Bodi ya mikopo kama hamkuwa na budget ya kutosha bora msingeongeza bumu au kuwapa mikopo diploma

hermanthegreat

JF-Expert Member
Mar 2, 2021
858
2,046
Ni vilio tu huku, yaani waliopata angalau asimilia 2% ya Ada yao ni wale yatima au walemavu, ila wengine ni bumu tu.

Hii imekatisha sana tamaa ya wanafunzi kuendelea na elimu ya juu kwani wengi wanaopitia advance wanakuwa na hali ngumu za kimaisha.

Sifa tu kwamba wamewapa mkopo diploma afu kumbe hakuna kuwalipia degree Ada, huku wakijidai wameongezea boom huo ni unafiki.

HESLB mjitathini.

IMG-20231020-WA0061.jpg
 
Roho mbaya haijengi mkuu..hao diploma wamekwambia wanataka kwenda kusoma degree..keki ya Taifa kuleni wote
Miaka mingine walikuwa hawapewi mbona walikuwa wanaenda kusoma, afu shida sio diploma kupewa, ni njia waliyotumia yaani wamepunguza huku wakaweka huko, inshort wamefosi tu
 
nakumbuka nli kosa huu mkopo nka soma bila boom wala ada ayo maisha ya chuo una yajua buda.

Halafu leo niki ona mtu ana lalamika na ana boom namuonaje sijui while mkifika chuo ni bata tu
 
Una uhakika gani mkuu
Mara nyingi ndivyo inavyokuwa japo kila siku si ijumaa , Wanafunzi wa mwaka wa tatu sasa mwaka wao wa kwanza walipewa 20% mwaka wa pili wakaongezewa mpaka 100% .Wa mwaka wa 2 sasa nao wameongezewa mwishoni wa semester ya kwanza sasa hivi karibia wote wana 100% japo wakati wanaingia chuo waliingia Kinyonga.
 
Back
Top Bottom