Road map 2024 Kwa Vijana: Kuwa Mtu katikati ya Binadamu

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,900
ROADMAP2024 Kwa Vijana: Kuwa Mtu katikati ya Binadamu.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Unaweza ukajiuliza kwa nini katika sensa za zamani Wanawake hawakuchukuliwa kama Watu. Hata katika Biblia tunaona Yesu akilisha Watu(wanaume) elfu tano huku wanawake na watoto wakiwekwa kando. Jambo hilo halikufanyika kwa bahati mbaya.

Hukohuko kwenye Biblia na Quran wakati Mungu anaumba ulimwengu. Akasema aumbe mtu kwa mfano wake na aliyeumbwa ni Mwanaume. Pia jambo hilo halikufanyika kwa bahati mbaya.

Kihistoria, Watu wa baraza ulàya walipokuja Afrika walisema Waafrika sio Watu ila ni mifano ya watu. Wengine waliokosa staha wakatuita manyani. Nalo halikufanyika kwa bahati mbaya.
Na hicho ndicho tutakachoenda kukijadili katika andiko hili ambalo kimsingi nimeliweka liwe ndio Roadmap ya Vijana kwa mwaka 2024.

Binadamu ni kiumbe kama walivyo viumbe wengine. Lakini Mtu ni zaidi ya kiumbe. Mtu anauungu ndani yake. Uungu huo ndio uitwao "UTU"
Binadamu mwenye uungu ndio huitwa Mtu.

Sitaki kukuchosha wala sitaki nami kujichosha.
Mtu ni mkamilifu lakini binadamu hajakamilika. Kwa sababu Mtu aliumbwa na Mungu na chochote kilichoumbwa na Mungu ni kikamilifu. Ila binadamu hàkuumbwa na Mungu isipokuwa alizaliwa na Mtu.
Mtu ni upungufu wa Mungu, na binadamu ni upungufu wa mtu.
Mtu ni mfano wa Mungu na binadamu ni mfano wa mtu.
uungu unaishi ndani ya mtu. Utu unaishi ndani ya binadamu.
Mtu pasipo Uungu huitwa binadamu. Binadamu mwenye uitwa Mtu.
Mtu hafi/hapatwi na mauti lakini binadamu anakufa(anapatwa na mauti).
Tuachane na falsafa.

Mtu ili akamlike atahitaji mambo makuu yafuatayo;
1. Nafsi hai
2. Utashi
3. Utawala na Mamlaka.

Mwaka 2024 ni mwaka wa wewe kuwa Mtu.
Baada ya kuzaliwa wewe huitwa binadamu lakini ukishakuwa mkubwa utachagua kuwa binadamu au kuwa Mtu. Ni maamuzi yako tuu.

1. Nafsi Hai
Binadamu ni nafsi hai. Lakini hiyo haimaanishi yeye ni mtu. Uwepo wa nishati ya Uhai(roho) mwilini mwako ndiko kunakufanya uitwe nafsi hai.

2. Utashi.
Uwezo wa kuchagua mazuri na mabaya. Mema na maovu. Kuhisi hatia pale unapotenda kosa. Kuhisi kupongezwa pale unapofanya mazuri. Uwezo wa akili kupambanua mambo, kuyachunguza, kuchambua, kutathmini, kudadisi, kutatua matatizo. Yote ni sehemu ya utashi ambao ni sehemu muhimu ya Utu.
Binadamu akishakuwa na utashi huitwa mtu. Kinyume chake hn tofauti na mnyama.

3. Utawala na Mamlaka.
Hapa ndipo kwenye kamzozo.

Sifa kubwa ya mtu ni kujitawala na kutawala mazingira yake mwenyewe. Kiumbe kinachojitawala na kutawala mazingira yanayomzunguka kiumbe hicho huitwa Mtu.
Binadamu asiyeweza kujitawala au kutawala mazingira yake moja kwa moja anakosa sifa ya kuitwa mtu.

Kujitawala kunaendana sambamba utashi wa mtu, upeo wa akili na maarifa aliyonayo mtu.
Huwezi kuwa mtawala kama huna Akili.

Katika kujitawala na kutawala mazingira ambapo ndio Utu wenyewe ambapo ndio akili yenyewe kuna kitu kinaitwa SHERIA.
Hakuna utawala au Mamlaka bila sheria. Hakuna Utu bila sheria.
Mtu huweka sheria ili azifuate na zimuongoze katika kujitawala na kuyatawala mazingira yake.

Binadamu huweka sheria ili azivunje na asizifuate. Huweka sheria ili awakandamize wengine na sio kuwaongoza na kujiongoza yeye mwenyewe.

Katika kujitawala kuna kujitegemea ili kuwa huru. Mtu lazima ajitegemee na awe huru kwa sababu anaakili na anakutawala na kuyatawala mazingira yake.
Kujitegemea kutamfanya binadamu afanye kazi ya kujihudumia na kulinda mazingira yake na wahusika wake.
Kazi ni kipimo cha utu. Mtu lazima aishi kwa kufanya kazi.
Kazi ni nyenzo ya utawala na mamlaka. Kujitegemea.

Huwezi kuwa na utu kama hujitegemea. Kama wewe ni tegemezi moja kwa moja wewe sio mtu.

Mtu hanunuliwi kwa sababu ya utu wake. Ndiko kujitegemea, akili na kujitawala.
Binadamu ananunulika kwa sababu yeye ni kama viumbe wengine. Ni kama mbuzi, ng'ombe, Bata n.k.

Wanawake zamani walinunuliwa kwa sababu wao hawakuwa Watu. Kwa kile kiitwacho Mahari biashara ya kuuza wanawake ilipamba moto.
Mwanamke akishakuwa mtu huwezi kumnunua kwa sababu Watu hawanunuliwi.
Sio ajabu wanawake wengi kwa vile sio Watu hawaoni shida kujiuza kwa namna moja ama nyingine.
Binti za Tibeli ni Watu ndio maana Baba yao ninawaambiaga lazima wafanye kazi na wajitegemee. Kumtegemea binadamu mwingine ni zaidi ya kujidhalilisha. Jitegemee, ili uwe mtu.

Ikiwa unahitaji kuheshimiwa na kuheshimika sharti uwe Mtu. Linda utu wako ili uheshimiwe.

Kwa mtu kuuzwa au kujiuza ni aibu, fedheha na unyanyasaji. Kwa aab6ya utashi na akili ya mtu. Lakini kiumbe kama binadamu hakioni shida kuuzwa kama Kuku. Kwa sababu utashi wake umezimia, haoni kama yeye kulinganishwa na Ng'ombe sio tatizo.

Mwaka 2024 ni mwaka wa kuhakikisha binadamu wanaona utu wako. Wanakuona kama mtu.

Sio wanawake tuu. Hata baadhi ya wanaume wapo ambao sio Watu. Kuuzwa au kujiuza kwao sio tatizo.

Kujitegemea ni kuwa huru. Kujitegemea ni kuwa mtu.

Mtu hufuata Ukweli, haki, upendo, akili na maarifa.

Binadamu yupo after material ( Materialists) Kwa sababu anatawaliwa na vitu. Lakini mtu yupo kwa ajili ya utu na ndio maana huyatawala mazingira.

Binadamu atakuthamini kwa kigezo cha vitu kama mali, pesa n.k. lakini mtu atakuthamini kwa kigezo cha tabia yako.

Mwaka 2024 kuwa mtu.

Na huwezi kuwa mtu pasipo kuwa na Uungu ndani yako. Lazima ufuate sheria na amri za Mungu ili uwe mtu.
Kufikia hapo nakutakia mwaka mpya mwema. Katika kufikia ndoto ya kuwa Mtu.

Ni yule shahidi kutoka Nyota ya Tibeli.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Back
Top Bottom