Binti (miaka 19) amepotea, naomba msaada kwa atakayemuona

ELIMU PESA

Member
Jul 22, 2017
62
36
Habari ndugu zangu.

Ninaomba msaada, binti huyu ninaambatanisha picha zake amepotea tangu tarehe 27/08/2023.

Binti huyu anaitwa Antia Focas, nyumbani walizoea kumuita Nyakato. Ana umri wa miaka 19. Mkazi wa Mkundi Morogoro, japo ana miezi mitatu tu tangu ahamie mkundi, mwanzoni tulikuwa tukiishi Kihonda-Maghorofani. Mimi ni baba yake mdogo, nimekuwa nikiishi naye kwa muda wa miaka mitatu sasa tangu nimtoe kwa wazazi wake.

Niligundua kuwa amepotea tarehe 27/08/2023 muda wa saa 7:30 (saba na nusu) mchana, hii ni kwa sababu alikuwa akimpeleka mtoto shule alafu anapitia kujifunza cherehani, ikifika saa sita na nusu anakwenda shule kumfata mtoto, wanarudi nyumba muda wa saa 7:30. Siku hiyo ilifika muda huo hajarudi, ilipofika saa nane na nusu tukapiga simu shuleni na kugundua kuwa hata mtoto alikuwa hajachukuliwa pale shuleni, shule inaitwa WESLEY.

Tulipopiga simu kwa mtu aliyekuwa akimfundisha cherehani, alisema kuwa alifika tu asubuhi, akaaga kuwa anakwenda saloon, kuosha nywele na kusuka. Tulipofatilia saloon, tukaambiwa kuwa hakufika. Tulitoa taarifa katika kitua cha polisi cha Kihonda, tukaambiwa turudi baada ya masaa 48 kama hajapatikana, tuliporudi tukapewa RB namba na kuambiwa tuendelee kumtafuta.

Bahati mbaya hadi leo hatujampta, alikuwa na simu lakini tangu apotee haipatikani. Pengine ni rahisi kufikiri kuwa labda katoroshwa na mwanaume, lakini mazingira aliyoondoka yatia shaka, kwani hakubeba kitu chochote. Hakubeba hata nguo moja wala mkoba. Naomba msaada wenu kwa atakayemuona.

Simu 0766729127/0688746145.

Asanteni.

IMG-20230831-WA0086.jpg
IMG-20230831-WA0097 (1).jpg
IMG-20230831-WA0098 (1).jpg
RB.jpg
 
Pole sana mkuu, ILA hawa police ni piece of shit, why wasubirie 48hrs?,hii sheria ya wapi?nchi hii kweli ni pithole one,mtu akiwa potea, police wanatakiwa waanze muda huo huo kumtafuta, 48 hrs ameshavuka hizi porous borders zetu ndio maana jeshi la police nitalivunja na all above 40 yrs nitawapa marching order, leta vijana wapya wenye ari mpya
 
Back
Top Bottom