Binti wa Keenja kortini kwa dawa za kulevya

Patrick Nyemela

JF-Expert Member
Nov 25, 2008
332
26
MTOTO wa aliyekuwa Waziri wa Kilimo Bw. Charles Keenja, Bi. Aghata Keenja ameburutwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala akikabiliwa na makosa ya kukutwa na dawa za kulenvya kinyume cha sheria.

Mshitakiwa huyo alifikishwa mahakamani hapo jana na kusomewa mashitaka mbele ya Hakimu wa Wilaya Bi. Janeth Kinyage.

Bi. Keenja anatuhumiwa kwa makosa ya kupatikana na dawa za kulevya kinyume cha kifungu 12(d) cha sheria ya kuzuia na kupambana na dawa za kulevya.

Alidaiwa kuwa Oktoba mosi, mwaka huu katika mtaa wa Makunganya, Dar es Salaam alikamatwa na gramu 6.6 za dawa ya kulevya aina ya Heroini yenye thamani ya sh. 60,000. Hata hivyo mshitakiwa huyo alikana kutenda makosa hayo na upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

Mshitakiwa huyo aliiomba mahakama kumpatia dhamana ambapo ilimtaka kuwa na wadhamini wawili wa kuaminika ambao watasaini dhamana ya sh. 500,000. Alitimiza masharti ya dhamana na kesi yake itatajwa tena Novemba 2 mwaka huu.
 
Alidaiwa kuwa Oktoba mosi, mwaka huu katika mtaa wa Makunganya, Dar es Salaam alikamatwa na gramu 6.6 za dawa ya kulevya aina ya Heroini yenye thamani ya sh. 60,000. Hata hivyo mshitakiwa huyo alikana kutenda makosa hayo na upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

Hivi mahakama imejuaje kuwa hayo madawa yanauzwa kwa bei hiyo iliyotajwa?
 
Wacheni wafu wazike wafu wao yaani gm 1 9000 nani kawadnganya waje kinondoni
 
Huo uzito ni mdogo sana na ni kupoteza wakati na pesa ya serikali, kupeleka shitaka kama hili mahakamani kwa sababu kama mshtakiwa ni mjanja anaweza sema hii ni kwa matumizi yake binafsi. Hapa ilikuwa wamng'ang'anie awaelekeze nani amempa haya madawa ama amenunua kwa nani? The focus should be on big fishes and not small fish kama kweli tunataka kupambana na hili tatizo la madawa.
 
Hakuna mwenye interest hiyo; nani anataka kupiga risasi mguu wake mwenyewe? Lol!
 
Hawa watoto wa Keenja wana matatizo gani hawa....tulisikia Eliaisa....na sasa mdogo Mtu Agatha...........Amani Mkuu wangu....sijui na wewe tutakusikia na lipi....lol
 
Oyaa wakuu at least I am close to the person in question and her family and this is what I am reliably informed:

Huko ofisini kwake anakofanya kazi (She's a lawyer for a credit facilities company-jina kapuni) kuna supplier flani alikuwa terminated service yake kutokana na uzembe na kutokuabide as per contract.Baada ya hapo akaenda mahakamani na Agatha akaenda kuidefend kesi jamaa akashindwa kesi.

Huyo supplier hakufurahishwa na hicho kitendo. Anyway baada ya hapo wakawa wakikutana na Agatha na wanazungumza vizuri tu. Lakini kumbe mshikaji alikuwa na kinyongo....

Of recent Agatha alikuwa anauza gari yake na huyo jamaa akasikia kwamba Agatha anauza gari. Hiyo juzi akampigia simu Agatha akamwuliza vipi nasikia gari yako unauza ni kweli? Agatha akasema ndio nauza, basi huyo jamaa akaja na watu akasema ni wateja. Agatha akampa dreva wao funguo akamwambia wapeleke washikaji wakaicheki gari wakiipenda waje tuzungumze bei.

Dereva akawapeleka halafu baadae wakarudii wakasema gari wamaeipenda. Wakakubalia terms na baadae wakamwambia ziko wapi original docs? Agatha akasema zipo home ila nitazileta kama mko tayari kununua basi kesho warudi ili naye a draft mkataba na wao waje na hela ili transaction ifanyike.

Hao jamaa wakaondoka kwa makubaliano hayo. Walipoondoka tu wakaja watu ofisini kwa Agatha wakasema tuna suspect gari yako ina madawa ya kulevya.

Basi wakamchukua yeye na mfanyakazi mwenzie wakashuka chini na wakamwambia ingiza mkono chini ya seat ya dereva toa kilichopo kuingiza na kutoa basi wakakuta huo Unga.

Can see how fishy this was??????? Anywayz the truth will be revealed. Kama kuna mtu anadhani has some other facts to prove otherwise anaweza pia kuziweka hapa.

My take: Tujitahidi kutofautisha facts na opinions.
 
Kama binadamu wanaweza kuwa na roho mbaya kwa sababu tu ya kutokwepesha ukweli, sasa huyo jamaa kataka kumkoa huyo mdada kwa kuwa alikuwa mkweli katika kesi yake. Dah inauma sana kusingiziwa kitu, hata hivyo si kila unayecheka nae ni rafiki yako, wengine ni maadui kama huyo mshkaji aliyemfanyia kitu mbaya huyo mdada na kumuharibia jina lake katika jamii. hope mungu atamsaidia mdada na atashinda hiyo kesi ya kusingiziwa
 
Its so sad maana ninavyofahamu mabinti wa Keenja na kaka zao akiwemo Amani- wamelelewa katika familia nzuri yenye maadili.Ni watu wastaarabu sana na sidhani Agatha angeweza kujishughulisha na madawa ya kulevya -tena gram 1 ya 9,000/-!
Ukweli utajidhihirisha tu.
Poleni the Keenjas!
 
Oyaa wakuu at least I am close to the person in question and her family and this is what I am reliably informed:

Huko ofisini kwake anakofanya kazi (She's a lawyer for a credit facilities company-jina kapuni) kuna supplier flani alikuwa terminated service yake kutokana na uzembe na kutokuabide as per contract.Baada ya hapo akaenda mahakamani na Agatha akaenda kuidefend kesi jamaa akashindwa kesi.

Huyo supplier hakufurahishwa na hicho kitendo. Anyway baada ya hapo wakawa wakikutana na Agatha na wanazungumza vizuri tu. Lakini kumbe mshikaji alikuwa na kinyongo....

Of recent Agatha alikuwa anauza gari yake na huyo jamaa akasikia kwamba Agatha anauza gari. Hiyo juzi akampigia simu Agatha akamwuliza vipi nasikia gari yako unauza ni kweli? Agatha akasema ndio nauza, basi huyo jamaa akaja na watu akasema ni wateja. Agatha akampa dreva wao funguo akamwambia wapeleke washikaji wakaicheki gari wakiipenda waje tuzungumze bei.

Dereva akawapeleka halafu baadae wakarudii wakasema gari wamaeipenda. Wakakubalia terms na baadae wakamwambia ziko wapi original docs? Agatha akasema zipo home ila nitazileta kama mko tayari kununua basi kesho warudi ili naye a draft mkataba na wao waje na hela ili transaction ifanyike.

Hao jamaa wakaondoka kwa makubaliano hayo. Walipoondoka tu wakaja watu ofisini kwa Agatha wakasema tuna suspect gari yako ina madawa ya kulevya.

Basi wakamchukua yeye na mfanyakazi mwenzie wakashuka chini na wakamwambia ingiza mkono chini ya seat ya dereva toa kilichopo kuingiza na kutoa basi wakakuta huo Unga.

Can see how fishy this was??????? Anywayz the truth will be revealed. Kama kuna mtu anadhani has some other facts to prove otherwise anaweza pia kuziweka hapa.

My take: Tujitahidi kutofautisha facts na opinions.
Nyambala, umeandika as if ni mimi nimeandika. Nilifuatilia baada ya kuisikia hii issue lakini nilichoambulia ni hiki ulichoandika juu. Amechezewa rafu mbaya ambayo imetokana na uzembe wa kumwamini mtu ambaye tayari alikuwa amemjengea chuki (huenda yeye hakujua).

It's obvious rafu hii imepangwa kabisa maana gharama ya madawa yenyewe ni ndogo sana kulinganisha na credibility yake Agatha. Ati 60,000/=? Give me a break!

Inahitaji akili ndogo sana, polisi waliotumika kwenye mchezo huu wanatakiwa kuchukuliwa hatua za kinidhamu kwani huu mchezo inaelekea umeandaliwa na wamehusishwa huku wakiona wazi kuwa ni deal la kumchafua.

Watanzania wengi wanachezewa hivi, kesi za kubambikizwa na polisi wapuuzi wenye dhamira ya kula rushwa na kusahau wajibu wao kazini. Nasubiria kuona kama haki itatendeka!
 
Pole Agatha, yote haya ni mambo ya kiswahili watu wanaendekeza. Haki siku zote husimama.
 
Back
Top Bottom