Bilicanas imarisheni ulinzi

Man kama unajijua kwamba huwezi kuzi hande bia kwanini uende na laki nane club? Kwanza bia nane tu zinakulewesha sasa kwanini usingeenda na sh 20000 hata zikipotea hujutii sana! Mi sometimes nalewaga kupita kiasi so naachaga HTC simu yangu ya laki 7 nachukua ka samsung ka 30000 na nshawahi kukapoteza nikanunua kengine, iliniuma lakini haikuuma sana, ingeuma sana kama ningepoteza HTC. Sometimes tunajifunza kwa makosa yetu wenyewe so nadhani sasa utajua cha kufanya kuanzia sasa. Kumbuka: Jambo lililokutokea in the past haimaanishi litakutokea tena kama ukiwa proactive.
 
Halafu sidhani kwamba baunsa wa club ana jukumu la kukulinda wewe binafsi, yeye analinda usalama inapotokea vurugu au mtu asiingie na silaha club. Tafuta bodyguard akulinde, tena una laki nane unaweza kumlipa!
 
sheria ya wizi na ubakaji

Hivyo ulibakwa pia?

Huwezi kumshitaki mtu utathibitisha vipi uliingia na hivyo vitu ? ulionyesha mlangoni ? tena una bahati kuna vijana pale wangedai we ndugu yao wanakupeleka nyumbani baada ya kukunukisha madawa ya kulevya,na kuishia kukuoa bila mahari wala sherehe.

Mkuu hilo pia walimtenda, sema hawakuwa na haja ya kutoka naye nje..
Labda atakuwa amejifunza kunywa pombe kulingana na uwezo wake siku nyingine..
 
Ijumaa iliyopita niliamua kuwatembelea baada ya kusikia sifa zenu. Kwa kweli nilichokutana nacho ni matatizo ya hali ya juu. Baada ya kupiga ndovu nane niliamua kujipumzisha counter na kupitiwa na usingizi. Baada ya kuamka nilijikuta sina laki nane zangu, sina saaa na blackberry yangu ikawa imenitoka. Kama mnataka kupata wateja basi jaribuni kuimarisha ulinzi, vinginevyo mtapoteza wateja wenu hivihivi

Du! Laki nane night club? Unekoma kama ungekuwa Jolly Club. Halafu inaonekana wewe kichwa cha panzi, bia nane unazimika? Mwanamme anakata hadi ishirini na anarudi nyumbani salama. Ungeanzia break point na supu ya kuku.
 
Ringi hawakukwiba?
 
labda unaona laki nane ni nyingi saaaana kwasababu mshahara wako haufiki laki 6
 
Hata mimi nimeshangaa bia nane tena tule tu ndovu mwanamme ? nakifahamu kabinti 22yrs kanakunywa Safari za moto 10-12 na kanatufunga pool na hakapepesuki wala nini.
 
Ijumaa iliyopita niliamua kuwatembelea baada ya kusikia sifa zenu. Kwa kweli nilichokutana nacho ni matatizo ya hali ya juu. Baada ya kupiga ndovu nane niliamua kujipumzisha counter na kupitiwa na usingizi. Baada ya kuamka nilijikuta sina laki nane zangu, sina saaa na blackberry yangu ikawa imenitoka. Kama mnataka kupata wateja basi jaribuni kuimarisha ulinzi, vinginevyo mtapoteza wateja wenu hivihivi

na huu ni upuuzi,kwani kwenda/kutembelea billcanas_kunywa ndovu nane_kuibiwa laki nane_saa na simu nako ni u-celebrity,...pumbafu kama vp peleka huu upuuzi fb
 
labda unaona laki nane ni nyingi saaaana kwasababu mshahara wako haufiki laki 6

Laki nane ni nyingi mno kwenda nazo club kwa kigezo chochote kile. Weka laki mbili kwenye waleti, laki moja ya kununulia mchuchu na nyingine ni vinywaji (na kadi ya ATM) standby kama unaishiwa labda umekutana na kampani. Hiyo blue nakusahihisha, kipato changu kwa mwezi hakifikii hata laki mbili unusu ndo maana nashangaa, hiyo laki nane kwetu unanunua ng'ombe wawili wa kienyeji.
 
sheria inasema ulipoingia club ulikuwa na buku tatu na nokia ya tochi bila kusahau ulikuwa tayari umeshalewa kibuku na ulivuta bangi ambayo ilikupelekea kuona nokia ya tochi kuwa blackberry na buku tatu kuwa laki nane!

khaaaaaaaaaaa!!!!!!!
 
Babu wee maisha yenyewe haya magumu, umejinywea mibia yako kichoyo alafu umesasambua kila kitu...kwanini wenye njaa tusichukue chetu mapema?? au ulitaka tukuamshe alafu tukukumbushe kuchunga mali zako? tena ushukuru ulijikuta hapo hapo club hujafanyiwa madhara dhidi ya ubinadam ungejikuta gesti asubuhi bila ch***p
 
Mkuu ki ukweli umenivunja mbavu!!! Hiii kali sanaaaa!!!! watu wengine ni wa ajabu sana pale posta kuna ATMs kibao za karibu benki zote yet bado mtu anaingia club na laki 8 huku hawezi ku manage unywaji wake!!!
sheria inasema ulipoingia club ulikuwa na buku tatu na nokia ya tochi bila kusahau ulikuwa tayari umeshalewa kibuku na ulivuta bangi ambayo ilikupelekea kuona nokia ya tochi kuwa blackberry na buku tatu kuwa laki nane!
 
Acha na mimi nijipe fagio.
Ebana kweli pale Bills ulinzi ni hafifu sana.
Kuna siku nilienda pale nikapaki Vogue yangu ambayo niliijaza mafuta full tank.
Kumbuka hapo nilitoka kudroo vilaki tano ambavyo nilichanganya na zile laki saba zilizo kwenye wallet zikawa kama 1.2M.
Kwenye akaunti nilibakisha kama 50M.
Baada ya kuingia nikaagiza wine kumbe badala ya kutoa noti ya elfu10 kumbe nikatoa noti3 nikizani ni moja tu.
Yule mhudumu hakuniambia.
Da! pale Bils sio kabisa.
 
Nickie+-+Dreaming+Drunkard.jpg
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom