Je, hiki kinachofanywa na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu kuanza tena kuwakata makato wale wanaufaika ambao tayari walishamaliza marejesho?

Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
28,394
81,877
Ninaomba tu kufahamau kama hiki kitendo kinachofanywa na hii Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HELSB), kama ni sahihi au la. Binafsi naona kama ni kitendo cha kihuni.

Maana mwezi uliopita kuna kundi kubwa la wahitimu wa vyuo vikuu walioko kwenye utumishi wa umma, na ambao kimsingi walishakatwa kwa miaka mingi deni la hii Bodi na kumaliza; wameanza tena kukatwa na hii upya kwa kisingizio cha retention fees, na bla bla nyingine!

Yaani watu wamebambikiwa madeni kwa sababu tu hawakuchukua cheti cha kumaliza hayo makato!

Hivi inawezekana kweli taasisi ikukopeshe pesa, baadaye ikuwekee deni kwenye salary slip na kuanza kukukata mpaka deni linaisha! Halafu baada ya miaka 5, taasisi hiyo hiyo inaanza kukukata tena deni lile lile, huku kukiwa hakuna maelezo ya kujitosheleza!

Natoa rai kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na pia Waziri mwenye dhamana waingilie kati jambo hili. Maana wanachofanyiwa wafanyakazi wa nchi hii na hii Bodi ya Mikopo, kwa mtazamo wangu ni uonevu. Na kitachangia sana kuendelea kurudisha nyuma morali ya kufanya kazi.

Watu wa sheria pia wangeingilia kati jambo hili! Usawa huu mfanyakazi ana majukumu lukuki ya kifamilia, halafu unakuja kumkata tena makato upya, na wakati ulishamkata huko nyuma kwa miaka mingi, mpaka deni lake likaisha.

Moderator, naomba uniandikie hapo mwishoni kwenye kichwa cha hii mada yangu, haya maneno matatu; yao, ni sahihi?
 
Mawakili Wasomi na wadau wote wa Elimu, mawazo na ushauri wenu ni muhimu sana kwenye huu uzi. Maana unagusa maslahi ya msingi ya mnufaika. Je, ni sahihi?

Let us say, imekuandikia deni inalokudai kwenye salary slip! Mfano milioni 7+. Ukakatwa mpaka deni likaisha. Ukiwa huna hili wala lile, baada ya miaka mitano mbele, makato yanaanza tena!

Unaenda kuwauliza, wanakuambia deni lilikuwa bado halijaisha! Kwa hiyo unatakiwa ukatwe tena kiasi hiki, halafu ukimaliza ndipo uje uchukue certificate ya kumaliza deni na kuipeleka kwa Afisa utumishi, ili makato yasitishwe!

Je, ni sahihi wanufaika kufanyiwa hivi na hii Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu?
 
Hapa hutopata Msaada labda ungeanzisha mada ya kuponda ccm 😁😁

Hata Mimi nitamaliza deni kabla ya mei ila kama Kuna huo ushenzi wakome kabisa hao kenge wa Bodi.
Potelea mbali mkuu. Muhimu ujumbe umefika. Mwezi uliopita kuna watu kibao wameanza kukatwa upya, na wakati walishamaliza deni miaka kadhaa iliyopita. Ukiwauliza wanaleta bla bla, na makato yanaendelea!

Jambo hili halikubaliki hata kidogo
 
Mawakili Wasomi na wadau wote wa Elimu, mawazo na ushauri wenu ni muhimu sana kwenye huu uzi. Maana unagusa maslahi ya msingi ya mnufaika. Je, ni sahihi?

Let us say, imekuandikia deni inalokudai kwenye salary slip! Mfano milioni 7+. Ukakatwa mpaka deni likaisha. Ukiwa huna hili wala lile, baada ya miaka mitano mbele, makato yanaanza tena!

Unaenda kuwauliza, wanakuambia deni lilikuwa bado halijaisha! Kwa hiyo unatakiwa ukatwe tena kiasi hiki, halafu ukimaliza ndipo uje uchukue certificate ya kumaliza deni na kuipeleka kwa Afisa utumishi, ili makato yasitishwe!

Je, ni sahihi wanufaika kufanyiwa hivi na hii Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu?
Hili nalo wakalitazame upya
 
Hili nalo wakalitazame upya
Bodi ya Mikopo ya wanafunzi wa Elimu ya Juu ina madhaifu mengi sana. Kuna wakati unaweza kufikiri labda kuna Bodi za Mikopo mbili!

Kuna watu walisoma enzi za ada ya chuo kwa mwaka ni laki 6 kwenye baadhi ya course, huku boom likiwa ni 2500 kwa siku! Lakini cha kushangaza mnufaika anakatwa deni alilowekewa kwenye salary slip, baadaye ukiwauliza statement ya deni lako, unaletewa hesabu tofauti kabisa na ile ya kwenye salary slip!
 
Mkuu kuna kipindi walipita kwenye mikoa kikanda kuhakiki madeni na wenye changamoto mbalimbali..ulienda? Kama vipi nenda kwenye ofisi zao zilizo karibu utasaidika..
 
Bodi ya Mikopo ya wanafunzi wa Elimu ya Juu ina madhaifu mengi sana. Kuna wakati unaweza kufikiri labda kuna Bodi za Mikopo mbili!

Kuna watu walisoma enzi za ada ya chuo kwa mwaka ni laki 6 kwenye baadhi ya course, huku boom likiwa ni 2500 kwa siku! Lakini cha kushangaza mnufaika anakatwa deni alilowekewa kwenye salary slip, baadaye ukiwauliza statement ya deni lako, unaletewa hesabu tofauti kabisa na ile ya kwenye salary slip!
Hili nalo ni tatizo, binafsi baada ya kumalizana nao niliwafuata wakanipa certificate ya kumaliza deni na mpaka sasa hawajanisumbua.
Wakati mwingine lile deni wanalokuandikia kwenye salary slip na deni halisi wanalo kudai unakuta ni tofauti.

Mfano kwenye salary slip deni linaweza soma 8,760,000/= ukalipa lote ila ukienda kwao ukakuta deni lako lilikuwa 10,000,000/=.

Ukienda ofisini kwao huwa kuna vitu vingine vingi unakuta wemekuwekea kama deni mpaka unabaki hauelewi elewi.

Hili la mtu kumaliza deni lake then baada ya miaka 5 linazaliwa lingine kwa kweli inafikirisha ila ninaamini watalifanyia kazi.

Pia watu ambao hawajamaliza deni lao ni vema waende kuomba statement ya "Outstanding loan" ili ujue deni lako halisia kuliko kutegemea hilo lililoko kwenye salary slip.
 
Naomba kurudia kuuliza tena; Bodi ya Mikopo wanatenda haki kurejesha makato upya kwa wanufaika ambai walishamaliza makato waliyowekewa kwenye salary slip zao?

Yaani deni liliisha miaka 5 iliyopita, halafu leo wanaanza kukukata upya kwa visingizio visivyo eleweka?

Rais Samia uko wapi? Waziri mwenye dhamana uko wapi? Huu ni uonevu wa wazi kabisa! Na huenda ukazidi kuondoa morali ya kufanya kazi kwa watumishi wengi wa umma.

Usawa huu kuanza tena kukatana 15% kwenye basic salary! Hii nchi mbona ni pasua kichwa sana? Yaani kila mtu ni kambale.
 
Hili nalo ni tatizo, binafsi baada ya kumalizana nao niliwafuata wakanipa certificate ya kumaliza deni na mpaka sasa hawajanisumbua.
Wakati mwingine lile deni wanalokuandikia kwenye salary slip na deni halisi wanalo kudai unakuta ni tofauti.

Mfano kwenye salary slip deni linaweza soma 8,760,000/= ukalipa lote ila ukienda kwao ukakuta deni lako lilikuwa 10,000,000/=.

Ukienda ofisini kwao huwa kuna vitu vingine vingi unakuta wemekuwekea kama deni mpaka unabaki hauelewi elewi.

Hili la mtu kumaliza deni lake then baada ya miaka 5 linazaliwa lingine kwa kweli inafikirisha ila ninaamini watalifanyia kazi.

Pia watu ambao hawajamaliza deni lao ni vema waende kuomba statement ya "Outstanding loan" ili ujue deni lako halisia kuliko kutegemea hilo lililoko kwenye salary slip.
Mimi nililipa Pesa ya Research mwaka watatu ambayo wao hakuniingizia hila nilishamaliza Deni Leo
 
Back
Top Bottom