kilimasera
JF-Expert Member
- Dec 2, 2009
- 3,068
- 268
KAMBI Rasmi ya Upinzani Bungeni imetangaza vipaumbele na mwelekeo wa bajeti ijayo ya mwaka 2011/12 ambapo na fkutangaza kuunda kitengo maalum cha kushughulikia mafisadi wkubwa anaolalamikiwa na wananchi
Kambi hiyo imetaja vipaumbele sita katika bajeti hiyo ambavyo ni miundombinu, umeme, kuwezesha ukuaji wa sekta za uzalishaji na ukuaji wa uchumi vijijini, maendeleo ya rasilimali watu, utawala bora pamoja na kuimarisha usimamizi wa mashirika ya umma.
Vipaumbele muhimu vya kambi hiyo imeadhimia kufuta posho za vikao
kwa lengo la kupunguza matumizi ya serikali, ikiwemo na kupunguza misamaha ya kodi kutoka asilimia 4.5 hadi asilimia moja.
Lingine ni kukuza elimu nchini na kuhakikisha bodi ya mikopo ya elimu ya juu inapata fedha za kutosha kutoka kwenye kodi ya uendelezaji ujuzi
Ikiwemo na kuanzisha bima ya afya kwa wananchi wote ambayo itakuwa ni ya lazima kwa wafanyakazi na wasio wafanyakazi ambayo itachangiwa na wananchi pamoja na serikali.
Bajeti hiyo itafafanuliwa na kuwasilishwaji na Waziri Kivuli wa wizara ya Fedha na Uchumi Bw. Zitto Kabwe .