Bila ushiriki wa UKAWA kwenye BMK, hakuna Katiba Mpya!

Ndugu wanajamvi tumeshuhudia tunaendelea kushuhudia jinsi nguvu kubwa inavyotumika kuwashawishi UKAWA kurudi bungeni,na kwanini nguvu Kama hiyo isitumike kuwashawishi CCM wakubali kujadili rasimu ya warioba?
 
Mkuu hata mimi nilijiuliza sana swali hilo na nikabahatika kupata jibu,ni kuwa hao wote wanaojifanya kuishinikiza ukawa kurudi bungeni kujadili rasimu haramu ya ccm ni misukule ya ccm,ukawa hawakutoka tu bungeni kama vichaa,ila walionyesha kwa uwazi mapungufu yaliyoko upande wa ccm na vibaraka wake kutaka kui derail rasimu halali na waweke ya kwao,sasa ukawa tatizo lao linaeleweka,wanataka tu ccm iheshimu rasimu halali,ni zipi sababu za ccm kuikataa rasimu halali?
 
Mkuu hata mimi nilijiuliza sana swali hilo na nikabahatika kupata jibu,ni kuwa hao wote wanaojifanya kuishinikiza ukawa kurudi bungeni kujadili rasimu haramu ya ccm ni misukule ya ccm,ukawa hawakutoka tu bungeni kama vichaa,ila walionyesha kwa uwazi mapungufu yaliyoko upande wa ccm na vibaraka wake kutaka kui derail rasimu halali na waweke ya kwao,sasa ukawa tatizo lao linaeleweka,wanataka tu ccm iheshimu rasimu halali,ni zipi sababu za ccm kuikataa rasimu halali?
 
ccm hawako tayari kujadili rasimu ya warioba kwa sababu:- kwanza, kama inavyojulikana wazi, maslahi ya mafisadi na wahafidhina ndani ya ccm yanatishiwa mno na rasimu hiyo; pili, kwao ni rahisi kuchakachua matokeo ya kura za maoni, hivyo ni salama kwao katiba itakayopendekezwa na bunge iwe ya kulinda maslahi yao tofauti na ikiandikwa yenye muelekeo wa rasimu ya warioba. ndiyo maana wanatumia nguvu nyingi kijadiliwe kitu tofauti na kupitishwa kwa kura ya wengi; tatu, kwa kuwa ukawa tayari wamewawahi na kutangaza hila za ccm kwa wananchi wanatumia mbinu zote hizi vitisho na kubembeleza ili ukawa warudi na ccm jamii iwaone ukawa vigeugeu na kwamba ccm hawakukosea chochote. wanaogoka ukawa wakiendelea kususia bunge hilo, basi hila ya ccm itadhihirika wazi.
 
Makelele yamekuwa mengi, katiba mpya ,katiba mpya ,na had ukaletwa mdahalo unaouliza ni nani anawazuia Watanzania kupata Katiba mpya?

Nataka nitoe rai yangu na Mimi bee hee ( maana kila wa tu saiv wapo Bize kutoa matamko ,hata kama hayo matamko mengine wanatoa ni yale waliyotamkiwa ili wayatamke)

Binafsi nahitaji katiba mpya bora ,siyo tu katiba mpya. Sababu unaweza kuwa na kitu kipya lakini kisiwe kizuri na bora. Na naona kabisa kuwa hiki ndo kitu ambacho watanzania wengi wenzangu na mimi wanahitaji ,japo wengi baadhi katika hawa wanaweza rubuniwa na kupumbazwa kutokana na shida, umaskini na ujinga wa ,lakin hiki ndicho wengi wanachotaka.

Hatutaki tu kuingia mwaka 2015 na katiba mpya No! Tunataka kuingia mwaka 2015 na katiba bora ambayo itachochea yafuatayo.

1. Uwajibikaji Kwa viongozi na wananchi wote

2. Ukuzaji wa uchumi na Huduma bora Kwa wanajamii

3. Mgawanyo mzuri wa madaraka ,ambao utawezesha kuwe hakuna mtu (individual) ambaye yupo juu ya sheria ,kuchochea umoja na mshikamo na usimamizi bora wa utajiri wa taifa hili .

4.katiba ambayo italeta mfumo bora wa checks &balances na kuleta hali ya usawa kati ya walionacho na wasionacho.

Hii ndo katiba mpya na bora nayoingoja ,kama itabid ichelewe ili ije hii ni bora Mara elfu kuliko iwahi ,halafu iwe haina mashiko .

Kama unaungana nami kutaka katiba bora na siyo tu katiba mpya, tafadhali ungana nami ,paza sauti, comment ,like ,sambaza ujumbe .

Na watu wote wajue kuwa si katiba mpya tu tunayoihitaji Bali ni katiba itayosolve changamoto za kiuchumi ,kijamii na kisiasa tulizonazo sasa na tunazoweza kuwa nazo baadae

"Nimeshindwa kunyamaza na mimi nimetoa tamko " Pinno 2014.
 
Mimi nimeandika uzi kama huu umenyofolewa fasta. Kumbe kwenye hili jukwaa Ukawa wananguvu sana! Haya time will tell.
 
mi naamin tatizo kubwa la kutokupatikana kwa muafaka ni ukawa kwa kuwa wanaendekeza ubinafsi bila kujal maslah ya nchi

We Papu Chii acha unafiki. Suala hli la katiba ccm walidhani wananchi ni wale wale wa enzi za Mwalimu, akiongea yeye ni agizo la Mungu. Kumbe wametaamaki serikali 3 na mambo yake hayo wakachanganyikiwa. Baada ya hapo wakaanza kulishana viapo vya kufa kwa kupandikiza serikali 2 na ku2plia mbali Rasimu ya Jaji Warioba na kumdhhaki na ma2c kbao. Sasa kwann ccm wang'ang'anie kura ya wazi na serikali 2 uoni kama wao ni tatizo?
 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
*Asema malumbano ya viongozi hayawasaidii wananchi
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda ametoa saa 30 na kutaka kupatiwa majibu ni kwa nini maelekezo aliyotoa kuhusu kiwanda cha kusindika nyama cha Mbeyahayajafanyiwa kazi.
Ametoa kauli hiyo leo mchana (Ijumaa, Agosti Mosi, 2014) wakati akizindua Kongamano la siku tatu la Uwekezaji la Mikoa ya Iringa, Njombe na Mbeya lamwaka 2014 ambalo limeanza leo kwenye ukumbi wa Benjamini Mkapa jijini Mbeya.
“Mbeya inaweza kuwa na fursa kubwa ya viwanda vya usindikaji nyama, unga wa mahindi ili kuongeza thamani ya mazao mnayozalisha katika mkoa wenu.Nilipokuwa hapa ziara yangu ya mwisho 2012, niliagiza kiwanda hiki kitafutiwe mwekezaji ili kianze uzalishaji. Jana nimeuliza kiwanda cha nyama kimefikiawapi, naambiwa watu bado wanaongea. Wanaongea nini?,” alihoji.
“Mtu akija kusikia habari ya kiwanda hiki atatuona ni wajinga tena ni wajinga wa kujitakia, kisa watu bado wanazungumza… hiki kiwanda cha nyama ni chaMbeya na manuafaa yake ni kwa ajili ya wana Mbeya. Hivi wahusika ni kwani hamuioni hiyo fursa?” alisema.
“Dk. Mary Nagu watafute watu wa CHC waje hapa kujieleza ni kwa nini suala hili limechukua muda mrefu. Kabla sijaondoka hapa Mbeya kesho natakanipate majibu kuhusu jambo hili,” aliagiza.
Katika hotuba yake ya ufunguzi, Waziri Mkuu alisisitiza suala la watendaji wa mikoa na wilaya kuchukulia kwa umakini suala la uwekezaji kwani wasipofanyahivyo wao ndiyo watageuka kikwazo na kukwamisha maendeleo ya wananchi wanaowaongoza.
“Ndugu zangu wa Serikali za mitaa msiwe vikwazo, kuwezi wawezeshaji. Ninyi si watawala bali ni waleta maendeleo kwa jamii. Natoa wito mshirikiane nawafanyabiashara kuharakisha maendeleo ya wananchi mliokabidhiwa kuwaongoza. Acheni kudai hongo, kwani badala ya kuwasadia jamii, mtajikuta ninyi ndomnakuwa vikwazo vya maendeleo,” alionya.
Alisema Serikali za Mitaa zinapaswa kuwa wawezeshaji na siyo wakwamishaji wa masuala ya maendeleo na ili kufanikisha hilo aliwataka wakuu wa mikoawaanzishe one-stop centre katikangazi ya mkoa na Halmashauri ili wawekezaji wanapofika katika mikoa yao wasizungushwe na kukatishwa tamaa kwa sababuya mlolongo wa taasisi zilizopo.
“Uzoefu unaonyesha kuwa baada ya kufanya makongamano kama haya, wawekezaji wengi wanajitokeza lakini katika ngazi ya Mkoa na Halmashauriwanakosa mahali ambapo wanaweza kushughulikiwa na kupata huduma bora kwa pamoja “One Stop Centre”. Hali hiyo huwafanya wakate tamaa.”
“Ninashauri kila Mkoa na kila Halmashauri iweke mfumo mzuri wa kuwapokea wawekezaji hususan kuwa na Mratibu (Focal Point) wa masuala ya uwekezajiambaye ndiye atakuwa “One Stop Centre” wa kushughulikia wawekezaji wanaojitokeza na kuwahudumia kwa ufanisi bila urasimu. Ni imani yangu kuwatukifanya hivyo, tutawezesha Kanda hii kuwa kitovu kikubwa cha uwekezaji katika nchi yetu,” aliongeza.
Alisema kila mmoja hana budi kuendelea amani na utulivu wa nchi ili uwekezaji uweze kufanikiwa na kushamiri. “Hakuna uwekezaji endelevu na wenye tijakatikati ya fujo na migogoro, na uwekezaji utashamiri pale tu penye amani na utulivu,” alisisitiza.
Mapema, Waziri wa Nchi (OWM-Uwezeshaji na Uwekezaji), Dk. Mary Nagu alisema ili uwekezaji uweze kuwanufaisha wananchi, ni lazima rasilmali za nchizigeuzwe kuwa bidhaa. “Ukiangalia chuma cha Liganga kipo pale miaka mingi, bila kukigeuza kuwa bidhaa, bado hakiwezi kuwanufaisha wananchi wetu,”alisema. Alisema bila uwekezaji hakuna uchumi, na bila uchumi hakuna maendeleo na bila maendeleo hakuna maisha bora kwa kila Mtanzania.
Katika hatua nyingine, Wakuu wa mikoa ya Mbeya, Iringa na Njombe walipewa nafasi ya kuzungumza na washiriki wa kongamano hilo ikiwa ni pamoja nakuelezea fursa mahsusi zilizomo kwenye mikoa yao.
Mada zitakazowasilisha katika kongamano hilo ambalo kaulimbiu yake ni “Maendeleo ya Kiuchumi na Kijamii katika Nyanda za Juu Kusini” zinahusu fursaza uwekezaji katika sekta za uchumi na miundombinu katika kanda hiyo, fursa za uwekezaji katika sekta za huduma za jamii katika kanda hiyo, fursa zauwekezaji katika kilimo cha mazao ya bustani (matunda, mboga, maua na viungo) na mchango wa taasisi za fedha katika uwekezaji.
Nyingine ni mchango wa sekta binafsi katika uwekezaji, na nafasi ya MKURABITA katika kukuza mitaji ya uwekezaji.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
IJUMAA, AGOSTI MOSI, 2014
 
Katiba ni mkataba na mkataba ni maridhiano. Maridhiano kati ya CCM na Ukawa ndi hivyo yameshindikana.
CCM wanaenda sasa kuandika katiba yao peke yao. Tukitazama mika 10-20 ijayo hii inaliweka wapi taifa?
 
Kumbe na hiyo hoja hapo juu inahusiana na ukawa? Kuna haja ya kuongeza madaraja NECTA/NACTE kuwe na Div 7
 
bado majadilianao yanaendelea TULIZA MAHABA
SIKU WAKI STEP IN NA KUJADILI WAKIWA WENYEWE

NDO UJE ULETE HIZI PUMBA HAPA
 
Na waandike tu! Wanataka wabembelezwe kama tunawataka ndiyo warudi bungeni??!. No time to waste.
 
MaCCM watahangaika sana lakini mwisho wa siku watarudi kwa wananchi kuwaomba radhi kwa kukanyaga maoni yao.
 
Teh teh, kumbe maslahi ya nchi ndo maslahi ya ccm? Maana kwa ccm maslahi ya chama kwanza, pili maslahi ya mafisadi, na tatu maslahi ya nchi! Ccm wamepuuza waziwazi maslahi ya umma!

CCM wamejisahau sana. wanadhani kwamba zama hizi ni za chama kushika hatamu na kudumisha fikra za mwenyekiti. huku kujisahau kwao ndiko kutawafuta kabisa kwenye ramani ya siasa za tanzania.
 
If there had been none sense dreams are those of CCM about the possibility of getting new constitution without
UKAWA.
 
Back
Top Bottom