Bila UMAFIA hujawa tajiri bado. Umafia ndio dira ya utajiri

Abrahamovich nafaham umafia wake na Rafiki yake Putin. Bill Gates sifahamu chochote mi nilidhani amepitia njia za kawaida tu bila makandokando yoyote, kwani ana tuhuma gani?
Inadaiwa hata hio idea ya window iliibwa kwa bwana Steve jobs
 
Inadaiwa hata hio idea ya window iliibwa kwa bwana Steve jobs
Uongo mwingine huu hapa. Bill Gates akishirikiana na Paul Allen na wengine walitengeneza OS ya computer (windows), Steve Jobs, akishirikiana na Steve Wozniak na wengine walitengeneza Computer (Mackintosh).
 
Sasa umebadili wimbo, siyo "umafia" tena?

Kijana hakuna utajiri wa namna hizo, utajiri ni mawazo yako tu.

AlhamduliLlah Uislam unafundisha namna kuwa utajiri, wanaofata njia hizo wanatajirika tu, hakuna cha kuwazuwia.

Kwanza ni lazima uelewe, kuwa tajiri siyo kuwa na pesa zisizokuwa na kazi.
Kwamba waislam masikini wanaupenda sana umasikini kiasi cha kutotaka kuzifuata hizo njia?

Watu wa dini bado mnaishi zama za kitumwa sana.
 
Nani kakuambia umafia wa matajiri utausikia direct??
...umafia wa watu wenye fedha nyingi upo very technical!!!
Utaishia kusikia za juu juu tu, na mengine ya kimafia huwezi kuyasikia popote hata kama mhusika ni mtu wako wa karibu kiasi gani, iwe ni mtu wa smile kila wakati, moyo wa huruma n.k!!
Sasa kama umafia wa matajiri umekua ni siri hivyo, Nyinyi mmejuaje takwimu za matajiri ambao ni mafia ?

Hadi mkaja na hitimisho ili uwe tajiri lazima uwe mafia.

Mmepataje takwimu za jambo ambalo mnakiri ni siri sana ?
 
Qur'an 2:261. Mfano wa wanao tumia mali zao katika Njia ya Mwenyezi Mungu ni kama mfano wa punje moja iliyo chipuza mashuke saba. Katika kila shuke zimo punje mia. Na Mwenyezi Mungu humzidishia amtakaye, na Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa na Mwenye kujua. 261
Wewe umepata utajiri kiasi gani kwa kutumia hii mbinu?
 
Uongo mwingine huu hapa. Bill Gates akishirikiana na Paul Allen na wengine walitengeneza OS ya computer (windows), Steve Jobs, akishirikiana na Steve Wozniak na wengine walitengeneza Computer (Mackintosh).
Waliotengeneza program za macrosoft za Bill Gates ni Indian mathematics professors na Gates kwa ajiri 40% wahindi so ni mjanja mjanja tu
 
Back
Top Bottom