Kwanza kabisa 1% ya $1.2 bil ni $12m siyo $1.2m. Kwa hiyo 12x20 ni $240mWanabodi, kwa hisani ya mwana jf mwenzetu,
Nimefanikiwa kutembelea huko na kuiona sura ya masharti ya kukopa kutoka Exim Bank ya Uchina, japo mimi sio mtaalam wa uchumi, ila there is something fishy!.
Unapewa mkopo mkubwa mnene wa masharti nafuu ya ajabu with grace period ya miaka 20 ndipo uanze kulipa tena kwa riba ndogo ajabu ya asilimia 1% tuu kwa mwaka!.
Niliposoma masharti ya awali, nikakuta mfano huu mkopo wetu wa Dola bilioni 1.2 utaanza kulipwa mwaka 2032!, ila katika hii miaka 20 ya grace period, kila mwaka tunatakiwa kulipa ile interest ya 1% ya dola bilioni 1.2 ni dola milioni 1.2 kwa mwaka!. Kwa ile miaka 20 tuu ya grace period, tutakuwa tumelipa riba ya dola milioni 24!. Hapo ndio kwanza bado hatujaanza kulipa ile principal ya mkopo huo!.
Wachumi na wana mahesabu hebu angalieni hii kitu na mtusaidie kutufafanulia siye tusio wachumi and correct me if I'm wrong!, kumbe hicho kinachodaiwa kuitwa ni grace period ya miaka 20 huku tukilipa interest, sio grace period lolote, sii chochote kwa sababu tunailipia interest kila mwaka!.
My Take:
Lengo sio kuibeza serikali tena mimi ni miongoni mwa wale ma supporter gesi ije Dar!, bali tunahitaji tuu uwazi Jee this time kwenye mkataba wa bomba la gesi, tumeingia mkataba wa aina gani?. Tutaulipa kwa miaka mingapi?, Ukipiga thamani ya mkopo ambao ni dola bilioni 1.2, kwa interest ya asilimia 1% kuanzia mwaka 2032, jee tutalipa deni kwa miaka mingapi?. Jee jumla tutakuwa tumelipa kiasi gani?!.
Tunaelezwa uchumi wa gesi ni uchumi mkubwa, kama ni uchumi mkubwa then tunaweza kulipa deni lote la US $ 1.2 ndani ya miaka 5 tuu ya uchumi wa gesi, hivyo interest itakuwa low, kwa Wachina hawa watulazimishe tusubiri hadi miaka 20 ipite, lakini katika miaka 20 hiyo wanatulipisha interest kila mwaka?.
Paskali
Update.
Nimepata majibu ya baadhi ya maswali yangu na kujiridhisha hizi concession loans toka Exim Bank of China are the best