Bodi ya mikopo wamekiuka mikataba yetu!

KIDUNDULIMA

JF-Expert Member
Aug 18, 2010
966
538
wameanza kukata 8% tofauti na makubalianop ya awali ya kurejesha kwa kipindi cha miaka kumi. Mi kwa mfano baada ya kuanza kazi walianza kunikata sh. 17,000 kwa mwezi ili baada ya miaka kumi niwe nimemaliza deni lao lote. Nikiwa nimelipia deni kwa miaka mitatu ghafla kwenye mshahara wangu wameanza kukata sh. 250,000 kwa mwezi jamani mabadiliko haya yameniathiri sana kiuchumi maana sikujiandaa kwa hilo.

kwa wana sheria nisaidieni. naweza kuweka injunction ya mahakama kuzuia makato haya mpaka tutakaposeattle mkataba wangu na board?
 
What? sh.250,000.00 kwa mwezi? bila taarifa? hakyanani hii bodi sijui kama huwa wanafikiria kabla ya kutenda.

Hata benki ukienda kuomba mkopo kabla hujakopeshwa wanaangalia na kiwango cha mshahara wako kwanza ili baada ya makato ubakiwe na kiasi cha kutosha kumudu maisha. Sasa hawa loan board kwa staili hii wasishangae wanufaika wa mikopo kuendelea kujificha kwa kuhofia haya makato yasiyozingatia mkataba wa mkopaji.
 
ss hivi jamaa wanakata 10% ya mshahara wako kabla ya makato,b4 walikua wanakata 8%ya net paid baada ya makato ndo maana imependa kwa kasi ila hata hivyo ni nyingi sana 10% ya hiyo laki tatu si hiyo may be atakua amepigwa na penati
 
Bodi ya Mikopo wameanza kuwa wakali kudai pale Serikali ilipokiri kuwa haina fedha.
Bodi ya mikopo imewaweka hata waliomaliza mwaka jana kwenye kundi la wadaiwa Sugu.
Baadhi ya watu pia wamewekwa kwenye kundi la wadaiwa sugu ilhali bado hawajamaliza vyuo..
Kwa kifupi watendaji wa Bodi ya mikopo wanakurupuka kufanya maamuzi badala ya ku act kisomi..
 
Wakinikata hela nyingi nje ya makubaliano naacha kazi kabisa,nikiajiriwa sehemu nyingine ndio nanegotiate mshaara mpya including deni lao ila kwa huu mshaara wakate tena bodi khaaa bora nirudi kijijini nikaendelee kukata mkaa tuone itakuaje kama mbwai mbwai.
 
Ni kweli huu utaratibu wa Bodi wa kukata 8% umevuruga kila kitu. Mimi mwenyewe nilianza kuwalipa toka mwaka 2007 mara baada ya kugadruate 2006. Lkn ghafla mwaka huu wameanza kunikata 8% badala ya 22,000/= waliyokuwa wanakata kila mwezi na kwasasa wananikata zaidi ya 150,000/= kwa mwezi. Kwa kweli huu ni unyanyasaji mkubwa, kwani mimi mkataba nilioingia nao ni wa kukatwa 22,000/= kwa miaka 10 toka 2007 lkn si huu wa 8% kwani hakujawahi kuwa na makubaliano hayo mapya na bodi ya mikopo. Na mbaya zaidi kwasasa nimesafiri nje ya nchi, hivyo nashindwa kufuatilia na kujua kulikoni?

Kwa hakika hii hali imetuathiri sana.
 
Back
Top Bottom