Bima ya afya ni lazima kwa kila mwananchi - Bajeti upinzani

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
266
KAMBI Rasmi ya Upinzani Bungeni imetangaza vipaumbele na mwelekeo wa bajeti ijayo ya mwaka 2011/12 ambapo na fkutangaza kuunda kitengo maalum cha kushughulikia mafisadi wkubwa anaolalamikiwa na wananchi
Kambi hiyo imetaja vipaumbele sita katika bajeti hiyo ambavyo ni miundombinu, umeme, kuwezesha ukuaji wa sekta za uzalishaji na ukuaji wa uchumi vijijini, maendeleo ya rasilimali watu, utawala bora pamoja na kuimarisha usimamizi wa mashirika ya umma.

Vipaumbele muhimu vya kambi hiyo imeadhimia kufuta posho za vikao
kwa lengo la kupunguza matumizi ya serikali, ikiwemo na kupunguza misamaha ya kodi kutoka asilimia 4.5 hadi asilimia moja.

Lingine ni kukuza elimu nchini na kuhakikisha bodi ya mikopo ya elimu ya juu inapata fedha za kutosha kutoka kwenye kodi ya uendelezaji ujuzi

Ikiwemo na kuanzisha bima ya afya kwa wananchi wote ambayo itakuwa ni ya lazima kwa wafanyakazi na wasio wafanyakazi ambayo itachangiwa na wananchi pamoja na serikali.

Bajeti hiyo itafafanuliwa na kuwasilishwaji na Waziri Kivuli wa wizara ya Fedha na Uchumi Bw. Zitto Kabwe .
 
let us go men,peoples powerrrrrrrrrrrr bajet ni kwa maslay ya wa tz wote lisimamieni hilo.
 
Ukitoa bima ya afya kwa watanzania wote, vifo vingi sana visivyo vya lazima vijijini na mijini vitapungua kwa asilimia kubwa sana. This is a fact.
 
CDM tupewe serikali tuiendeshe na turudishe hadhi ya Tanzania...Peeepooooooooooooooooooooooooooooz!!
 
Ukitoa bima ya afya kwa watanzania wote, vifo vingi sana visivyo vya lazima vijijini na mijini vitapungua kwa asilimia kubwa sana. This is a fact.

Hamna kitu hapo ni siasa, wekeni na vyanzo vya mapato ili tujue serikali yenu bandia itakuwa na hizo pesa, au ni bajeti ya kujitafutia umaarufu wa kisiasa kama siku zote mfanyavyo
 
CDM tupewe serikali tuiendeshe na turudishe hadhi ya Tanzania...Peeepooooooooooooooooooooooooooooz!!

Sasa fursa hiyo mlipewa 2010 mkashindwa , jaribuni labda labda 2025, kwani kwa sasa wananchi walio wataka kuongoza dola ndio wako madarakani
 
bima ya afya haiwez kuwa lazma kwa kila mwananchi kwa miaka ya karibuni..hapa kuna watu wafanyakazi wanakatwa bimaya afya na hawajapewa vitambulisho mwez wa tano sasa na kwa hali hiyo hawajaanza kutumia huduma ingawa wanalipia....na hao ni asilimia ndogo sana ya wananchi, je ikiwa nusu tu ya wananchi si itachukua miaka 50 kupata vitambulisho?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom