Utajiri/pesa ndio kiu inayowatesa watu wengi sasa

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,514
Habari wakuu,

Niende moja kwa kwa moja kwa mada..

Nionavyo sasa, kuna upepo unaovuma, upepo huo ni wa kila mtu anataka awe tajiri, yaani awe na pesa mingi.

Kiu ni kubwa ya watu kutaka kuwa matajiri yaani wenye pesa kuzidi wengine, yaani pesa inasakwa sana.

Ajabu ni kuwa pesa nayo imekimbia haipatikani kwa haraka, watu wanalazimisha njia mbalimbali ili wapate.

Watu wanawaza wafanyeje ili waweze kutoka kimaisha, iwe kazi halali au hata isiyo halali bora liende.

Si wanaume tu yaani hata wanawake kila mmoja anakiu awe tajiri.

Vijana ndio kiu hiyo imekuwa kali sana maana wanawaza kuwa matajiri kwa namna yeyote Ile.

Tena vijana ndio wamevurugwa mbaya mbovu, yaani wako tayari kwa lolote bila kujali utu wao ili wawe matajiri.

Manabii feki nao wamezuka nao wanatangaza wanatoa utajiri, ni kama wanacheza na kiu ambayo watu wengi wamekuwa nayo.

Wameshaijua kiu hiyo ya kutaka kuwa matajiri, basi nao wanatumia kama fursa kuwadanganya wajipatie pesa.

Kila uchao Manabii wa mchongo wanaongezeka ilimradi wamejua ndio njia pekee ya kujipatia utajiri.

Ikumbukwe Manabii feki nao wapo katika lile lile kundi la kusaka utajiri kwa namna yeyote bila kujali lolote.

Waganga feki nao wanazidi kuongezeka wakaifanya utapeli wao kwa lengo la kujipatia utajiri, kiu hiyo.

Utajiri/pesa inatafutwa sana ...
 
Ni kweli. Hata Natafuta Ajira anashusha vinu vya nyuklia sababu ya uhaba wa pesa
 
Back
Top Bottom