Kilimo cha mboga mboga, mahindi na migomba ndizo zimepamba moto lakini hakuna mtu yeyote mwenye mamlaka anayeona na kuchukua hatua.

Je, walioondolewa mwanzoni na wengine kupewa maeneo huko Mabwe-pande walionewa kuondoshwa an kwamba uharibifu wa mazingira katika bonde hilo kwa sasa ni ruksa?
 
Huwa nashangaa kwa nini serikali inawalea sana hawa wa mabondeni. Si bonde la Msimbazi tu ila mabonde yote wanatakiwa kutolewa ili outo wa asili urudi na maji yapite vizuri, ndo maana marufiko huwa hayaishi.
 
Wakiondolewa pia kuna watu wataleta thd hapa eti wanyonge wanaonewa,wananyanyaswa kwenye nchi yao!
 
Mvua za masika zikianza wataondoka wenyewe Ila Kwa kipindi hiki cha kiangazi huwezi kuwatoa HAO jamaa ni wabishi hatari.

Eneo la jangwani Hadi kigogo sambusa watu wanachimba mchanga na serikali wapo kimya Tu
Serikali ndio imeruhusu ili kina cha mito kiongezeke
 
Ukila ukashiba huwezi kumthamini mwenye njaa.

Ungekuwa mmojawao sidhani kama ungeleta hii mada.

God have a mercy.
 
Wakuu wa Jukwaa

Kama mada ilivyo hapo juu, miaka kadhaa iliyopita kwenye awamu ya tano wavamizi wote wa bonde la Msimbazi na Jangwani waliondolewa, nyumba kuvunjwa ikielezwa walikiuka sheria hivyo kusababisha uchafuzi wa mazingira uliokithiri.

Baada ya muda zoezi hilo kufanyika uoto wa asili kama ilivyo kuwa mwaka 1961 ulirejea kwa kasi huku kijani kibichi na unyenyevu mwaka mzima kutamalaki.

Hata hivyo ukipita sasa hivi bonde hilo na Jangwani, uoto wa asili unafyekwa kwa kasi ya ajabu huku shughuli za kibinadamu zikiendeshwa wazi wazi kila mmoja akiona bila hatua zozote kuchukuliwa.

Kilimo cha mboga mboga, mahindi na migomba ndizo zimepamba moto lakini hakuna mtu yeyote mwenye mamlaka anayeona na kuchukua hatua.

Je, walioondolewa mwanzoni na wengine kupewa maeneo huko Mabwe-pande walionewa kuondoshwa an kwamba uharibifu wa mazingira katika bonde hilo kwa sasa ni ruksa?
WAPIGA KURA WETU HAO WASIBUGUDHIWE KABISA
 
Ikiwa wanalima bostani za migomba ,sioni tatizo kwani ni mimea muhimu kwa chakula kwa wananchi na ni chanzo cha ajira.

Kama wanaweka majengo kwenye hilo bonde msimbazi sikubaliani nao ,kwani ni hatarishi.
 
Mvua za masika zikianza wataondoka wenyewe Ila Kwa kipindi hiki cha kiangazi huwezi kuwatoa HAO jamaa ni wabishi hatari.

Eneo la jangwani Hadi kigogo sambusa watu wanachimba mchanga na serikali wapo kimya Tu
Serikali imewahurusu wachimbe mchanga pale Jangwani ili iwasaidie kuupanua ule mto.

#RudiNyumbaniKumenoga
 
Wakuu wa Jukwaa

Kama mada ilivyo hapo juu, miaka kadhaa iliyopita kwenye awamu ya tano wavamizi wote wa bonde la Msimbazi na Jangwani waliondolewa, nyumba kuvunjwa ikielezwa walikiuka sheria hivyo kusababisha uchafuzi wa mazingira uliokithiri.

Baada ya muda zoezi hilo kufanyika uoto wa asili kama ilivyo kuwa mwaka 1961 ulirejea kwa kasi huku kijani kibichi na unyenyevu mwaka mzima kutamalaki.

Hata hivyo ukipita sasa hivi bonde hilo na Jangwani, uoto wa asili unafyekwa kwa kasi ya ajabu huku shughuli za kibinadamu zikiendeshwa wazi wazi kila mmoja akiona bila hatua zozote kuchukuliwa.

Kilimo cha mboga mboga, mahindi na migomba ndizo zimepamba moto lakini hakuna mtu yeyote mwenye mamlaka anayeona na kuchukua hatua.

Je, walioondolewa mwanzoni na wengine kupewa maeneo huko Mabwe-pande walionewa kuondoshwa an kwamba uharibifu wa mazingira katika bonde hilo kwa sasa ni ruksa?
Ni bora waendelee na bustani kuliko kuacha machaka ya kuficha vibaka
 
Back
Top Bottom