Recta
JF-Expert Member
- Dec 8, 2006
- 855
- 38
Mkuu Nyambala, ulichokisema ndicho kilichotokea. Ama kweli unamfahamu Agatha vyema. Nashukuru kwa kujitokeza mapema na kuweka ukweli hapa jamvini.Oyaa wakuu at least I am close to the person in question and her family and this is what I am reliably informed:
Huko ofisini kwake anakofanya kazi (She's a lawyer for a credit facilities company-jina kapuni) kuna supplier flani alikuwa terminated service yake kutokana na uzembe na kutokuabide as per contract.Baada ya hapo akaenda mahakamani na Agatha akaenda kuidefend kesi jamaa akashindwa kesi.
Huyo supplier hakufurahishwa na hicho kitendo. Anyway baada ya hapo wakawa wakikutana na Agatha na wanazungumza vizuri tu. Lakini kumbe mshikaji alikuwa na kinyongo....
Of recent Agatha alikuwa anauza gari yake na huyo jamaa akasikia kwamba Agatha anauza gari. Hiyo juzi akampigia simu Agatha akamwuliza vipi nasikia gari yako unauza ni kweli? Agatha akasema ndio nauza, basi huyo jamaa akaja na watu akasema ni wateja. Agatha akampa dreva wao funguo akamwambia wapeleke washikaji wakaicheki gari wakiipenda waje tuzungumze bei.
Dereva akawapeleka halafu baadae wakarudii wakasema gari wamaeipenda. Wakakubalia terms na baadae wakamwambia ziko wapi original docs? Agatha akasema zipo home ila nitazileta kama mko tayari kununua basi kesho warudi ili naye a draft mkataba na wao waje na hela ili transaction ifanyike.
Hao jamaa wakaondoka kwa makubaliano hayo. Walipoondoka tu wakaja watu ofisini kwa Agatha wakasema tuna suspect gari yako ina madawa ya kulevya.
Basi wakamchukua yeye na mfanyakazi mwenzie wakashuka chini na wakamwambia ingiza mkono chini ya seat ya dereva toa kilichopo kuingiza na kutoa basi wakakuta huo Unga.
Can see how fishy this was??????? Anywayz the truth will be revealed. Kama kuna mtu anadhani has some other facts to prove otherwise anaweza pia kuziweka hapa.
My take: Tujitahidi kutofautisha facts na opinions.
Inatakiwa tuwe makini na watu wenye visa kama hao wanafikia hata kumbambikizia mtu madawa ya kulevya kama ilivyotokea kwa Agatha. Itafika wakati tutaacha kuaminiana ili kuokoa heshima na kuwa salama zaidi. Ni wengi sana wanaopatwa na masahibu kama hayo.
Swali ninalojiuliza ni; Je, walikuwa na nia nyingine zaidi ya hiyo endapo wangefanikiwa kukutana nae? Maana kuna mifano ni mingi ya watu kuuawa, kumwagiwa tindikali n.k.