kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 12,319
- 12,622
Saa nyingine utawasikia wakisema kwenye kipindi chao cha usiku wa manane "leo washindi 30 usiku huu watajishindia kila mmoja sh. milioni 5, bodaboda 1, TV screen ya nchi 40 na jezi pair 2 kwa kila mmoja". Hii ni baada ya kutoa ahadi kama hiihii kwenye vipindi vyao vingine kama vile vya sports saa 3 usiku, Countdown, nk.
Najiuliza maswali mwenyewe kuwa ni kweli wako wanaozipata hizo hela na badaboda, au ni mchongo unachezwa kati ya Redio na watu wanaojifanya wameshinda na kupewa zawadi hizo? Je, Bodi ya michezo ya kubahatisha inawalinda wacheza kamali hizi na kuona kweli haki inatendeka?
Hivi kweli ni kweli usiku wa manane kwenye kipindi kimoja mchongopesa inaweza kutoa 5,000,000 x 30, bodaboda 30, TV 30 na jezi 60? Je, kwa siku moja Redio ina vipindi vingapi na kila kipindi kuna washindi wangapi na kwasiku nzima Redio inatoa kiasi gani cha pesa, bodaboda, TV na Jezz?
Hakuna wizi kwa wananchi hapo kwa njia ya ulaghai?