bill za bar!

Nadhani bar inayoongoza kwa kuchomekea aina hii ya bill ni nguruko mbezi beach, siku ya kwanza nilidhani kakosea kweli, siku ya pili, na mara ya tatu the same, nikaona kumbe ndo ujanja wao, hawanipati tena, cm iko na kikokotozi
 
Last Sunday Pale Njiro complex jamaa walinibambika bill zaidi elf 13500.Nilipoenda nao sawa wakaanza bisha,nikawaomba waje na maneja wao,uwezi amini wakaja na bill ya ukweli nikalipa nikaenda zangu.Dar ndio kiboko unaweza pewa bili ya mpaka Amarura wakati wewe unakunywa Konyagi
 
Hata ningekua mimi lazimi niipitie hii.. na Huyu jamaa alokupa hii bill ni bonge la kiazi how comes unamchomekea bill mtu hata tone la konyagi kichwani hana.. Maana sioni bia hata moja
 
sio kwamba hatushtuki ukikuta bar maid mzuri unakaushia tu kama noti zipo nyingi mfukoni.kuna day tulikuwa tunasherekea birthday ya mshkaji mitaa fulani hapa a-town tukaletewa bill ya laki moja na thelathini.watu tukazama mifukoni,kabla ya kutoa mademu zetu wakaja juu,mtalipaje bili bila kuikagua fresh?e bwana kupiga mahesabu kitu kinafika 70 tu.mademu walileta noma mpaka manager akamfukuza baa medi.
 
duh... nusu kuku na ndizi tatu kwa watu wawili?? na kuku zetu ndio zile za wiki sita??

aisee....
 
Mimi kila raundi huwa na lipa!!! i don't wait for final calculation ....yalishawahi nikuta pale usa river sitaki kurudia tena makosa hayo
Uzuri wa calabashi(mwenge) lipa nd uhudumiwe mambo ya bili hakuna...
 
Back
Top Bottom