BISHOP KAKOBE::Tanganyika Huru Lazima Ipatikane

Kakobe ni bora aendelee hivyo hivyo kuwa mpiga kura kutokana na hisia zake lakini asiwabague wafuasi wake wanaotaka serikali mbili,au tuseme kakobe hana wafuasi wa CCM

Kama mchungaji ana wajibu wa kuwapa maarifa ya kiMungu waumini wake. Na ameweza kuwaonesha leo kuwa mpango wa Mungu ni kurudi kwa Tanganyika. Naongeza maarifa zaidi kuwa Tanganyika ilitolewa kafara kwa Lucifer katika zindiko la nchi, sasa mfalme wa utukufu anakaribia kurudi ni lazima Lucifer aitapike Tanganyika apende asipende.
 
Wakati mwingine Z. Kakobe kama MTU vile........au sijui alikuwa anawalia timing waumini awachukulie Sadaka (pesa).........?
 
Kakobe aliendelea kueleza, "Mungu pekee ndiye asiyefanya kabisa makosa, lakini hakuna mwanadamu hata mmoja duniani, ambaye amewahi kuishi bila kufanya makosa (MHUBIRI 7:20). Kuna upepo unaovuma ambao unataka tuamini kwamba Nyerere hakuwahi kufanya kabisa makosa. Roho hii, ni roho mbaya sana ambayo inataka tumkubali Nyerere kuwa ni Mungu ambaye hakosei! Tusiwe kama Korea Kaskazini wasiokubali dini za Mwenyezi Mungu tunazozijua, ambao walimtangaza rasmi Rais wao Kim Il Sung kuwa mungu wao. Pamoja na kwamba Rais huyu alifariki mwaka 1994, mpaka leo anajulikana kwamba ni "Rais wa milele" wa Korea Kaskazini! - Unaweza kuangalia taarifa hizi za mungu huyu wa Korea Kaskazini, kwa ku-Google, "North Korea's cult of personality - Wikipedia". Baada ya maneno haya, Kakobe alisema kamwe hayupo tayari kumwabudu "mungu Nyerere", kisha akasema mara kumi mfululizo,"NYERERE SIYO MUNGU". Na kuendelea,"Ni kweli kwamba Nyerere alikuwa Kiongozi wa kipekee, mazuri au mema aliyolifanyia Taifa letu, ni mengi sana kwa mbali ikilinganishwa na makosa yake. Hata hivyo, alifanya makosa kadha, na mengine mabaya sana, likiwamo hili la kutuondolea urithi wa Tanganyika yetu, kinyume na mpango wa Mungu".
 
mkuu tupia audio yake fasta hawa ndo viongozi wa dini sio kina askofu mdegela na mtetema hawawezi kukemea maovu ya watawala

Comrade mdegela muache usimfananishe na mtetemela mdegela hawaogopi watawala hata siku moja nimehudhulia ibada alizoziongoza akiwasema watawala
 
Usichanganye mada utapeli wake hautuhusu sie tuko na ishu ya Tanganyika yetu hizo ishu za utapeli kuna sehemu ya kuzipeleka usituchanganyie ishu hapa!!
Safi sana mkuu, humu huwa kuna watu wapuuzi wakiona uzi unawachoma wanaanza kuleta vitu vya kipuuzi ili kuhamisha mjadala.
 
Hili suala la kuchanganya dini na siasa ambalo baadhi ya watu kwa nia binafsi wamekuwa wakilipigia kelele na ukiwauliza waeleze kwenye Biblia wapi inazuia hawakuelezi!Mbaya zaidi wanalipigia kelele kwa mtu anayesema ukweli unaowagusa wao.Askofu Kakobe angesema mambo yanayowafurahisha watawala usingesikia kabisa suala la kuchanganya dini na siasa.Wapo viongozi wa dini kadhaa wanaozungumza mambo yanayowafurahisha watawala,husikii huyu amechanganya dini na siasa!.Ifikie pahala tupende kuambiwa ukweli ili tuiponye nchi na vizazi vijavyo.Tusifurahie kudanganywa hakuwezi kulijenga Taifa.Anayedhani anaweza kumnyamazisha Askofu Kakobe kwa kauli za kusema anachanganya dini na siasa ni kupoteza muda.Kwa suala la Biblia amepewa neema kubwa sana ya Mungu ya kuijua kwahiyo huwezi kumdanganya kwa porojo hizo!Soma Biblia uone jinsi watumishi wa Mungu walivyowakemea watawala walipofanya maovu.Watanzania sio matahira hivyo mnavyodhani,wanajua ngano na makapi.Kama kuna mshirikina bado anawadanganya kwamba watanzania wataendelea kuwa mazezeta kwa uchawi wake anajidanganya nafsi yake.KILA LENYE MWANZO LINA MWISHO.

Na masheikh wa kiislam wanaamini hivyo hivyo,vita udini vibaya sana,nakumbuka yaliyotokea lebanon
 
ni -------- pekee anayeweza kuidai tanganyika ya wakoloni na kuibeza Tanzania yetu


Ndio muone sasa kufanya maamuzi ambayo yana wafanya watoto, wajukuu na vitukuu kuchukua uamuzi wa kufukua makaburi yenu kuangalia vichwani mwenu mlikuwa na matatizo gani?

Bila ya Tanganyika na Znz hamna Tanzania. Na huwezi kuwa na Tanzania inayo ipuuza Tanganyika ukafikiri uko salama, hata kama huipendi hiyo Tanganyika kwa sababu ya kumchukia mkoloni.
 
Kakobe aliongeza kusema,"Inashangaza kuona kila tarehe 9.12. tunasherehekea Uhuru wa nchi ambayo watu wengi, pamoja na Viongozi wakuu wa Taifa, wanashindwa kuitaja, na kuionea haya. Kutamka "Uhuru wa Tanganyika" kwao ni kosa kubwa. Baadhi yao wanathubutu kusema,"Uhuru wa Tanzania Bara" au "Uhuru wa Tanzania", wakati katika historia, hakuna Uhuru wa nchi hizi! Tunaposema "Tanzania Bara", je, na wakazi wa Mafia, wao nao wako Bara ipi, wakati Mafia ni Kisiwa? Upande wa pili, mambo yasiyo ya Muungano yanashughulikiwa na Serikali ya Zanzibar, sasa upande wetu, mambo yasiyo ya Muungano, yanashughulikiwa na Serikali ipi, wakati hakuna Serikali ya Tanganyika, wala Serikali hiyo ya "Tanzania Bara"????? Muungano wa namna hii siyo mpango wa Mungu, na ni Mwasisi wake tu Nyerere, aliyekuwa na uwezo wa kuushikilia, kutokana na "mamlaka yake ya ubaba, na uasisi". Yeyote ambaye siyo baba au Mwasisi, hawezi kuushikilia Muungano wenye muundo huu. Ikiwa wakati wa uhai wa Nyerere, bado kulikuwa na Tume za akina Nyalali n.k, pamoja na G55, basi nyakati za sasa moto wa kuidai Tanganyika, hakuna awezaye kuuzima. Hata Marekani hivi leo, yako mambo mengi ya Mwasisi wa Taifa lao, George Washington, ambayo yamebomolewa kabisa, na kutupwa kule!! HATA HAPA NI SUALA LA MUDA TU!!!!!!!!
 
Usiseme BISHOP KAKOBE sema SHETANI KAKOBE maana hakuna Bishop mwenye tabia chafu kama za Kakobe hilo ni jini sio Bishop
Duh, kutetea Utanganyika sasa kumebatizwa ushetani na wahafidhina. CCM, mtawatukana na kuwakana wangapi? Jaji Joseph Sinde Warioba, Jaji Augustino Ramadhani, Mwenyekiti mstaafu wa OAU Salim Ahmed Salim na waheshimiwa wote waliokuwa kwenye Tume ya Katiba, waliodiriki kusikiliza maoni ya wananchi badala ya CCM, sasa wanatuhumiwa kuwa na tabia chafu za kishetani. Mbonamasabo Job, safari hii CCM have bitten more than they can chew...subirini, hizi ni rasha rasha tu! Tanganyika inakuja mtake msitake!
 
Last edited by a moderator:
Hongera Baba Askofu ZK kwa kunena mema yanayompendeza Mungu juu ya ujio wa Tanganyika yetu.
Ni suala la muda tu fikira,akili,ari na nguvu za kuidai TANGANYIKA YETU hazitashindwa kamwe. Hatulali, haijarishi CCM na utawala wao wanatutia usingizi vipi macho yetu na sauti zenu hakika tutazipaza juu ya ujio wa Tanganyika yetu. Tupo tiari kuandika dibaji ya ufunuo mpya wa TANGANYIKA YETU hata kwa tone la damu.
Mungu ibariki TANGANYIKA na uyanyooshe mapito yetu tuangazie nuru ya haki, upendo na uzalendo tusirudi nyuma.
Natuseme AMINA!
 
Dini na siasa ni vitu viwili tafauti,ushauru wangu Askofu angalia neno la bwana acha siasa kwa wanasiasa

Kakobe hachanganyi dini na siasa kwasababu haongelei chanma cha siasa wala kugombea nafasi yoyote serekalini. Ila anachokifanya ni kutete haki za Watanganyika kuwana serekali inayo pigania haki zao. anacho kifanya ni sawa na alicho fanya Bisho desmond Tutu. Mbona Kunamashehe na maaskofu kwenye bunge la mabadiliko ya katiba?.
 
Naskia 2015 atagombea ubunge

Amerudia kauli hii ya kutotaka hata uwaziri wa kuteuliwa mara kadhaa, hana mpango huo, kazi yake ni kuhakikisha kuna usawa katika uendeshaji wa siasa ya demokrasia nchini, sio upande mmoja kumkandamiza mwingine na kusema hiyo ndiyo siasa safi. KAKOBE KUGOMBEA NAFASI YOYOTE YA KISIASA FUTA KABISA AKILINI MWAKO.
 
Asante sana baba Askofu Kakobe tunakushukuru kwa kutuelewesha kwa kutumia maandiko. Tanganyika yetu yunaipenda na tunaitaka. Mungu akuzidishie maisha marefu ili watu wamjue Yesu wajue na haki zao pia.

Na huyu mtumishi wa MUNGU Kakobe ni hazina ya taifa tuliyopewa na MUNGU.
 
hata nabii "Samuel" alikemea maovu aliyoyafanya Mfalme "Sauli",na pia Mfalme "Daudi" kutembea na mke wa mtu,alikemewa na nabii "Nathani",naye akatubu,ila "Sauli" hakutubu akafa kifo kibaya,yupo Mfalme Ahabu alifanya mabaya kwa kumuua "Nabothi",Myzreeli,Mungu akamtuma Nabii "Eliya" amkemee kwa kitendo alichofanya,baadaye naye Mfalme "Ahabu" alikufa kifo kibaya.Leo tunahitaji watumishi wa Mungu wanaosema kweli kwa viongozi,big up Mch.Kakobe na Rev.Mtikila

List ya wachungaji hambao hawamumunyi maneno kwa yeyote wakiwepo watawala wa dunia
1)Z. Kakombe
2) J Gwajima aliyesema serikali imemnyofoa kucha Ulimmboka tena wasijaribu tena kumtuma gaidi kanisani kwake kutubu.
3)C.Mtikila
4)G. Mwingira
5)Mchungaji Msigwa (Mp)
 
Usiseme BISHOP KAKOBE sema SHETANI KAKOBE maana hakuna Bishop mwenye tabia chafu kama za Kakobe hilo ni jini sio Bishop
Shetani ambaye anatenda kazi ndani yako anajua kuwa Kakobe ni mtumishi wa Mungu na hapa anafanya kile ambacho shetani na watawala wasingependa watu wajue; yaani kuziexpose kazi za shetani mojawapo ikiwa ni ya wizi wa kuliiba taifa na kulificha kuzimu, Tanganyika njoooooooooo!!!
 
Back
Top Bottom