Bomoa Bomoa Yatua Pasua, Moshi

Kimetah

JF-Expert Member
May 8, 2013
1,049
188
Taharuki,vilio na majonzi vimehamia manispaa ya moshi,mtaa wa PASUA baada ya kukuta nyumba zao zimewekwa alama ya X na maneno ONDOA na BOMOA.
Zaidi ya wakazi mi2 waliojenga katika eneo lililopimwa na serikal mwaka 2005,wamevamiwa na watu wasiojulikana kwa kuandika kwny ukuta wa nyumba zao maneno ONDOA na BOMOA kisha kuweka alama ya X na kutoa notisi ya siku 30 za kubomoa nyumba,notisi hiyo inaonyesha imetoka kwny kampuni hodhi ya rasilimali za reli (RAHACO).

Historia ya eneo hilo.
Eneo hilo lilitwaliwa na manispaa ya moshi toka kampuni ya reli kwa utaratibu wote wa kiserikali,kisha manispaa ya moshi ikapima na kuwagaiya wananchi na kuwakabidhi hati ya ardhi na masharti ya kuyaendeleza maeneo hayo.Wananchi walifata mashart hayo ikiwa ni pamoja na kujenga kwa kuwa na ramani iliyothibitishwa na manispaa pamoja na building permit.

Uthibitisho wa makazi halali.
Wananchi hao wameonyesha hati ya kumiliki eneo hilo,barua ya ofa,risiti za malipo,ramani ya nyumba na barua ya kuruhusiwa kujenga.

Wananchi wanahoji.
1.Kwa nini wavamiwe kwny nyumba zao na kuambiwa wabomoe,wakati wamefata sheria za kupata eneo na kuliendeleza?
2.Kwa nini manispaa haijahusika katika kutupa hiyo notisi wakat wao ndio wamehusika katika kutukabidhi maeneo.
3.Mgongano kati ya kampuni hodhi ya reli na manispaa unatokana na nini wakati ni nchi moja?
4.Hao kampuni hodhi ya reli haioni jinsi mtaa ulivyopangiliwa kwa vigezo vyot na nyumba zilivyojengwa?

Wananchi Wanaomba.
1.Wasivunjiwe kwani ni wamilik halali wa eneo husika
2.Waziri wa Ardhi Mh.Lukuvi tunaomba aje katika eneo la tukio ili ajionee dhuluma inayopangwa kisha atoe tamko.
3.Mkuu wa mkoa na wilaya njooni eneo la tukio kushuhudia,msisubiri taarifa ofisini.
 
Naona mungu wao ndo anawafanya akili zao kuruka na kujichanganya wafanye lipi mungu wao afurahi
 
Naamini na WW Ni miongoni WA waathirika nikupe pole Tu kwa sababu nchi yetu inajengwa na ramani ya mkoloni eneo walilopiga x manispaa inasema Ni eneo la reli na waliouziwa wametapeliwa sabab manispaa haimilik reli kwa ushauri wangu Anza kungoa mabati na tofali moja baada ya nyingine unitafute nitakuungisha waswahili wanasema kufa kufahana
 
Hakuna kuilaumu serikali, tatizo ni rahco kuto toa mawasiliano kwa, ofisi ya mkuu wa mkoa, mkurugenzi wa mji wa Mosh,
 
Mwaka 1993maeneo hayo ya Pasua wananchi waliondolewa kwa kuwa inajulikana ni eneo la reli lakini watu walianza kurudi kinyemela na wengine wajanja waliuza maeneo hayo baada ya kuona ramani ya reli. Baadhi ya watu wa manispaa wasiowaaminifu walibadirisha matumizi ya eneo hilo na kuruhusu watu wajenge bila kuwasiliana na kuelewana na reli ambao muda wote toka miaka hiyo ni wamiliki wa eneo hilo. Ushauri wote mliowekewa X ondokeni wenyewe ama sivyo mtakuja juta baadae
 
Watanzania bado wanaishi kwa mazoea enzi hizi
 
Taharuki,vilio na majonzi vimehamia manispaa ya moshi,mtaa wa PASUA baada ya kukuta nyumba zao zimewekwa alama ya X na maneno ONDOA na BOMOA.
Zaidi ya wakazi mi2 waliojenga katika eneo lililopimwa na serikal mwaka 2005,wamevamiwa na watu wasiojulikana kwa kuandika kwny ukuta wa nyumba zao maneno ONDOA na BOMOA kisha kuweka alama ya X na kutoa notisi ya siku 30 za kubomoa nyumba,notisi hiyo inaonyesha imetoka kwny kampuni hodhi ya rasilimali za reli(RAHACO)).

Historia ya eneo hilo.
Eneo hilo lilitwaliwa na manispaa ya moshi toka kampuni ya reli kwa utaratibu wote wa kiserikali,kisha manispaa ya moshi ikapima na kuwagaiya wananchi na kuwakabidhi hati ya ardhi na masharti ya kuyaendeleza maeneo hayo.Wananchi walifata mashart hayo ikiwa ni pamoja na kujenga kwa kuwa na ramani iliyothibitishwa na manispaa pamoja na building permit.

Uthibitisho wa makazi halali.
Wananchi hao wameonyesha hati ya kumiliki eneo hilo,barua ya ofa,risiti za malipo,ramani ya nyumba na barua ya kuruhusiwa kujenga.

Wananchi wanahoji.
1.Kwa nini wavamiwe kwny nyumba zao na kuambiwa wabomoe,wakati wamefata sheria za kupata eneo na kuliendeleza?

2.Kwa nini manispaa haijahusika katika kutupa hiyo notisi wakat wao ndio wamehusika katika kutukabidhi maeneo.
3.Mgongano kati ya kampuni hodhi ya reli na manispaa unatokana na nini wakati ni nchi moja?
4.Hao kampuni hodhi ya reli haioni jinsi mtaa ulivyopangiliwa kwa vigezo vyot na nyumba zilivyojengwa?

Wananchi Wanaomba.
1.Wasivunjiwe kwani ni wamilik halali wa eneo husika
2.Waziri wa Ardhi Mh.Lukuvi tunaomba aje katika eneo la tukio ili ajionee dhuluma inayopangwa kisha atoe tamko.
3.Mkuu wa mkoa na wilaya njooni eneo la tukio kushuhudia,msisubiri taarifa ofisini.
maeneo yote ya reli reli haijayatoa kwa wananchi ila waliazimwa kwa shughuli za muda mfupi pale walipoona wanahitaji.wananchi wengi wamerubuniwa kwa kuwa maafisa ardhi wengi halmashauri walikuwa wanakula na watu wa ardhi wizarani na kuwapa hati za magumashi.
hawakuongea na reli ambaye ni mmiliki wa eneo na km waliongea waliongea kirafiki kila mtu akachukua chake.

nasaha kwa wenye pesa zao nunueni maeneo yasiyo na migogoro hasa maeneo ambayo huna uhakika na mikataba ya awali yakimbieni bora uende nje ya mji
 
Ndio maana Waindi na Waarabu wengi hawana mzuka wa kujenga apa Tanzania. Wao wanaishi kwenye kupanga miaka yote. Pesa yao ni kwenye biashara bora akae na pesa taslimu, kikinuka katika nchi anasepa zake.
Na kama akinunua kiwanja Lazima kiwe na Hati za kueleweka na kimepimwa
 
Kwa hili eneo nyumba zikishavunjwa miaka ya 90s likakaa wazi kwa zaidi ya miaka 20 miaka ya juzi hapo ndo palipimwa na

watu wakauziwa na kila kitu kilichohitajika kilitolewa na halmashauri sababu eneo hili inadaiwa kuwa ilikua ipite reli ya

kuunganisha mitaa ya viwanda na reli iendayo Tanga/Dar lakini imeshindikana kujengwa hiyo reli tangu enzi ya mkoloni

hadi wakati huu ambapo wala haina mashiko tena ndo wamekuja kuweka X ingawa kuna wengine ni ubishi wao coz

walijenga ndani ya mita 35 za eneo la reli ambayo ipo (ingawa imekufa) hao inaweza kuwa sawa wakivunjiwa sabab waliikuta reli.
 
Back
Top Bottom