BISHOP KAKOBE::Tanganyika Huru Lazima Ipatikane

Akaendelea kusema,"Sasa, kuondolewa kwa Tanganyika kinyemela, na kupotezwa, na kuleta habari tu ya Tanzania, ni kuondoa mipaka ya watu wa kale, na kosa hili alilolifanya Nyerere, limetusababishia laana ya KUMBUKUMBU 27:17. Laana hii ni pamoja na fedha yetu kuwa na thamani hafifu, ikilinganishwa na majirani. Nyakati za Muungano, mwaka 1964, thamani ya shilingi yetu, ilikuwa haina tofauti sana na dola ya Marekani. Shilingi yetu ilikuwa na nguvu sana kuliko fedha za majirani zetu, ikiwamo Kenya. Lakini leo, Shilingi moja ya Kenya ni karibu sawa na Shilingi 20 za Tanzania. Baada ya vita na Uganda mwaka 1978, ilikuwa ukibadilisha Shilingi chache tu za Tanzania, unapewa "gunia" la Shilingi za Uganda, kutokana na uchumi wao kuporomoka kutokana na vita hiyo. Leo 1TSh = 1.5 USh ! Mbaya zaidi, Rwanda na shida zake za mauaji ya kimbari n.k, faranga moja ya Rwanda (Rwanda Franc), ni sawa na Tsh 2.5, yaani fedha ya Rwanda ina nguvu kuliko yetu!!!???
 
waulize wachungaji wake waliomshtaki watakuambia utapeli wake.
Mmoja ya wachungaji walio mshitaki anaitwa Patrick deesdery 0755832121 huyu ametelekezwa na watawala na mara ya mwisho alifukuewa nyumbani kwa Mtikila akiwa amelewa pombe. NA BAADA YA HAPO AKAENDA NYUMBANI KWA MAMA RWAKATARE. SASA ILE KESI IMEPOTEZA MWELEKEO KWA KUWA WAMEKOSEA KUFUNGUA.

KESI HIYO NI YA JINAI KWA MAANA YA WIZI WA BILIONI 14. LAKINI WAO WAKIWA NACCM WAMEFUNGUA KESI YA MADAI JAMBO AMBALO LINATUMIWA NA CCM KUMCHAFUA KAKOBE.
 
mkuu tupia audio yake fasta hawa ndo viongozi wa dini sio kina askofu mdegela na mtetema hawawezi kukemea maovu ya watawala

Audio au video nenda pale mlangoni kwa kanisa lake wambie unataka cd ya pasaka utapewa, gharama yake haizidi 5000
 
Dini na siasa ni vitu viwili tafauti,ushauru wangu Askofu angalia neno la bwana acha siasa kwa wanasiasa

chabuso;
Angesema kuwa serekali 2 ndiyo muafaka ungemuunga mkono wala huo uongozi wake wa dini usingeli uona. Kaitamka tu Tanganyika tayari ushaanza kumtishia nyau. Kweli, majitu mengine, baasi tu.
Miye sio mfuasi wa Kakobe lakini nasema, nimempenda bure tuu. Kawafungua macho viongozi wengine wa dini. Wamuunge mkono tu.
 
Angekuwa ni sheikh ungesikia mdini huyu Lakini kwa vile ni mchungaji hamna shida.

Uelewa wako mdogo, Kakobe hakuzungumzia lolote kuhusu uislamu wala ukristu,wala kuhusisha dhulma zinazofanywa na watawala na dini yeyote ile,chuki hizo za kipepo mfuate Kakobe akawatoe au unataka kuwapunga? Wewe Boko haram nn?
 
Itabidi Askofu Kakobe amualike mh. Lukuvi ili aje abalance haya madai ya Tanganyika yetu. Itabidi watawala wetu watafute propaganda mpya, maana madai ya Tanganyika siyo ya UKAWA tu kama wanavyotaka kutuaminisha na kututishia.
Lukuvi anamuogopa Kakobe
 
Palipo na ukweli uongo hujitenga, hapa tulipofika uongo hauna nafasi tena, uwe profesor, uwe doctor, uwe askofu, uwe na cheo serikalini, uwe Rais au nani, huwezi kusimama na kuudanganya umma, na ni ukweli usiopingika kuwa Nyerere hakuwa Mungu wala maraika, alipokosea ni lazima tuseme wazi kwa lengo la kuanza upya kwa taifa letu, alipofanya vizuri hatuna budi kumpongeza, lakini kumgeuza binadamu mwenzio na kumsjudia kama mungu mtu, kutenda dhambi mbele ya Mungu, umefika wakati tuseme kweli, historia ya kweli italipeleka taifa mbele kutoka hapa tulipo, serikali mbili zimeishavunja muungano.
Mkuu, ni unafiki tu unaowahangaisha eti wanamuenzi baba wa taifa. Aliwaonya ubinafsishaji wa mashirika ya umma na hasa NBC, kupuuza sera ya ujamaa na KUJITEGEMEA na kuzika Azimio la Arusha. Mbona haya hawayaenzi kwa kumheshimu????????
 
Mzee Yusuf aliimba MIMI MZANZIBAR HALISI je sisi Watanganyika tunajiitaje kwa sasa, je tu Watanganyika halisi ama Watanzania halisi?
 
Nyie wakina abakorakamo mnaleta ubabaishaji ili kuivuruga mada iliyoko mbele yetu. Hili jambo ni la msingi sana kwetu na kwa vizazi vijavyo Tanganyika ni lazima irudi ni suala la muda tu.
 
chabuso;
Angesema kuwa serekali 2 ndiyo muafaka ungemuunga mkono wala huo uongozi wake wa dini usingeli uona. Kaitamka tu Tanganyika tayari ushaanza kumtishia nyau. Kweli, majitu mengine, baasi tu.
Miye sio mfuasi wa Kakobe lakini nasema, nimempenda bure tuu. Kawafungua macho viongozi wengine wa dini. Wamuunge mkono tu.

mkuu mimi ni mdau wa serikali tatu,Wala sina chama cha siasa,katika Sakarya hili la mungano ni CCM ndio wenye msimamo wa serikali mbili,lakini ujue kuwa katika wafuasi wa kakobe na CCM wako vile vile sasa unataka kuniambia kuwa wanachama wa CCM wamkimbie kakobe
 
Huyu baba Askofu ni wale watu wasiohongeka huyu siyo mchumia tumbo. Hata Kikwete anamjua sana ni kwamba haingiliki. Kiongozi wa dini anayeshabikia serikali dhalimu kama hii huyu sio mtumishi wa Mungu ni muuwaji, big up Bishop Kakobe.
 
Dini na siasa ni vitu viwili tafauti,ushauru wangu Askofu angalia neno la bwana acha siasa kwa wanasiasa
benegiciaries wa siasa na dini ni wale wale. Pia hakuna shida kwa kiongozi wa dini kionyesha msimamo wake wa kisiasa.
 
Amesema Tanganyika huru lazima ipatikane ni
suala la muda tu
Nchi yetu imekuwa katika laana kwa muda mrefu
kwa sababu tumeshindwa kuilinda mipaka yetu
Moto wa kudai Tanganyika umewaka na hamna
mtu awezaye kuuzima. Awaonya watawala kusoma
alama za nyakati na amewataka kuiepusha nchi
kuingia katika machafuko kwa kuridhia Serikali ya
Tanganyika.
Pia amesema Nyerere sio Mungu naye ana
mapungufu yake wanaomuabudu wanakosea.
Kosa alilolifanya Nyerere ni kuruhusu kuunda
serikali hewa ya Tanzania bara ambayo kimsingi
haipo ukiliganisha na Zanzibar.
Amewaonya viongozi wanaopinga kurejeshwa
kwa Tanganyika kuwa wataitumbukiza nchi katika
machafuko.
...Hizo zilikuwa salamu za Pasaka alizozitoa leo
katika kanisa la FGBF Dar es salaam.

Kakobe alishawahi kusema unafiki ufuatao!
(1) Mwaka 2000 alisema Lyatonga Mrema ndie chaguo la "mungu" na ndie rais ajae WA Tanzania. [Ukweli ulionekana na Mrema alishindwa vibaya mno na mkapa]

(2) Aliiambia serikali ikiwa nyaya za umeme zikipita juu ya kanisa lake basi hazipitisha umeme. [ukweli Ni kwamba nyaya zilipita na umeme umepita juu ya kanisa lake].


Kusikiliza utabiri WA Kakobe Ni sawa na kusikiliza Utabiri wa PELE wa Brasil.

KAKOBE ACHA KUTOKWA NA MAPOVU!
 
Ikiwa ulichoandika ni sahihi, unadhani ni kwa nini ndani ya bunge la kutunga katiba limejuisha maaskofu, mashehe na wachungaji kutoka dini na madhehebu mbalimbali??? kwanini wasingeachwa ili katiba itungwe na wanasiasa pekee????

Kwasababu tanzania ni nchi ya dini nyingi,sasa unataka na askofu wa pentakosa nae awahamasishe wafuasi wake serikali moja na wa katoliki nae aje aseme wafuasi wake lazima wapatiwe serikali nne,nk

na waislamu zehebu la Sunni lisime wao wanataka sehemu zote zenye waislam wa zehebu la Sunni wanataka raisi wa zehebu la Sunni,na wale waislam wa shia waseme jengine.........

mkuu unafikiri tutakuwa na nchi hapo,kakobe awaachie wenye kazi zao za siasa wafanye mambo kwa taaluma yeye mwache akae kanisani atukuze neno la bwana
 
Back
Top Bottom